Majambazi 13 wauawa Kibiti, wakutwa na Bunduki 8 pamoja na Pikipiki 2

Majambazi 13 wauawa Kibiti, wakutwa na Bunduki 8 pamoja na Pikipiki 2

Hell no. .that shouldn't be the way!
Washukiwa hawatakiwi kuuwawa hata kidogo.....

Kazi ya police ni ku enforce law and order na sio judgement......

Tukiwaachia police uhuru huo... Tumekwisha.

Hili ni kwa Usalama wetu sote, Hakuna Chama Wala Ushabiki kwenye mambo kama haya......

Uko sahihi kwa upande huo na nime kupa LIKE. Askari ni binadam wanaweza kukosea katika kazi zao, hivyo akauliwa MTU asiyestahili, any way hata wakipelekwa mahakamani wanenda hukumiwa na binadam haohao hivyo kukosea bado kunaweza kuwepo

Ili kuwapata hao wauaji inabidi muweke mitego. Na hata mkisikia na kujua fulani anahusika bado ni shida kumtia hatiani. Itabidi mumkamate kwenye tukio, tukio la kuua. Itabidi mumkamate akiwa ameua na akiwa bado na silaha yake. Kazi ngumu kweli kweli na pia Hatari kisawasawa.
Itabidi muwe na vifaa, mafunzo na nguvu kazi yenye kujitolea haswas.
Polisi kufanya hivi kuondoa kadhia hii ya huko rufiji Kibiti basi huenda hili si kitu kigeni.

Nasikia Arusha kuna kipindi ilikuwa Juu sana kwa uhalifu, kipindi cha mzee mkapa. Uhalifu huo ulienda sambamba na mauaji na ushenzi mwingine. Naamini kulikuwa na vijana waliokuwa wanafanya hizi operesheni na nyuma yao kulikuwa na wapanga mikakati na wafadhili wa huo ushenzi.

Kwa kuangalia uwezo wa polisi ilikuwa ngumu kuwakamata kwenye matukio wahusika. Na hata wakikamatwa hizo Mara chache na wakawataja wanaowafadhili ilikuwa ngumu kuwatia hatiani hao wafadhili, na kwa kuzingatia rushwa huko polisi mpaka mahakamani na serikali ni hao jamaa naona wakawa hawafungiki jela.

Polisi au serikali isingeweza kuendelea kujipanga mpaka iweze kuwakamata kwenye matukio hao wahalifu ambao kimsingi walikuwa wanajulikana. Isingeweza kuendelea kujipanga wakati wananchi wanaumia na wanailaumu serikali kwa kutochukua hatua

Hatua iliyochukuliwa nasikia Arusha si kama zamani. Uhalifu mkubwa wa kimabavu wa zamani nasikia umepungua.

Cha muhimu hao askari wawe na nia njema na kazi zao na wawe na uhakika na hao wahalifu. Tumeona na kusikia Mara nyingi vitendo vya kiuonevu vya polisi.
 
Naona maruweruwe tu, sijui kwanini, lakini sitaki kucomment kuhusu kuwapongeza Jeshi la polisi au vipi maana:
1.Walishindwa nini kumkamata mmojawapo akasaidia Jeshi kufahamu nani yupo nyuma yao??

2.Hakuna hata miili inaonyeshwa au any vivid evidence ?

3.Polisi wetu ni makini na wana mafunzo kiasi majambazi 13 wa kiwango cha Kibiti wanaweza kufyatua kupambana na asipate hata jeraha yeyote?

4.Jeshi la polisi halijashtuka namna silaha zote hizo za kivita zinatumika na hao majambazi?? Kwanini wasifunguliwe mashtaka hata mmojawapo ikibidi angekamatwa?

