Kabla ya kukujibu hayo naomba kwanza ukaisome Bibilia yako vizuri ujuwe imetoka kwa Mungu au kwa binadamu kama wewe. Biblia hizo mashuhuri zimetengenezwa na binadamu, hili ni jambo la ajabu sana.
Kisha ujiulize je kuna Qur'an tofauti zilizo tungwa na binadamu? Ukapata jibu ambalo si la kukatalika hakija tungwa na mtu. Kwani vitabu hivi na baadhi ya makala zingine ni chanzo cha mafundisho ya dini ya kikristo wanayo yategemea. Ukiwa una soma biblia zote hizo nne unajuwa takuta nini? Biblia ya Matthew inasema nini kuhusu Yesu inasema yafuatayo; Nabii Issa (Yesu) anatokana na kizazi cha Ibrahiim na Daud. kwa hiyo ni nani huyu Yesu? Si katika binadamu? Kweli yeye ni binadamu. Biblia ya Luka inasema; Anamiliki nyumba ya Yaqub milele, na hakuna mwisho wa milki yake. Biblia ya Mark inasema; Hii ni sababu ya family ya Jesus wanauko wa ki Mungu (Yesu)mtoto wa Mungu. Biblia ya Yohana inasema; Mwanzo ilikuwa ni neno,na ilikuwa ni neno kwa Mungu, lilikuwa neno la Mungu, na maana yake ni kwamba; Mwanzo alikuwa Yesu,na Yesu wa Mungu na Yesu ndie Mungu. Aisay hapo ukijiuliza katika nafsi yako, kuna tofauti kubwa katika biblia hizi nne kuhusu Yesu. Je yeye ni binadamu au mtoto wa Mungu au Mfalme au yeye ni Mungu. Na uhakika utakuwa una shaka kuhusu suala hili,wala usipate jibu lake. Sabubu ni uwongo mtupu:A S wink:
Kuhusu swali lako nadhani tumeisha kuelezeni sana humu Mitume wote wa Mungu wao walikuwa waislam, na walisali wapi kila mmoja alikuwa akisali kwa kufata Mungu wapi wanatakiwa waelekeze uso wake. Lazima watu wafahamu ya kuwa uislamu si dini iliyopewa jina na muasisi fulani na kusema kuwa wafuasi wake waitwe waislamu, isipokuwa Uislamu jina hili ukilitafsiri kwa lugha y kiswahili ni amani, kujisalimisha, kunyenyekea ndiyo maana yake. Mtume Muhammad si muanzishaji wa dini hii, na amelezea wazi kuwa uislamu mana yake (kujisalimisha kwa Mungu) toka kuumbwa kwa ulimwengu. Allah aliumba ulimwengu ili vitu vyote vimtii na kujisalimisha kwake, lakini viumbe hawa wawili (majini na watu) walipewa khiari na matamanio, na huo ndiyo mtihani wenyewe tulioumbiwa nao, ambao watu tunaelekezana, kuelimishana, kujadiliana, kuzozana mpaka tunafikia hata kugombana na kutoana roho katika mambo hayo. Watu walioishi mwanzo walikuwa na mfumo wao wa maisha, walipewa muongozo wa kuishi na Mungu, kwa kuwapelekea mjumbe kutoka kwake. Vitabu vya dini havipingani kabisa kuwa Adam na Hawa(Eva) walipewa muongozo na Allah na kuambiwa wasiukaribie mti huo walioukatazwa, kwa kuwa walikuwa na khiari na matamanio ndiyo yaliyowafanya wapinge sheriai hiyo na kutokea yaliyotokea. Kwa kuwa walikuwa wanyenyekevu, wakaomba msamaha na mwisho wakasamehewa, siyo kama Ibilisi(Shetani) ambaye hakuwa mnyenyekevu na kuangamia. Watu wasifikirie Uislamu ni dini ya Mtume Muhammad na kwa ajili ya warabu tu. Ukisoma historia ya kiislamu utumkuta Bilal (R.A) muadhini wa mtume ambaye alikuwa Mhabesh(Mu Ethopia), tunamsoma Salman Farsi (R.A) ambaye ni Mfarsi(Muiran), kuna wakina Bukhari watu kutoka sehemu za Urusi na Mayahudi wengi tu waliosilimu. Mtume aliifikisha dini hii kwa wafalme wengi tu wa pande za ulimwengu. Kwa hiyo Uislamu ulikuwepo kutoka kumbwa kwa dunia na mpaka mwisho wake. Dini nyingine huenda zilikuwa ni za usahihi kutoka kwa Allah ila baada ya kupita muda baadhi ya watu waliharibu dini hizo ikiwa kwa ujinga au maslahi yao binafsi haswa huyo Paulo mtume wawakristo. Ikiwa Allah kaumba ulimwengu na vilivyomo ndani yake hivyo hahitaji chochote kutoka kwetu, isipokuwa unyenyekevu wetu tu, na huo ndiyo Uislamu wenyewe. Na kitu kikubwa usamfananishe Mungu na kitu chochote hapa utakuwa umeingia kwenye madhambi makubwa mno hayana toba. Na huo ndiyo ulikuwa ujumbe wa Mitume wa Mungu. Uislamu si jina la mtu au sehmu au kitu, sipokuwa ni kitendo cha mtu kujisalimisha, kumnyenyekea Mungu na kufata mfano wa Mitume wote wa Mungu ambao walikuwa wakimtii Mungu, sijawahi kuona Paulo kamtii Mungu zaidi ya kuwapoteza binadamu wasimtii Mungu. Hasa hio ya kumfananisha Mungu kawa Binadamu. Paulo alimpa sifa hii Yesu kwa sababu moja kubwa; Alitaka kupata wafuasi wengi miongoni mwa Warumi na Wagiriki (watu wa mataifa). Wajentaili (Wagiriki na Warumi) walikuwa ni wapagani waliokuwa wakiabudu miungu wengi wenye historia ndefu iliyojaa imani za ajabu ajabu zisizokuwa na hoja wala dalili za kiakili. Miungu wengi wa kipagani wa wakati ule - Mithrus, Adonis, Attis na Osiris ndio kawaingiza kwenye dini yake mpya ya kikristo. Ya Mungu baba, Mungu mwana, na Mungu roho mtakatifu Poleni sana wakristo.