Majambazi 13 wauawa Kibiti, wakutwa na Bunduki 8 pamoja na Pikipiki 2

Majambazi 13 wauawa Kibiti, wakutwa na Bunduki 8 pamoja na Pikipiki 2

kama mtuhumiwa kamtaja Juma kama mshirika wake ulitaka waongeze na John kuleta balance??? Hicho kichwa ulipewa ukitumie kwa mambo mengi sio kushikilia macho tu yakusaidie kutazama magari wakat wa kuvuka barabara
Kwwn unajua mimi nimemaanisha nini?
Hutakiwi kuongea sana, inatakiwa usikie sana ndio maana mungu akaweka maskio mawili mdomo m1.

Sent from My GooglePixel using JamiiForums mobile app
 
kama mtuhumiwa kamtaja Juma kama mshirika wake ulitaka waongeze na John kuleta balance??? Hicho kichwa ulipewa ukitumie kwa mambo mengi sio kushikilia macho tu yakusaidie kutazama magari wakat wa kuvuka barabara
Hahahaha..ungemalizia na pambaf!
 
Hahahaha!!! yaani magaidi yote 13 yalijeruhiwa kwanza halafu yakafia hospitali. Polisi naona washatugeuza misukule... Anyway kama ni kweli wameyaua pongezi ziwaendee... Ila bila picha nitabakia Thomaso tu...

Sent from my Nokia-tochi using JamiiForums mobile app
 
IGP ndani ya uwanja wa mapambano.
Hongera sana Siro, yumkini wewe ni polisi wa wito.
Sijawahi kuona mkuu yeyote wa jeshi lolote kushiriki vita 'field', bali hupiganisha vita maofisini wakiplani na si kwa kwenda kujichanganya mstari wa mbele kujenga ari na morali wa wafuasi wao wa chini kama alivyofanya kamanda Siro.
Hapo tungesikia "nimetuma vijana wangu"
Huwa hakuna uwezekano wa wao kujeruhiwa, kuyekwa ama kuuawa, wakifia kazi yao ya kiapo.
Wao huishi salama maisha yao yote hadi wanapokufa uzeeni.
Picha hii ya mkuu wa jeshi kuonekana uwanja wa mapambano ni mapinduzi makubwa ndani ya jeshi la polisi na ni mfano wa kuigwa kwenye majeshi mengine pia.
Kwenye vyuo vyao vya uongozi na ukamanda hufundishwa na kuelekezwa kuwa, kwenye kazi hatarishi, hasa ihusuyo utapia roho, kamanda hustahili kazi hiyo kuisimamia yeye mwenyewe na si kukasimisha kwa kiongozi mwingine yeyote wa chini yake, hadi kuhakikisha kazi hiyo imemalizika.
Kwa hakika kamanda Siro umeonesha njia sahihi ya utendaji uliotukuka wa kamanda.
 
Kuna jambo moja wangetusaidia kutuelewesha. Siku hizi kila mhalifu anayewapeleka polisi maeneo ya tukio kuwaonyesha wengine wako wapi naye anaishia kufa katika mapambano "kwa kujeruhiwa na kuvuja damu nyingi"
Jee huwa anapowapeleka huko halindwi ili asidhurike?
 
Mkuu kutoka na kwenda kuzungumzia jambo hilo mbele ya waandishi wa habari sio kushiriki mapigano field, mbona unakuza sana sifa zisizokuwepo? Kwa taarifa yako wakati wa mapambano alikuwa kalala nyumbani kwake.
 
Hiki ni kiinimacho tu. Wanauhadaa uma jeshi lionekane linafanya kazi inayostahili. Kazi ya polisi sio kuua, na ikitokea wameua haitakiwi kudanganya walijeruhiwa wakafa baadae. Si rahisi kujeruhi watu 13 na wote 13 wakafa ndani ya saa chache.
Habari zingine wanatangaza lakini hazistahili kutangaziwa umma. Ni habari za intelijensia ya jeshi na zinabaki jeshini. Ni maadili gani ya kazi ya jeshi unatangaza hadi sehemu silaha ilipoibiwa na ilipotumika katika uhalifu? Ni sawa kwa jeshi kuhitimisha kuwa waliouawa walikuwa majambazi na/au wahalifu? Hii ni kazi ya mahakama, hata kama polisi inahisi hivyo hao wanabaki kuwa watuhumiwa tu. Ni mahakama pekee ndiyo ingehitimisha kuwa hawa jamaa ni wahalifu.
Jeshi la polisi linahadaa sana umma kwa kuuaminisha watu fulani ni wahalifu. Tena mbaya zaidi linataja na majina ya wengine ambao hawajakamatwa! Ni intelijensia ya wapi hii?
Ni wakati muafaka kitengo cha intelijensia cha jeshi la polisi kiangaliwe upya. Inawezekana hawatambui miiko ya kazi yao au kuna watu wanaingilia kazi isiyo yao, kazi inayotakiwa kufanywa na kitengo cha intelijensia cha jeshi.
kwa mtindo huu ni rahisi sana kwa siri za jeshi kuvuja, na ni moja ya sabau ya kukomaa kwa uhalifu nchini.
 
Hahahaha!!! yaani magaidi yote 13 yalijeruhiwa kwanza halafu yakafia hospitali. Polisi naona washatugeuza misukule... Anyway kama ni kweli wameyaua pongezi ziwaendee... Ila bila picha nitabakia Thomaso tu...