Yaani Bongoland full maruweruwe,but my instincts tells me something is going on,too much faking

Sent From Kisana Kiki Iphone
 
Wote13 wameuwawa? Bila ata mmoja kumkamata akiwa hai, ili kustrengthen uchunguzi wa kihalifu

Polisi hawakurupuki wanafanya kazi zao kwa ueledi mkubwa, wahusika wote na nyenendo zao zimekwisha julikana - ndiyo maana wanawawekea mitego na kuwazingira kirahisi - Jeshi la Polisi Tanzania wakipania kitu hawashindwi hata siku moja, masuala mengine inaweza kuwachukuwa muda kuyatatua lakini mara zote ufanikiwa eventually.
 
Majibizano ya risasi yameua watu wote 13 pamoja na mtuhumiwa aliowapeleka mafichoni lakini hakuna polisi hata mmoja aliopata shida yoyote ? Hata shati kuchanika?

Jeshi letu liko vizuri sana aisee.
Jeshi letu limepiga hatua sana kwa sasa... Nadhani walipeleka Robot kwenda kupambana na hao majamaa...

Ushaangalia movie ya Terminator??
 
Hawa jamaaa wangeachwa wangejisifu sana. Hongereni sana jeshi la polisi. Wote wanaohusika watafutwe na kuchukuliwa hatua
 
Watu 13 walikuwa wamepanda pikipiki mbili? Naona kwenye hiyo picha Kamanda Sirro anayoongea na hao wanakijiji, kuna kila dalili watu wasio na hatia ni wahanga.
 
Wakuu naona bunduki mbili za kwanza kwenye picha ni kama vile zile zinazotumiwa na FFU kurushia mabomu ya machozi..

Inakuwaje majambazi wawe na bunduki za kurushia mabomu ya machozi ..
Huu si ujinga wa kiwango cha SGR ..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bila picha ni sanaa tu..

Sent using Jamii Forums mobile app
U
Maheremu hakuna picha zao? Hata nusu miili tu? Na je hakuna aliyekuwa walau na kitambulisho chochote?

Sent using Jamii Forums mobile app

Mkuu mshana jr kila siku tunalisema hili, wanapotoa taarifa za kuua majambazi watupe basi na taarifa kuhusu "identity" zao (majina, vitambulisho, walipotoka e.t.c) au kama hazijulikani basi waseme hii inaweza basi kusaidia hata wasamaria kuwapa habari zaidi("inteligensia") iwapo itatokea wasamaria hao wamewatambua. Hii habari ya kuonyeshwa tu silaha inaleta ukakasi kwenye hizo taarifa zao.

Pili kama wanakabiliana na ujambazi/uhalifu wa kupangwa, unapoua majambazi kila siku unajikosesha nafasi ya kupata habari za "ki-inteligensia", kwanini kila siku we majambazi wote unaua tuuuuu kwanini usimkate akiwa hai ili akupe taarifa zaid? Jeshi letu linahitaji mabadiliko makubwa sana vinginevyo itakuwa ni sanaa tuuuuuu kila siku na matukio hayatakoma au kupungua.

My Country!!!! My Police!!!!
 

Tarehe 09.08.2017 majira ya saa 21:00 Hrs (saa tatu usiku) katika mapori ya kijiji cha Rungungu mtuhumiwa akiambatana na Askari Polisi alikwenda kuonyesha Ngome ya watuhumiwa wenzake aliokuwa anashirikiana nao kufanya uhalifu.

Baada ya kukaribia eneo la tukio ulitokea upinzani mkali wa majibizano ya risasi jambo lililopelekea hata Abdallah Abdallah Mbindimbi @Abajani kujeruhiwa na risasi sehemu mbalimbali za mwili wake.

Kufuatia majibizano hayo, Askari Polisi walifanikiwa kuwajeruhi wahalifu 12 (kumi na mbili. Jitihada zilifanyika kuwapeleka Hospitali majeruhi wote 13 (kumi na tatu) ingawa baadae walifariki dunia kwa nyakati tofauti wakipelekwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kutokana na kuvuja damu nyingi zilizosababishwa na majereha ya risasi sehemu mbalimbali za miili yao. Miili ya marehemu imehifadhiwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Jijini Dar es salaam.

