Maisha yangu ya ndoa ni tofauti na nilivyoyatarajia

TAFUTA HELA MKUU. Hata nje ya ndoa wanahitaji matunzo. Jipange mkuu
 
Pole sana kiongozi, wakati mwingine tunachagua watu wasiofaa au tunadanganyana wakati wa mahusiano na kujidhihirisha hali zetu baada ya kuoa.

Tatizo lenu litazidi kukua kwa sababu ya frustrations za kila upande (nafikiri mkeo pia hana furaha juu ya hiyo migogoro isiyoisha)

Ushauri:
  1. Jitahidi mkeo apate shughuli ya kiuchumi ya kujitengenezea kipato (hata kama ni kwa mkopo) itasaidia kuondoa utegemezi kwenye hiyo hela yako ndogo ambayo tayari haitoshi.

  2. Kaeni pamoja mtengeneze bajeti ya familia na kuhakikisha matumizi yote ya msingi kama kodi, chakula n.k yako kwenye hiyo bajeti.

  3. Kua muwazi kwenye mambo ya fedha, muonyeshe mkeo unapata kiasi gani na kinatumika vipi, ili naye aielewe hiyo changamoto ya kipato na kuondoa lawama zisizo za lazima.

  4. Afya yako ndiyo mtaji wako uliobaki, kuwa makini na zingatia afya ya mwili na akili. Kula vizuri kadri utakavyoweza na tafuta activity ya kukufurahisha kama michezo n.k

  5. Zungumza na wanaume wenzako walio kwenye ndoa, fedha na mambo ya kiuchumi ni sababu kubwa sana ya migogoro. Washirikishe wakupe ushauri pia, baada ya hapo za kuambiwa changanya na zako.

    All the best!
 
Hata uwe na kipato cha kutosha bila upendo, uaminifu, uvumilivu, ushirikiano na uelewa; ndoa huwa ngumu pia. Utajiri au kipato kikubwa hakijawahi kuwa dawa ya ndoa,. Kupendana, kuaminiana na kuvumiliana jinsi mlivyo ndiko hudumisha ndoa.
 
Maisha ni kuchagua chagua kile kinachoendana na wewe sio kufanya show off mwisho wake ndo haya
 
Kataa ndoa wanakucheka kwa dharau.
 
Expectation Vs Reality=Reality Win
 
Pole
 
pole san kwa kuchelewa kujua ukwel,ndoa ni baraka kwa maelezo ya dini lkn ni magum san hasa pale ukiwa na kipato cha chin kibaya zaid uwe na mwanamk mweny akil km njugu mawe aseh utajuta kuoa utakuta limwanamk linagubu,kisirani,kiburi hajui km unahela ya hauna yeye ni "anataka umpe hela" wallah ni shida sana kwa kwel.

Ndio maana huwa nawashaur vijana wenzangu ambao hawajao b4 inabid mtangulize san Mungu wako atleast umpate kichaa mwenzako mweny hofu ya Mungu,uvumilivu wa kimaisha mengine mtavumilian tu kiubinadam
 
Pole na hongera. Mko wawili tu au mna mtoto?
Kama mko wawili tu, tafuta siku muelekeze kuhusu uwezo uliopo. Kubalianeni vitu gani mviondoe katika bajeti, kitu gani kifanyike kuongeza kipato kidogo.

Panga nae plan za muda mrefu kwa kuandika ndani ya miaka kumi unataka ufike nae wapi. Wakati mnapanga hayo mpe nafasi yeye ndio awe anaongea sana.

Hapo utakuwa unaisoma na akili yake pia kama mtakuwa pamoja au la.
 
Mimi siyo mganga ila mke wa mtoa mada ana Tako kubwa alafu anatamaa ya vitu vikubwa, ila mwanetu hivo vikubwa Hana na kuachia Tako liende hataki. Ngoja tusubirie part2
😁😁😁😁
 
Watoto wa mtume wanakuona fala tu.
Mkuu punguza mawazo, jikaze kiume, mwanajeshi anafia vitani.
 
We wanawake kumbe huwajui wewe
 
We wanawake kumbe huwajui wewe
Hawa viumbe hakuna anaewajua vizuri, unachotakiwa ni ku probe ili ukitoa hitimisho liwe na mantiki.

Hamna wakati huwa naweza kumuangamiza mtu kama wakati ninaompa muda wa kuongea sana, wengi huwa wanajishtaki ukiskiliza vizuri.

Ndio maana nikasema amwache mwanamke ndio awe anaongea sana... ili aone kama kuna haja ya kuendelea nae. Jamaa anaweza kulalamika hivyo kumbe mambo mengi anafanya kichwani na moyoni,mwenzake anakuwa anaona kama hakuna kinachofanyika anabaki njia panda.
 
Apo mkuu mkeo lazma ugongewe na watu au ujaona izo dalili?
 
Mwanamke kwenye Ubongo wake na Akili zake hakuna msamiati unaoitwa SINA au VUMILIA.

Ukitaka Amani, tumia akili nyingi sana kwenye kuweka baadhi ya hustle zako private ili mwisho wa siku akigundua akuheshimu. Mwanamke anakutesa kwasababu anhisi bila yeye haupindui
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…