Majambazi 13 wauawa Kibiti, wakutwa na Bunduki 8 pamoja na Pikipiki 2

Wakumbuke si bule watu hao kufanya ivyo? Waangalie pia upande wapi wa selikali ijitasimini waache kunyanya watu ili kuwepo na usalama wakutosha yangu ni hayo kamanda silo!!

Sent using Jamii Forums mobile app
Wewe inaonekana una kitu unakijua hapa na unaweza kuwa msaada kwa police, Nafurahi unajionea matunda ya huo utaahira mnaokaririshana huko mnapojazana ujinga na mtaendelea kula shaba mpaka kiama.
 
Hivi unadhani kama wasingekuwa na taarifa za kiitelijensia wangewapata hata hao 13. Naamini hawahitaji msaada wa hao watuhumiwa na ndio maana waliendelea kujibizana kwa risasi hata kuwapoteza. Watu wa intelijensia walishamaliza kazi yao siku nyingi, sasa hivi ni utekelezaji tu. Au ulitaka wawe wanapublish taarifa zao kwa media?
 
Na wakati mapolice wanauwawa hovyo ulisema hivi?
 
Mtuhumiwa wa tatu(3) huyu anakufa kwa kujeruhiwa kwa risasi alipokuwa ameambatana na polisi kwenda kuwaonyesha walipo wenzao.
Mtuhumiwa mlikuwa naye katika line moja. Yeye anapigwa risasi zaidi ya moja nyie mlio wengi hata mmoja hajajeruhiwa kwa risasi.
Ok. Mbinguni siri zote zitafichuliwa.
Kama ni kweli basi vizuri sana, haiwezekani watu wachache kwa hila zao watake Tanzania iendeshwe kama watakavyo.
 
Mkuu
Mkuu umeongea vizuri sana lakini nadhani hwa jamaa ukiwatubza jela siasa, na mambo ya kidini yataingizwa.
 
Kwanini polisi wa Tz hawatoi picha za wahalifu waliouliwa? [emoji23][emoji23]
Wakisha kupa hiyo picha wewe itakusaidia nini? Unajua kuna vitu vingine hata ukivifikiria tu havina mantiki,

Kama una ndugu yako kapotea kapeleke taarifa police station.
 
mkuu hatari sana
 
Tumeomba mtusaidie njia za kukamata mtu anayekurushia risasi, hamtoi, bali mnatoa pvu tu humu. Unakamata vp watu wenye bunduki 8? Zabaf
ushahidi upo wapi wa kuthibitisha walikuwa wanawarushia risasi polisi?kitendo cha kuuwa watuhumiwa 13 sio cha wewe kukifurahia ,ni kitendo kinachoonyesha jeshi lako la polisi linazidi kuwa katiri na halina intelligence ya ti infiltrate mtandao huu wa ugaidi,polisi wanamafunzo waliyopewa ya kukabiliana na watumia silaha za moto,why hawakuita back up ili isaidie?,sasa umeua watu 13 ambao mimi na wewe hatuna hard evidence ya kuthibitisha ugaidi wao,na kwako ni furaha kubwa,we need a police watakao kuwa wanatekeleza kiapo cha kulinda raia,wanalazimika kutumia nguvu once maisha yao yanapokuwa hatarini na maisha ya raia wengine,waulize watuonyeshe picha za wahalifu waliouawa,kumbuka uvamizi wa msikiti pale Lindi recently je tumepewa taarifa rasmi kutoka polisi?
 
Police huwa wamevaa bulletproof na strong preventive gears pamoja na silaha za kujihami, jiulize huyo mtuhumiwa alikua equipped?

Mara nyingi mmoja wao akishaonesha wenzake nae huuwawa sababu kazi yake imeisha
 
Police huwa wamevaa bulletproof na strong preventive gears pamoja na silaha za kujihami, jiulize huyo mtuhumiwa alikua equipped?

Mara nyingi mmoja wao akishaonesha wenzake nae huuwawa sababu kazi yake imeisha
Umewahi pitia mafunzo yoyote ya kijeshi ndugu?
Polisi hawavai bullet proof.
 
Sare za kombati kuna mtu kakamatwa kwa kuwa nazo rukuki!!
 
Swahiba mie nakuunga mkono kwenye hilo ila tatizo kubwa hawa washtakiwa wengi wakikamatwa wakiwa hai unakutana nao uraiani na wengine hujitamba mfano halisi mie kaka yangu alinyongwa na majambazi wakampora gari kwa bahati nzuri walimtupa kimara suka wakijua wameua lakini alizimia tu na kabla ya tukio alimtambua mmoja wa abiria wake ambae aliingia kwenye gari yake kama teksi ilipita miaka akamuona kariakoo mmoja wa mtu aliemfanyia tukio lile akakamatwa mpaka Central alivyoingia nae pale Central askari wote walikuwa wanamjua mtu yule dili zake ni wizi wa magari na akaachiwa ilhali kaka yangu hadi leo anazo alama za mnyororo shingoni hadi leo kwa hiyo bora wapotezwe tu wapungue.
 
Unachokiandika hapa nasoma kitu kingine ndani yako
Ni wazi pia kuwa hii taarifa si nzuri kwako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…