Majambazi 13 wauawa Kibiti, wakutwa na Bunduki 8 pamoja na Pikipiki 2

Na hao "majambazi" nao wanakuwa na ufahamu na uelewa kama huu wako wanapokuwa kwenye harakati zao?

Sent from my Device.
 
Kwa hiyo ni bora wananchi wauawe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maheremu hakuna picha zao? Hata nusu miili tu? Na je hakuna aliyekuwa walau na kitambulisho chochote?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani walikuwa wanafikiri serikali ya magufuli na vyombo vyake vya ulinzi na Usalama VIMEENDA LIKIZO?
Ngoja tu. Na BADO.
Hata kama watajificha MASHIMONI they will be smoked out one by one/ Watatolewa toka mashimoni mmoja mmoja.
Hadi wote WAISHE.
 
Ukiamua kuishi maisha ya kihalifu unakuwa umeweka maisha yako rehani. Unaishi maisha ya wasiwasi na mashaka. Kila unapoona polisi au watu wa kutiliwa mashaka, moyo hustuka. Kwa nini uishi maisha ya kuwinda na kuwindwa? Yana utamu gani?
Jitafakarini na kutubu!
 
Je, kulikuwa kuna ulazima wa kuwaua? Ingependeza kama wengine wakamatwe wakiwa hai ili kulisaidia jeshi la polisi katika upelelezi.
Hao waliouawa tayari kuna wengine walitoa ushirikiano hao wakapatwa ktk maficho yao!
Wauliwe tu tena ingependeza wawe wanawakata tu makoromea na kuacha wakifa kama kuku aliyekatwa shingo akaachiwa!
 
Hakuna majeruhi/survivor hata mmoja tu asaidie kueleza kwa nini walikuwa (allegedly) wanavamia na kuua viongozi wa CCM tu? Kwanini tumewaua wote? Kwanini hata mmoja tu hakupigwa shaba ya mguuni badala ya kifuani au kichwani?
Kwani toka mwanzo hujasikia kuwa kuna wengine walikamatwa?? Operation haijaanzia kwa hawa tu!
 
Busara peleka kwenu!
Kibiti Ni shaba tu!
Mbona wao hawatumii busara wakiua wananchi??
sawa mkuu, nitaondoka na busara zangu, lakini si zote......nyingine kidogo nakuachia wewe ndugu yangu kipenzi.

kwamba....siku chizi akikimbia na taulo lako uliloning'iniza bafuni mwako usimkimbilie kumnyang'anya..... baki bafuni, labda kama nawe wataka uonekane chizi!
 
Wameua basi!? Hamna lolote ... eti siku zote wanawauwa hamna miili tunayoiona wala nini.... hizo silaha tu tunaoneshwa ingekuwa kweli tungeoneshwa na miili ya hao watu..

MAIGIZO YANAENDELEA
 
Kuua mshukuiwa sio njia sahihi ya kukomesha ujambazi au mauaji ya Kibiti., utawala wa sheria uchukua mkondo wake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…