Pre GE2025 Majaliwa & Kinana washauri CCM itoe Fomu 1 ya Mgombea Urais 2025

Pre GE2025 Majaliwa & Kinana washauri CCM itoe Fomu 1 ya Mgombea Urais 2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Wapi BIA YETU nimemkumbuka sana huyu mwamba kipind cha magu
 
Kwa Mujibu wa Kinana na Majaliwa mwaka 2025 CCM itatoa fomu Moja tuu ya mgombea Urais Kwa sababu ni utamaduni wa ccm mgombea Rais lazima aendelee kuwa mgombea Kwa awamu ya Pili.

View: https://www.instagram.com/p/C1mxNWoAY4d/?igsh=NmJiYWZiY2E0Mg==

My Take
Utaratibu wa fomu Moja alianzisha Mwendazake
View attachment 2860314

Hii nzuri sana ila pia atambue hata asipokuwa next PM asikonde, sio kama hakuwa mchapakazi la hasha ni mchapakazi kweli kweli ila tu ni maono ya dereva ambaye yeye anaona mbele na ndio mwenye jukumu la kutufikisha nchi inapotaka
 
Hii nzuri sana ila pia atambue hata asipokuwa next PM asikonde, sio kama hakuwa mchapakazi la hasha ni mchapakazi kweli kweli ila tu ni maono ya dereva ambaye yeye anaona mbele na ndio mwenye jukumu la kutufikisha nchi inapotaka
PM ameshakuwa Kwa miaka 10,chance aliyonayo in future ni kuwa VP au kuwa Mwenyekiti wa Bodi au Mkuu wa Chuo ambayo ndio nzuri Kwa Cheo chake kuliko kuwa Mwenyekiti wa Board ambayo Rais anaweza ijenga.

Pia Rais anaweza unda jopo analoona yeye linafaa akawa Mwenyekiti kama ilivyo Kwa Katibu Mkuu mstaafu Sefue.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Nashukuru kuwa viongozi wetu wakubwa ngazi ya Taifa chamani na serikalini wameanza kutambua kiu ya mamilioni ya watanzania waliyo nayo ya vifuani pao ya kuhitaji utumishi wa Rais Samia kwa mhula wa pili.

Mh Kasimu Majaliwa ambaye ni waziri Mkuu wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania amemuomba makamu mwenyekiti wa CCM Taifa Mh Kinana kwenda kuwashawishi wajumbe wa kamati kuu na halmashauri kuu ya CCM Taifa kuchapisha Fomu moja tu ya Urais kwa ajili ya Rais Samia.

Jambo ambalo Mh kinana aliliunga mkono kwa kutambua kazi kubwa iliyofanywa na inayoendelea kufanywa na Mh Rais wetu mpendwa kipenzi cha watanzania mama samia suluhu Hasssan,akasema ni utamaduni wa CCM kumpa muhula wa pili kiongozi anayekuwa amemaliza muhula wake wa kwanza .akasema ameona kila mtu anayesimama kuzungumza anazungumza namna Mh Rais alivyofanya kazi kubwa katika Taifa letu.

Mimi mwashambwa nimewahi kuzungumza humu jukwaani kuwa wanaccm wanapaswa kukata kiu ya watanzania kwa kuwapa chaguo na hitaji lao Ambalo ni Rais Samia. CCM itawakatisha Sana tamaa , kuwavunja moyo na kuwabubujisha sana machozi Watanzania isipowapelekea Rais Samia kama mgombea wake.

Watanzania wanamhitaji Rais Samia.huyo ndio chaguo lako,.ndio chaguo la vijana,akina mama,wazee, bodaboda,waendesha bajaji,wakulima, wafanyabiashara,wanafunzi wa vyuo, watumishi wa umma.n.k.

CCM Haina budi kusikiliza sauti za watu zinazoendelea kupazwa zikimhitaji Rais samia muhula wa pili. Huyo ndiye ambaye atapewa kura za ndio kwa kishindo kitakachoitikisa Tanzania nzima. CCM tuleteeni Rais Samia kukata kiu yetu watanzania.CCM tuleteeni chaguo letu Rais Samia.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
Haaa mzanzibar kutawala bara big no ....atapata tabu sana watu tumemvumilia kwa sababu ya kifo cha jpm tu ila hatuko tayari kuvumilia upumbavu zaidi....hofu ya kifo cha jpm ndiyo kinamsumbua mzanzibar maana anaogopa kesi ya uhaini
 
Si karejesha demokrasia nchini? Atakataa huo ushauri wa kidikteta.😁.
 
Kidumu chama cha mapinduzii ingengua swala la ajabu kuchapisha form zaidi ya moja awamu hii hata wapinzani Wana furaha
F_CM5RmXYAAzxD7.jpeg
 
Haaa mzanzibar kutawala bara big no ....atapata tabu sana watu tumemvumilia kwa sababu ya kifo cha jpm tu ila hatuko tayari kuvumilia upumbavu zaidi....hofu ya kifo cha jpm ndiyo kinamsumbua mzanzibar maana anaogopa kesi ya uhaini
Ondoa ujinga wako hapa .Sisi sote ni watanzania.wewe kama ni lihamiaji haramu nakushauri urejee haraka sana kwenu.lakini sisi watanzania chaguo letu ni Dr Samia Suluhu Hasssan kutuongoza kwa muhula wa pili tena.
 
Back
Top Bottom