Majambazi 13 wauawa Kibiti, wakutwa na Bunduki 8 pamoja na Pikipiki 2

Majambazi 13 wauawa Kibiti, wakutwa na Bunduki 8 pamoja na Pikipiki 2

Hell no. .that shouldn't be the way!
Washukiwa hawatakiwi kuuwawa hata kidogo.....

Kazi ya police ni ku enforce law and order na sio judgement......

Tukiwaachia police uhuru huo... Tumekwisha.

Hili ni kwa Usalama wetu sote, Hakuna Chama Wala Ushabiki kwenye mambo kama haya......
Kwa hiyo wao wawauwe watz kama watakavyo. Lkn wao wasiuawe!!!!!
 
mkuu
ktk picha zote hizo sijaona hata tone moja la damu.... na hizo silaha zinaonekana zimetolewA sehemu salama...

ina maana hao majambazi yalipigwa risasi bila taharuki yoyote na kufa hapo hapo....
Fika kituo cha polisi chochote waambie dukuduku lako
 
Kwa hiyo wao wawauwe watz kama watakavyo. Lkn wao wasiuawe!!!!!
Ni jambo la kushangaza sana, wananchi wakiuwawa kibiti utayasikia yakisema serikali iko wapi wananchi wanauwawa hovyo,

police wakifanya kazi kuyauwa hayo magaidi utashangaa hayo hayo yanapayuka kwa nini mnawauwa watu bila mahakamani, hapo ndipo utachoka zaidi
 
Polisi wana bahati sana wanajua namna ya kukwepa risasi, maana kwenye majibizano hayo ya risasai hakuna hata polisi mmoja aliyejeruhiwa!!

# Si rahisi kuwaamini polisi bongo.
Wamefunzwa wenzio wanajua moto ukitokea kushoto watajenga ngome kulia hayo ndo mafunzo
 
Hell no. .that shouldn't be the way!
Washukiwa hawatakiwi kuuwawa hata kidogo.....

Kazi ya police ni ku enforce law and order na sio judgement......

Tukiwaachia police uhuru huo... Tumekwisha.

Hili ni kwa Usalama wetu sote, Hakuna Chama Wala Ushabiki kwenye mambo kama haya......
Watu waliouwawa waliwakosea nini? Ni rahisi kujidanganya kwamba wako untouchable au hawawezi kufikiwa kwa urahisi. Lakini dhuluma yao imetosha. Wameua watu wasio na hatia na wengine bila haya waliwasifu.
Acha wavune wanayopanda.

Nalipongeza sana jeshi la polisi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unamkamata vp mtu ana silaha ya kivita na anapambana na ww?
 
Watu 13 wanaodaiwa kuwa ahalifu wameuawa na Askari wa Jeshi la Polisi. Watu hao wamekutwa na Bunduki nane, Pikipiki mbili pamoja na Begi moja la nguo.

Tukio hilo limetokea katika maeneo ya Tangibovu Kijiji cha Milaweni, huko Kibiti Mkoani Pwani.
View attachment 562464 View attachment 562465
View attachment 562467
View attachment 562466
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Operesheni Maalumu za Jeshi la Polisi, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Liberatus Sabas kuhusiana na tukio la kuuawa wahalifu 13 katika majibizano ya risasi baina ya Polisi na wahalifu hao katika eneo la Tangibovu, Kijiji cha Miwaleni Kata ya Mchukwi, Tarafaya Kibiti.Chini ni silaha 8 aina ya SMG pamoja na vifaa vingine zilizopatikana katika majibizano hayo.
Chanzo: Jeshi la Polisi Tanzania(Ukurasa wa Twitter)
--------------

UPDATES..

Orodha ya Majina ya wahalifu 7 kati ya 13 waliouawa leo na Jeshi la Polisi eneo la Tangibovu ktk Wilaya ya Kibiti mkoani Pwani
1be4dcb1030cefec4c7b5919ad64b788.jpg
Criminal mind at work,sasa kama kila jambazi/gaidi ni mwendo wa risasi tu,tutapataje intelligence,kamateni mmoja,ahojiwe,ijurikane motive ya matendo wanayofanya nini,?
Je ni ugaidi tu,ni visasi tu,au kuna siasa ndani yake,jeshi inabidi lijipange,nimesikia baadhi ya waliouliwa,walikuwa na mafunzo ya kijeshi,sasa hapa ndio hatari zaidi,hawa wenye mafunzo wapo kibao mtaani,juzi nirikuwa wilaya ya misenyi mkoani Kagera,vijiji vya ndani kabisa,karibu na mpaka was UG,nikakuta,JWTZ,wanatoa mafunzo ya mgambo kwa vijana,kijijini hapo,kati ya vijana watano,unaokutana nao,watatu,wamepigilia kombati za mgambo,wanaishi kijeshi muda wote,kuanzia mavazi,mpaka staili ya kunyoa denge LA wazee,
Sasa hawa vijana,wakiamua kushika mitutu,polisi mtapona?jipangeni wakuu,kutwanga risasi tu,sio suluhisho,mnauwa 11,nyie mnapoteza vijana wenu 8,...no hatari
 
Watu waliouwawa waliwakosea nini? Ni rahisi kujidanganya kwamba wako untouchable au hawawezi kufikiwa kwa urahisi. Lakini dhuluma yao imetosha. Wameua watu wasio na hatia na wengine bila haya waliwasifu.
Acha wavune wanayopanda.



Nalipongeza sana jeshi la polisi.


Mkuu heshima kwako,
Mwenye mamlaka ya kuthibitisha Kama wameua ama la ni polisi Au mahakama?
 
Polisi imeanzisha orodha yake ya mauaji. Yawezekana ikavunja rekodi ya ile ya wahalifu wengine
 
Back
Top Bottom