Tetesi: Majadiliano ya Makinikia: Tanzania inapumulia mashine

Sitegemei Mtanzania mwenye akili timamu asherehekee sisi kupoteza katika majadiliano yanayoendelea.
ni lazima ieleweke kwamba, pamoja na kwamba mikataba na sheria zinatubana lakini hawa jamaa wametuibia sana sana sana. Wametuibia kwa kushirikiana na Watanzania. Hivyo juhudi zozote zinazofanywa na serikali kurekebisha dosari hizi lazima ziungwe mkono sambamba na ku recover kiasi fulani cha fedha ambazo tulikuwa tunaibiwa kwa kutumia sheria zetu wenyewe.
Hovyo kabisa. Yaani Bunge linaenda kutunga sheria eti Mchanga ni mali ya Accasia wakati kwenye mchanga kuna dhahabu na madini mengine lukuki. Bunge letu limekuwa likipofushwa macho kila uchao na hawajifunzi hawa jamaa wazee wa mihemko na kupiga meza.
Nina mashaka na lile la Tanzanite kama litakuwa na Jipya maana kamati iliyoundwa kuchunguza imeundwa na hawa hawa wazee wa mihemko na kupiga meza. Siju Credibility yao ikoje.
Inakera sana kutufanya watu wengine tuanze kuhoji credibility za vyombo muhimu kama hivi hasa katika michakato yao ya kufana maamuzi kwa nia ya kukomoana kisa tu hoja Haijatokea rangi ya Yanga.
 
Duh 36% huku declared share ikiwa ni 4%...Somebody has to answer where was the 32% going???
 
Mchawi unaombea nchi kufilisika lakini kwa Magufuri kila goti litapigwa ,
usiongee ushetani kila koti litapigwa likiwemo la huyu mungu mtu wako uliemtaja mbele za YESU mwana wa Mungu Alie Hai sio hawa wenyeji wa dunia hii
 
Mchawi unaombea nchi kufilisika lakini kwa Magufuri kila goti litapigwa ,
Magoti ya familia yenu labda...una laana kiasi cha kumkufuru aliyekuumba kwa kumtukuza mwanadamu. Usifikiri kwa maneno haya ndio unakuwa umempenda sana, la hasha! Unakuwa umemharibia uhusiano wake na Mungu...
 
Ukiona dereva anaendasha gari kwa kasi kulielekeza kwenye korongo, halafu wewe ni abiria upo kwenye gari, ukasema dereva huyu anaendesha gari kwa kasi na mbele kuna korongo, garilitaanguka katika korongo, tumuonye abadili uendeshaji, hapo umesherehekea gari kuanguka katika korongo kivipi?

Sent from my Kimulimuli
 
Kwanza ka isa shetani hayupo.

Tuache kudanganyana.

Tuchukue responsibility wenyewe.

Habari za kusingiia Shetani na Mungu ambao hawapo ni chanzo kikubwa cha umasikini.

Sent from my Kimulimuli
 
Naona unatafuta updates za makinikia kwa ku provoke the institution!

"the highest risk should give maximum profit"
 
Endelea kuomba iwe hivyo.Ndio kazi pekee ya upinzani iliyobaki kuiombea nchi mabaya.
 
Kama kwenye mkataba wazir na nywele zake zoote amesaini Mali za nchi zibebwe kama alivyofanya Chifu Mangungo wa Msovero leo walewale walioshuhudia na kutekeleza wizi kabla hata ya kuweka taratibu za kuvunja mikataba ya kikoloni wanadiriki kutuletea muvi tena mubashara ati tunaibiwa shaabaash! Aliewaleta nani? Hivi hizo pesa tunaziomba au tunadai? Mnakumbuka chenji ya radar? Serikali iliona aibu kutoa ushirikiano kwa shirika la kuchunguza ufisadi la Uingereza Serious Fraud Ofence (SFO) hadi huruma ndani ya bunge la uingereza ndo ikarudishwa na hili lilikuwa dili la JOKA LA MAKENGEZA na maofisa wa BAE Systems na JOKA liliendelea kupeta hadi kesho tena akapewa cheo buñgeni leo yale yale yanajirudia mtu anazomoka ati CDM wanaiombea umasikini nchi hivi kwanini usipimwe kimba?
 
Kumpa mtu kesi kubwa ambayo hauna ushahidi nao.
Unakuwa ni upumbavu wa hali ya juu.

Mtu kama unataka usaidiwe inabidi uongee ukweli tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama kuna ukeeli hivi! Mbona hakuna hata kamrejesho kutoka ukumbini? Au wamejifungia kuandika ripoti ya kumfurahisha na kumsifu aliyewapa kazi? Wiki ya pili hii imekwisha bila kupata muafaka. Kimya kingi kina mshindo na tusubiri kishindo kikuu.
 
Yule Profesa alivyokuwa anasoma ile ripoti tu ni janga la taifa.

Profesa mzima hata kusoma tu tabu.

Sasa mtu kama yule hata akipangiwa cha kusema na Magufuli siwezi kushangaa.

Sent from my Kimulimuli

Osollo anaitwa ni janga
 
Hili siyo la kushangilia, lakini kama ni la ukweli basi tupambane na hali yetu (kama wasemavyo wahenga wa siku hizi).
Mkurupuko tuliotoka nao kwenye hayo makinikia ndio tulioingia nao kwenye majadiliano. Tupeane pole tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…