Maisha yangu ya ndoa ni tofauti na nilivyoyatarajia

Hao viumbe wakitaka hela wanajua ipo tu na kama haipo ni kama watoto utatupiwa lawama zote zilizo chini ya jua
Hao viumbe itoshe tu kusema HATA UNGEMPA NINI; HAWATOSHEKI.
Kwa wale walio ndani ya ndoa watatoa uzoefu wao hapa. Mwanamke kabla ya ndoa utamwona anajiremba, msafi, lugha nzuri na ya sauti ya chini, hakasiriki hovyo i.e. muda wote anapendeza; anamvuto. Mkifunga ndoa tu baada ya ndoa e.g. mwezi mmoja hata pengine mwezi haupiti..utaona: Sauti kubwa, mahitaji na matumizi ya kijinga-jinga e.g. hichi silagi mie, naumwa hapa au pale, naenda kusalimia fulani, nimejiunga vikoba na leo kuna kikao, umeme & maji wanataka malipo yao n.k. Ukimshauri labda aibue na aanzishe kamradi fulani amazing atakuuliza mradi gani?? utasikia unanidharau n.k. ww ni mbishi sana etc. Kwa mantiki hiyo; ndoa ni mapambano na ni mtihani endelevu wa kudumu.
Na cha kushangaza zaidi ni kwamba unatunukiwa cheti hata kabla ya kumaliza kozi.
 
Kumbe hata nzi akitulia anaweza tengeneza asali ? Leo umetema madini sana mkuu , kongole kwako.
 
Hukuchagua vizuri
Wewe unaishi maisha ya ndoa au umeshaishi na mwanamke/mwanaume kinyumba zaidi ya miezi 6? (Sio wale unaoa jioni asbh. mnaachana hapana. Hiyo sio ndoa).
Hakuna hata mtu mmoja hapa duniani anayeishi maisha ya ndoa atakuambia alichagua vizuri. Kila ndoa ina KASORO zake na CHANGAMOTO zake..
 
Basi umeangukia pua
 
Basi umeangukia pua
Sawa. Basi, kama yupo aliyefanya vizuri kwenye hilo, wewe utakuwa ni wa kwanza na ni wa kutolea mfano. Otherwise ur a unique person or unmarried dude.
 
Umeandik kwa uchache lakn umemanisha Ndoa kwa upana wake na kwa mtazamo wake katika karne hii tunayoishi ,

Hayo tunaptia mengi , mi najiapang kuhamia mkoani , nitahudumia familia nkiwa mbali maan ukiwa karbu shda ukiw mbali shida ila nmeona ukiw mbali bora utarud utavyojisikia na utaondok utapo choka
 
Ndoa inahitaji pia mwanamke amheshimu mumewe
 
Mkuu; Hauogapi kwamba utakuwa umejisogeza karibu zaidi na upande wa lile kundi la Kataa ndoa?
 
Sawa. Basi, kama yupo aliyefanya vizuri kwenye hilo, wewe utakuwa ni wa kwanza na ni wa kutolea mfano. Otherwise ur a unique person or unmarried dude.
Duniani pair zipo tafuta pair yako utaipata
 
I bet mke wako anavaaa mawigi mda wote, ana shepu na tako, anatumia mkorogo alaf ni much know. Pole sana
 
Ishi nao kwa akili.
Bado Kuna wanawaqke wema na wacha Mungu.
 
Shida ni kwamba vigezo vya msingi katika kuoa tunaviepuka tunafuata chura la mwanamke. Matokeo yake ndio tunaoa wanawake hawana akili hata ya kujiongoza wao wenyewe achilia mbali kuongoza watoto.
Hapa ndipo penye tatizo,vijana hawazingatii kuoa kwa kuangalia mwanamke ana siha gani wanachoangalia wao amebinuka vipi na akikatiza nae mitaani watu macho yanawatoka?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…