1. Argument from authority hata wasioamini Mungu wanaweza kusema kuna wanasayansi mashuhuri hawaamini Mungu yupo, wakakupa sources nzuri tu na arguments nzuri tu.Kwa hiyo hii haina uzito. Hizi habari za kukubali kitu kwa sababu ya authority zilishapitwa na wakati. Za kuambiwa changanya na zako, usikubali kitu kwa sababu mwanasayansi mashuhuri tu kasema.
Watu walioamini vitu kwa sababu mwanasayansi mashuhuri kasema walirudisha nyuma maendeleo ya sayansi kwa miaka 1600 kwa sababu waliamini maneno ya Aristotle tu miaka yote hiyo.Kwa sababu Aristotle alikuwa mwanasayansi mashuhuri. Mpaka Galileo alipofanya experiment katika mnara wa Pisa na kugundua kwamba Aristotle alichosema kuhusu mass na kuanguka si sahihi.
Kwa hiyo usipende kukubali kitu kwa sababu wanasayansi mashuhuri tu wamesema,Chunguza,
Unaweza kuamini maneno ya Aristotle wa leo ukarudisha nyuma maendeleo ya elimu kwa miaka 1600 na wewe.
2. Hiyo habari ya "hupotezi lolote kwa kuamini Mungu yupo" ni Pascal's Wager. Ni uongo na ujinga.
Kama Mungu hayupo, na wewe unaamini Mungu yupo, na unatoa sadaka maisha yako yote ili umpendeze Mungu, unatumia muda wako ili uende kanisani ili umpendeze Mungu, unaishi kwa hofu kwa kumuogopa Mungu, katika maisha yako utakuwa umepoteza hela nyingi sana, umepoteza muda mwingi sana na umepoteza amani sana kwa kumuogopa Mungu ambaye hayupo. Kwa hiyo kusema "hupotezi lolote kwa kuamini Mungu yupo" kaama Mungu hayupo inakuwa si kweli.Unapoteza mengi sana kwa kuogopa kitu ambacho hakipo.