ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 66,537
- 75,687
Kwa Mujibu wa Kinana na Majaliwa mwaka 2025 CCM itatoa fomu Moja tuu ya mgombea Urais Kwa sababu ni utamaduni wa ccm mgombea Rais lazima aendelee kuwa mgombea Kwa awamu ya Pili.
My Take
Utaratibu wa fomu Moja alianzisha Mwendazake
=======
Mbunge wa Ruangwa (CCM), Kassim Majaliwa amesema maendeleo yanayofanyika jimboni humo chini ya utawala wa Rais Samia Suluhu Hassan yanawafanya kushawishi vikao vya juu ya chama hicho kutoa fomu moja tu ya Urais ndani ya chama katika Uchaguzi Mkuu 2025.
Majaliwa ambaye pia ni Waziri Mkuu wa Tanzania, amesema hayo leo Jumanne, Januari 2, 2025 kwenye Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM wa Wilaya ya Ruangwa uliofanyika Uwanja wa Likangara.
“Na mimi sikosei, mbele ya wajumbe wenzangu hawa kusema kuwa mheshimiwa makamu mwenyekiti, vyovyote itakavyokuwa, tunaomba tushauri kule Kamati Kuu na Halmashauri Kuu tutoe fomu moja tu ya (Rais) Samia Suluhu Hassan mwaka 2025 kama mgombea pekee wa CCM.
Hoja hiyo, imeungwa mkono na Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Abdulrahman Kinana ambaye amesema: “Utamaduni tulionao, Rais anapokuwa kwenye awamu ya kwanza, huwa tunapenda aendelee kwenye awamu inayofuata, kweli sio kweli.” amesema Kinana akitoa mfano kwa kutaja marais waliotangulia kutumia utamaduni huo tangu awamu ya tatu chini ya Hayati Rais Benjamini Mkapa.
Soma zaidi katika tovuti ya Mwananchi