Hahahaha!!! yaani magaidi yote 13 yalijeruhiwa kwanza halafu yakafia hospitali. Polisi naona washatugeuza misukule... Anyway kama ni kweli wameyaua pongezi ziwaendee... Ila bila picha nitabakia Thomaso tu...
Sent from my Nokia-tochi using JamiiForums mobile app
Ndg zetu polisi wanafanyakazi zao katika mazingira magumu sana.
Ninamaanisha kuwa, wao si jeshi la vita. Lazima watamke maneno kulingana na mipaka na mazingira ya kazi zao kisheria.
Wanaruhusiwa kukamata tu na si kuua.
Wanatakiwa wafanye wawezavyo kukamata, kwa njia yoyote ile na kuhakikisha wanamkamata mhalifu wao akiwa hai, kuua kwao ni mwiko.
Eti kwao kuua ni hukumu itolewayo na mahakama kwa mhalifu aliyehukumiwa.
Nadhani ifike mahali kazi ya polisi isiwekewe siasa.
Polisi kuwekwa kisiasa hutukanishwa sana katika jamii kwa kuonekana waongo.
Polisi si waongo, ila mazingira ya sheria duni zilizopo huwabidi waongee uongo wa kulazimisha.
Mfano huo wa uongo ni hili la watuhumiwa 13 kujeruhiwa na kufa wakipelekwa hisipitali.
Jeshi lolote linapokuwa limeingia katika operesheni ya kivita, huwa hawakurupuki tu.
Hufanya maandalizi ya kina namna watakavyoendesha oparesheni hiyo.
Pamoja na mambo mbalimbali ya kiutawala, huunda Echeloni watakapopelekwa majeruhi na kutibiwa, lazima kuwe na madaktari bingwa wa kuweza kutibu wagonjwa na majeruhi wa pande zote mbili hukohuko kwenye uwanja wa mapambano kabla ya majeruhi hao kusafirishwa.
Lazima waelewe jinsi watakavyohifadhi maiti za wahanga pindi wanaposubiri kusafirisha.
Pia waelewe watakavyowahifadhi mateka wao kwa muda, kabla ya kuwasafirisha location ya jela iliyoteuliwa kuhifadhi aina hiyo ya wafungwa nk nk.
Tujiulize sasa, hivi mtu anaweza kupigwa risasi na kujeruhiwa Kibiti halafu ategemee kupata matibabu hosipitali ya Muhimbili bila kupata kwanza huduma ya kwanza kwa usafiri wa kusuasua na apone?
Ninajua lengo ni kuangamiza na kutokomeza, lakini kuua mateka wote kwa pamoja ni kupoteza fursa ya kupata habari za kina.
Ninajua pia ilivyo starehe adui yako aliyekusumbua kipindi kirefu kufia mikononi mwako ukishuhudia.
Lakini tunasahau kuwa kupata 'zawadi' ya kifo cha harakaharaka bila kukisotea pia ni starehe.
Kumuua mhalifu bila ya kumhangaisha ni kumstarehesha.
Wahalifu aina ya majambazi wa kibiti, ingawa wamekataa kuwapatia "cheo" cha magaidi, wanaoua watu kwa dhana za uonevu na bila hatia, hawastahili kupigwa risasi na kutunukiwa vifo vya starehe.
Walistahili wakamatwe wakiwa hai, waeleze kinagaubaga kwa kulazimishwa ama kwa hiari yao kuwa, ni kwanini wanawatenda ndugu zao Watanzania wasiokuwa na hatia?
Baadaye sasa baada ya kusoteshwa miaka kadhaa, ndiyo wangeliulizwa kila mtu aina ya kifo anachotaka auawe.
Aina yoyote ya kifo ambacho muuaji angelikichagua, angeuziwa kifo hicho na ndugu zake wangelikilipia.
Kwa mfano: kama muuaji angelichagua kuchinjwa, ama risasi ama kamba ya kitanzi, basi vifaa hivyo vya kumuulia vingegharamiwa na ndugu zake ama jamaa zake kwa kulazimishwa kuvinunua, kuepuka kutumia ovyo pesa za walipa kodi.
Hapo jamii ingelipata somo.
Lakini hili la kupigwa risasi za bure na kufa kifo cha starehe halikubaliki.