Sent from my Nokia-tochi using JamiiForums mobile app
Ndg zetu polisi wanafanyakazi zao katika mazingira magumu sana.
Ninamaanisha kuwa, wao si jeshi la vita. Lazima watamke maneno kulingana na mipaka na mazingira ya kazi zao kisheria.
Wanaruhusiwa kukamata tu na si kuua.
Wanatakiwa wafanye wawezavyo kukamata, kwa njia yoyote ile na kuhakikisha wanamkamata mhalifu wao akiwa hai, kuua kwao ni mwiko.
Eti kwao kuua ni hukumu itolewayo na mahakama kwa mhalifu aliyehukumiwa.
Nadhani ifike mahali kazi ya polisi isiwekewe siasa.
Polisi kuwekwa kisiasa hutukanishwa sana katika jamii kwa kuonekana waongo.
Polisi si waongo, ila mazingira ya sheria duni zilizopo huwabidi waongee uongo wa kulazimisha.
Mfano huo wa uongo ni hili la watuhumiwa 13 kujeruhiwa na kufa wakipelekwa hisipitali.
Jeshi lolote linapokuwa limeingia katika operesheni ya kivita, huwa hawakurupuki tu.
Hufanya maandalizi ya kina namna watakavyoendesha oparesheni hiyo.
Pamoja na mambo mbalimbali ya kiutawala, huunda Echeloni watakapopelekwa majeruhi na kutibiwa, lazima kuwe na madaktari bingwa wa kuweza kutibu wagonjwa na majeruhi wa pande zote mbili hukohuko kwenye uwanja wa mapambano kabla ya majeruhi hao kusafirishwa.
Lazima waelewe jinsi watakavyohifadhi maiti za wahanga pindi wanaposubiri kusafirisha.
Pia waelewe watakavyowahifadhi mateka wao kwa muda, kabla ya kuwasafirisha location ya jela iliyoteuliwa kuhifadhi aina hiyo ya wafungwa nk nk.
Tujiulize sasa, hivi mtu anaweza kupigwa risasi na kujeruhiwa Kibiti halafu ategemee kupata matibabu hosipitali ya Muhimbili bila kupata kwanza huduma ya kwanza kwa usafiri wa kusuasua na apone?
Ninajua lengo ni kuangamiza na kutokomeza, lakini kuua mateka wote kwa pamoja ni kupoteza fursa ya kupata habari za kina.
Ninajua pia ilivyo starehe adui yako aliyekusumbua kipindi kirefu kufia mikononi mwako ukishuhudia.
Lakini tunasahau kuwa kupata 'zawadi' ya kifo cha harakaharaka bila kukisotea pia ni starehe.
Kumuua mhalifu bila ya kumhangaisha ni kumstarehesha.
Wahalifu aina ya majambazi wa kibiti, ingawa wamekataa kuwapatia "cheo" cha magaidi, wanaoua watu kwa dhana za uonevu na bila hatia, hawastahili kupigwa risasi na kutunukiwa vifo vya starehe.
Walistahili wakamatwe wakiwa hai, waeleze kinagaubaga kwa kulazimishwa ama kwa hiari yao kuwa, ni kwanini wanawatenda ndugu zao Watanzania wasiokuwa na hatia?
Baadaye sasa baada ya kusoteshwa miaka kadhaa, ndiyo wangeliulizwa kila mtu aina ya kifo anachotaka auawe.
Aina yoyote ya kifo ambacho muuaji angelikichagua, angeuziwa kifo hicho na ndugu zake wangelikilipia.
Kwa mfano: kama muuaji angelichagua kuchinjwa, ama risasi ama kamba ya kitanzi, basi vifaa hivyo vya kumuulia vingegharamiwa na ndugu zake ama jamaa zake kwa kulazimishwa kuvinunua, kuepuka kutumia ovyo pesa za walipa kodi.
Hapo jamii ingelipata somo.
Lakini hili la kupigwa risasi za bure na kufa kifo cha starehe halikubaliki.
 
Kuna jambo moja wangetusaidia kutuelewesha. Siku hizi kila mhalifu anayewapeleka polisi maeneo ya tukio kuwaonyesha wengine wako wapi naye anaishia kufa katika mapambano "kwa kujeruhiwa na kuvuja damu nyingi"
Jee huwa anapowapeleka huko halindwi ili asidhurike?

HIVI UNATAKA KUELEWESHWA ILI UKISHAELEWA UFANYE NINI? WALINDWE WASIDHURIKE KWA JAMBO JEMA GANI WANALO FANYA HAO WAHALIFU? TAFAKARI ACHA USHABIKI WA KIJINGA!!!!!
 
Kuna watu walikamatwa wapo wengi tu ndio wanawataja.....hao!!! Kwa sasa wana ushahidi na wanajua kila kitu juuu yao!! Ni suala la timing tu kwa sasa!! Ushahidi umeshkamilika mud mrefu sana! Wana watu wa kutosha sana kuwapa ushahidi!!
kwann wasiwakamate wakiwa hai ili wawabane waseme mtandao wao wa uhalifu badala ya kuwauwa na ushahidi kupotea kabisa. je kuna kitu kinafichwa?
 
Chachu Ombara unawakamataje wakati MNARUSHIANA RISASI, dhamira ni KUWAKAMATA, lakini wahalifu Wa aina ni watu walioharibika akili HAWAKUBALI KUSHINDWA KIRAHISI

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom