Majaji, Viongozi wa serikali, Magari ya Jeshi yanaongoza kwa kuvunja Sheria za Usalama barabarani

Majaji, Viongozi wa serikali, Magari ya Jeshi yanaongoza kwa kuvunja Sheria za Usalama barabarani

Magari ya jeshi huwa hayaendeshwi huku uraiani hasa nyakati hizi hatuna vita.
Mwanjeshi akiendesha gari lake binafsi na akavunja sheria za barabarani akamatwe apewe adhabu stahiki kama raia wengine.
Kabisaaa! Hii ni point nadhani ifike pahala Sheria iadhibu wote ili kuwe na heshima kama kipindi cha chuma
 
Kwa mantiki hii
Nikiamua kuendesha gari hata kama taa hazijaruhusu ni sawa? Such kila mtu akiamua kufanya lake itakuaje barabarani?
Hii nchi kila mtu akifanya jambo kwa ubabe wake tutafika pabaya ni swala la muda. cha msingi kuomba serikali yetu itusaidie katika hili kwa kushirikiana na Jeshi la ulinzi na usalama
 
Sheria na utekelezaji ni vitu tofauti ndugu.
Mtu mwenye pesa na mtu maarufu hawawezi hukumiwa SAWA na asiye Kwa kosa linalofanana.
Nani kasema! Kwa kuwa wao ni VIP kushinda raia wote? hapa ndipo matabaka huanzia sasa, na Road rage
 
Kama raia mmelala fofofo na hamjui haki zenu unataka sisi waheshimiwa tuchelewe kwenye foleni kama nyie?
Sasa nikutane na wewe mwenye haraka sana unambie sijui haki yangu, utakuwa wa mfano, kama wanataka twende kibabe tambueni kuna wababe waliowazidi na vyeo hawana ila wanasubiri mbuzi wa kafara ajichanganye
 
Askari wapo kazini mda wote akae foleni huyo muhalifu ana msubiria tu.
Na waliokesha LINDO usiku kukulinda wewe watatolewa saa ngapi.
Askari akiwa kazini hana Sheria ya Barbara anatumia zote ili kuwahi.
Nakuelewa, na pia naelewa kuna kipaombele lakini naona imepitiliza ustaarabu kabisa.
 
Wabanie wakutolee upepo ukae masaa unasubiria upepo uchelewe kufika.
We pisha kaa kushoto acha wapite unakereka Nini kwa kitu Cha dakika tu.
Unakuta jitu hata ambulance halipishwi Kisha ujinga TU sijui mama yake angekuwa ndie mgonjwa kabebwa akafanyiwa hivyo nae angejisikiaje.
Kigari chenyewe Cha dada
Tambua Kuna wababe na hali kama hiyo ni kama unani attack na kama huna kitu unachowahi me nakuchukulia kama raia wa kawaida na tutaenda sambamba tu
 
Hao ndio wenye nchi muhimu unakaa kushoto TU ukitaka haki hamia ulaya
Kila mtu akifanya analojisikia itakuwa nchi gani hii. au tifike hali za marekani za Ugensta kuuwana kila mtu akikuudhi, tutailinda amani namna hii
 
Kuna magari ya polisi yanayobeba kikosi cha FFU wanaoenda malindoni.

Hawa jamaa nao wanaongoza kwa kuvunja sheria barabarani.

Sijaelewa dharula zao zipo wapi kiasi cha kuvunja sheria za barabarani.
sasa Kwanini katika sheria za barabara wasiweke kwamba askari akienda lindoni asikae foleni
sheria ziko wazi mbona.

magari ya dharula yanaweza kupita njia isiyoruhusu,lakini kwa sharti lazima king'ora na udereva wa tahadhali,madhara yoyote dereva hatakuwa na kinga.

magari hayo ni ambulance,ya majeshi,zimamoto na hao viongozi kama majaji nk.
 
Kila mtu akifanya analojisikia itakuwa nchi gani hii. au tifike hali za marekani za Ugensta kuuwana kila mtu akikuudhi, tutailinda amani namna hii
Afrika ikiwa we ni masikini tii Sheria bila shuruti.
Kuuwana kunaleta ustaarabu kila mtu ataogopa kufanya upumbavu akiogopa bunduki.
Uaminifu wa wazungu umeletwa na bunduki,ukimzulumu mtu akikudaka bunduki,ukila mke WA MTU bunduki uaminifu ukaja ulaya Kwa njia hii
 
Back
Top Bottom