Watu 13 wanaodaiwa kuwa ahalifu wameuawa na Askari wa Jeshi la Polisi. Watu hao wamekutwa na Bunduki nane, Pikipiki mbili pamoja na Begi moja la nguo.
Tukio hilo limetokea katika maeneo ya Tangibovu Kijiji cha Milaweni, huko Kibiti Mkoani Pwani.
View attachment 562464 View attachment 562465
View attachment 562467
View attachment 562466
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Operesheni Maalumu za Jeshi la Polisi, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Liberatus Sabas kuhusiana na tukio la kuuawa wahalifu 13 katika majibizano ya risasi baina ya Polisi na wahalifu hao katika eneo la Tangibovu, Kijiji cha Miwaleni Kata ya Mchukwi, Tarafaya Kibiti.Chini ni silaha 8 aina ya SMG pamoja na vifaa vingine zilizopatikana katika majibizano hayo.
Chanzo: Jeshi la Polisi Tanzania(Ukurasa wa Twitter)
--------------
UPDATES..
Orodha ya Majina ya wahalifu 7 kati ya 13 waliouawa leo na Jeshi la Polisi eneo la Tangibovu ktk Wilaya ya Kibiti mkoani Pwani
Criminal mind at work,sasa kama kila jambazi/gaidi ni mwendo wa risasi tu,tutapataje intelligence,kamateni mmoja,ahojiwe,ijurikane motive ya matendo wanayofanya nini,?
Je ni ugaidi tu,ni visasi tu,au kuna siasa ndani yake,jeshi inabidi lijipange,nimesikia baadhi ya waliouliwa,walikuwa na mafunzo ya kijeshi,sasa hapa ndio hatari zaidi,hawa wenye mafunzo wapo kibao mtaani,juzi nirikuwa wilaya ya misenyi mkoani Kagera,vijiji vya ndani kabisa,karibu na mpaka was UG,nikakuta,JWTZ,wanatoa mafunzo ya mgambo kwa vijana,kijijini hapo,kati ya vijana watano,unaokutana nao,watatu,wamepigilia kombati za mgambo,wanaishi kijeshi muda wote,kuanzia mavazi,mpaka staili ya kunyoa denge LA wazee,
Sasa hawa vijana,wakiamua kushika mitutu,polisi mtapona?jipangeni wakuu,kutwanga risasi tu,sio suluhisho,mnauwa 11,nyie mnapoteza vijana wenu 8,...no hatari