Maisha yangu ya ndoa ni tofauti na nilivyoyatarajia

Pole mkuu ila bado una nafasi ya kusahihisha kwanini ufe na tai shingoni kama umezaliwa nayo
Mhh. Kwa wengi wetu kujinasua hapo ni mtihani mkubwa sana ujue. Utawahusisha ndg., familia/ukoo, jamii, mhakama na kisaikoljia. Mwisho wa siku Unajiuliza na kutafakari - yooote hayo ya nini? Bora tu nikubaliane na matokeo nikomae na hali yangu.
 
Mifumo ya ndoa ya namna hiyo haifai yani ukikosea huwezi kujisahihisha

Endelea kupambana mkuu huenda akabadilika
 
Kaza roho humu ukileta jambo lako😊Kuna mbwa ziko humu zinaweza kukuongezea pressure🙌uliweka matarajio makubwa kwa mtu ambaye humjui na ulidhani unamjua, jitahidi kufanya kadri ya uwezo wako, kwa afya Yako, usitumie nguvu kumfurahisha mwanamke(mkeo),akiona humuwezi mpe uhuru(Linda akili Yako),jipende kwanza. Cha msingi ukitaka kurejesha amani yako na uwe na amani hapo ndan jifunze kumpuuza mwanamke,zingatia neno kumpuuza usitoke nje ya lane😃...maisha haya Yana step,, kikubwa tafuta namna hata kufuga kuku hutokosa vihela vdg vdg.chukua👍
 
Mwee! Usishangae tena hata ivo vihela vdg vdg. (vya kuwinda kwa manati) ukastukia vimetumika kuendea saluni. Sshyeee!
 
Fanya hivyo mkuu ila usichelewe sana - Fanya maamuzi hata kama ni maamuzi magumu.
Mkuu wew ni mwenyekt wa kataa ndoa nni ,

Mnatak mfungue file la kataa ndoa la mwanacham mpya
 
Kabla ya kuoa, nilidhani ndoa ni chanzo cha furaha na baraka. Nilitarajia amani na utulivu, lakini ukweli umekuwa tofauti kabisa. Nimegundua kwamba changamoto za ndoa zinaweza kukuletea presha kubwa, hasa unapokuwa na kipato cha chini.

Kipato kidogo kimekuwa chanzo cha migogoro isiyoisha. Mahitaji ya nyumbani ni mengi, na mara nyingi mapato hayatoshi. Matokeo yake ni msongo wa mawazo, mabishano, na lawama zisizo na kikomo. Nilipokuwa peke yangu, nilikuwa na uwezo wa kujipanga na kufurahia maisha kwa kipato kidogo. Lakini sasa, inaonekana kama haitoshi hata kwa mahitaji ya msingi

Zaidi ya hayo, nilitarajia mke kuja na upendo, ushirikiano, na msaada. Badala yake, nimejikuta kwenye presha ya kukidhi matarajio ambayo ni vigumu kuyafikia kutokana na hali ya uchumi. Wanawake wengi wanatarajia waume zao wawape kila kitu bila kujali hali halisi ya kipato. Hili limeongeza msongo wa mawazo na kunifanya nipoteze amani ya moyo na hata afya yangu imeanza kudorora.

Kabla ya ndoa, nilikuwa na uzito wa kilo 68 na presha yangu ilikuwa 120/80. Sasa, uzito umeshuka hadi kilo 59 na presha imepanda hadi 130/81. Hii yote ni kutokana na presha ya maisha ya ndoa na kutokuwa na amani ya akili.

Nimejifunza kuwa kuoa kwa kutegemea kwamba mwanamke ataleta baraka au neema ni kujidanganya. Badala ya baraka, nimekutana na changamoto na presha zisizo na mwisho. Ni wazi kwamba bila kipato cha kutosha na ushirikiano wa kweli katika ndoa, maisha yanakuwa magumu sana.

Ndoa inahitaji zaidi ya upendo; inahitaji uvumilivu, ushirikiano, na uelewa wa hali halisi ya maisha. Bila haya, ni rahisi kugeuka kuwa chanzo cha laana badala ya baraka.
Chai
 
Waapi bhana!. Si nilijitumbukizamo ndoani sasa imeshakuwa ni Ndoano.
 
Pole

Kwa unayopitia kaka.pole
 
Pole sana mkuu. Umeandika changamoto inayokumba wengi ila kipato na uelewa kutofautiana ni jipu
 
Back
Top Bottom