Majambazi 13 wauawa Kibiti, wakutwa na Bunduki 8 pamoja na Pikipiki 2

Naomba majeruhi japo mmoja tu upande wa pili kama yupo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama hao majambazi wamekufa kwenye mapambano nadhani ni sawa, maana vita ni vita, pande zote mbili zinazopigana zinatumia risasi ambapo yeyote itakayempata awe polisi au jambazi kuna uwezekano huo wa kufa. Na ni sahihi kuwa anayekufa hapo ni jambazi na siyo polisi wetu, maana polisi wetu wana mafunzo ya kazi hiyo na wana wajibu wa kuonyesha uwezo wao. Lakini lipo jambo linalonitatiza sana. Inakuwaje hata yule mtuhumiwa waliyemkamata kabla ya mapambano akiwa hana silaha, tena akiwa alishajeruhiwa siku nyingi, naye ameingia katika mkumbo huo wa waliouawa? Mtuhumiwa aliyeko mikononi mwa polisi tayari amewezaje kurudi upande wa majambazi katika mpambano hadi naye akaishia kuuawa? Hapo kuna walakini, na hii inaweza kusababisha tukafikiri kuwa hapakuwako mapambano tunayoambiwa, labda walikamatwa wazima katika 'chimbo' lao hilo, na polisi wakaamua kumaliziapo hasira zao na visasi vya kuuawa wenzao.
 
Anakuwa ameshamaliza kazi yake, so naye shaba tu. Atapatikana mpya kwenye majibizano mapya kama naye alivyopatikana katika majibizano yaliyotangulia.
 
Ndugu, kesi nyingine ni bora kupoteza tu ushahidi. Hawa watu ukiwapeleka kizimbani watatoka tu halafu watakuja kusumbua tena uraiani, tena kwa kulipiza visasi kwa watoa taarifa (informants). Acha dola ifanye kazi yake. Vitu vingine ni vya ndani sana kiusalama, hatuwezi kupewa kila taarifa, tupende tusipende
 
Hongera Jeshi la Polisi, tuna imani kubwa na nyinyi.

Raia asiye na hatia, anavamiwa usiku na watu wenye silaha, anatolewa nje na kuchinjwa kama kuku, au anapigwa risasi hadi kifo, ukatili huu hauvumiliki kamwe.

Watu hao hawastahili kitu chochote, nasema tena hawastahili jambo lolote zaidi ya kuuwawa popote wanapoonekana.

Hao sio binadamu, na hawatakuwa binadamu kamwe, na hawatakiwi kushughurikiwa kama binadamu.

Wanaiga tabia za kigaidi, au ni magaidi kabisa.

Msiwatetee wala kuwachekea hao, ni makatili kupita kiasi, na kamwe hawaachi vitendo vyao viovu.

Chonde chonde jeshi la Polisi, mkishajirithisha kuwa ni wao, wapigeni risasi maramoja popote mnapowaona.

Asante jeshi la Polisi

Asante Kamanda Simon Siro

Mapambano ndo kwanza yameanza.
Wako wengi bado wazima.
Hawastahili kuwa hai.
 
Sema nao hata hawaelewekagii silaaa za staki shari siwalisema walizikama zote zikiwa zimefukiwa? Na jee wale majambazi waliokuwa wanauwawaa wanatwambia niwale waliouwa askar walikuwa hajaisha au ni wapya?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yan tunavyopenda makamera na malikes tuwauwe tusiwaonyeshee? Wale wamwanza waliuwawa tukaonyeshwa silaha zao na miili ilivyo zagaaa . huku kibiti huwa ni saund kila siku na upo uwezekano ni matukio yakutengenezaa ili waonekane wanafanya kazi kama kawaida yao. Kutaja majina sio shida inawezekana ni watu wanawatafuta wameshindwa kuwapata wanatumia gia hiyo ukijichanganya kwenda kumwangalia ndugu yako umeishaa wewe ndo ukamuonyeshe unae mtafuta. Toka matukio yameanza majambazi wanavamia na bunduki za mabomu ya machozi toka lini? Hiiii michezo yakimama sanaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Kwa nini wasikupeleke kukupiga risasi wewe mchonga ngenga?
 
Picha ni kitu muhimu sana usijifanye huelewi labda tukiona picha tunaweza kuwatambua na kujua marafiki zao wengine tukatoa msaada kwenye vyombo vya ulinzi kwani hizo picha za bunduki na mabomu zinatudaidia nini
Nenda mortuary
 
Afu Naona Humu Watu Wapimwe Akili Zao Kwanza
Yaani Jambazi Anafyatua Risasi Na bado Unashinikiza Polisi Wangewanasa wakiwa hai.
Naona Kupimwa Mikojo Watu Kumefika sasa😀😀😀😀😀😀😀
 
Afu Naona Humu Watu Wapimwe Akili Zao Kwanza
Yaani Jambazi Anafyatua Risasi Na bado Unashinikiza Polisi Wangewanasa wakiwa hai.
Naona Kupimwa Mikojo Watu Kumefika sasa😀😀😀😀😀😀😀

Risasi za majambazi za MCHANGA au maanake hata POLISI aliyejeruhiwa hakuna
 
Hapa ninachoshangaa ni kwamba wakti askari walipouliwa walionyesha miili yao. Hasa hawa 13 mbona hatuonyeshwi? Halafu tunaonyeshwa tu vifaa? Mkubali mkatae Jeshi letu la polisi lina ombwe na usanii mwingi sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wahub

Wahuni tu hawa hakuna lolote wanaigiza ili ionekane wanafanya kazi waonyeshe miili yao kama siyo uongo huo.
 

Mkuu hili igizo haliuzi kabisa. Wewe ingiza itikadi za kitoto za kuchafua jina la cdm ukidhani watu ni wajinga wa hivyo. Maiti 13 wala zisionekane zikipelekwa hospitali? Anyway hiyo sio lazima, maiti 7 zimetambulika na wenyewe wameenda kuzichukua hata wachukua maiti hapo mortuary wasionekane? Kama kukamata hao majambazi imeshindikana tafuteni mbinu nyingine sio hii ya kuona watu watoto na kuchafua majina ya vyama vya vingine kwa mambo ya kipuuzi.
 
Bunduki umetuonesha mbona hatukwenda CENTRAL POLICE STATION.
Mortuary ntaenda 2020 kuiangalia CCM
Pumba nyingine pelekeni huko DODOMA.....
Kwa akili yako ulishaona maiti inaoneshwa kwenye TV na police?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…