Ndugu Wanahabari
Watuhumiwa 7 (Saba) kati ya 13 (kumi na tatu) waliopoteza maisha kutokana na majibizano ya risasi wametambuliwa kuwa ni:

1. Hassani Ali Njame
2. Abdallah Abdallah Mbindimbi @ Abajani
3. Saidi Abdallah Kilindo
4. Abdulshakuru Mohamed Ubuguyu
5. Issa Mohamed Mseketu mtawa
6. Rajabu Thomas roja
7. Mohamed Ally Kadude @Upolo
Miili 6 (sita) iliyobaki haikuweza kutambulika mara moja hivyo utambuzi utaendelea huko ilikohifadhiwa Hospitalini DSM.

Ndugu Wanahabari
Vielelezo mbalimbali vilipatikana katika eneo la tukio, kama ifuatavyo:
S/N
KIELELEZO
UTAMBUZI
SILAHA, RISASI NA MABOMU
1.
SMG = 5
Mali ya Jeshi la Polisi tukio la kupora Silaha Askari huko Mtengeni – Jaribu Mpakani

2.
Anti Riot Gun 38mm = 2
Mali ya Jeshi la Polisi tukio la kupora Silaha Askari huko Mtengeni – Jaribu Mpakani

3.
SAR = 1
Mali ya Jeshi la Polisi tukio la kupora Silaha Askari Polisi huko Stakishari Jijini Dar es Salaam

4.
MAGAZINI = 2
Mali ya Jeshi la Polisi tukio la kupora Silaha Askari huko Mtengeni – Jaribu Mpakani

5.
Risasi za SMG 158
Mali ya Jeshi la Polisi tukio la kupora Silaha Askari huko Mtengeni – Jaribu Mpakani

6.
Bomu la kurusha kwa mkono = 1
Uchunguzi dhidi ya Bomu hilo unaendelea

7.
Mabomu ya kutuliza ghasia = 4
Mali ya Jeshi la Polisi tukio la kupora Silaha Askari huko Mtengeni – Jaribu Mpakani

VIELELEZO VINGINE

8.
Pikipiki = 2
Pikipiki hizi zilitumika kuwasafirisha wahalifu hawa kwenye utekelezaji wa matukio ya uhalifu maeneo mbalimbali

9.
Vitenge na Nguo mbalimbali
Vitenge na nguo mbalimbali viliporwa baada ya kufanya tukio la kumuua Diwani wa Zamani wa Kibwiwi

10.
Begi = 1
Liliporwa baada ya kumuua Mtendaji wa Kijiji cha Mangwe

Ndugu Wanahabari
Kwa mujibu wa taarifa za utambuzi wa vielelezo vilivyopatikana eneo la tukio na utambuzi wa baadhi ya miili ya watuhumiwa waliofariki inaonyesha kuwa walishiriki matukio ya uhalifu maeneo mbalimbali kama ifuatavyo:
1. Kuua OC CID na Watumishi 2 (Wawili) wa Idara ya Maliasili katika tukio la Jaribu Mpakani – Wilaya Kibiti
2. Kuua Askari Polisi 8 (Nane) katika tukio la Mkengeni – Wilayani Kibiti
3. Kuua Trafiki 2 (Wawili) katika tukio la Bungu “B” – Wilaya ya Kibiti
4. Kumuua Diwani wa Zamani CCM katika tukio la Kibwibwi – Wilaya ya Kibiti
5. Kuua Afisa Mtendaji, Mwenyekiti wa Mtaa na Mkulima katika tukio la Kijiji cha Mangwi – Wilaya ya Kibiti

Ndugu Wanahabari
Wito wangu kwa Wananchi ni kuhusu mambo muhimu yafuatayo:

a. Wananchi wote nchini kuondoa hofu ya kwamba eneo hili si salama. Nawaomba wananchi waendelee kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi na kwa kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu. Aidha nawaomba wananchi kutoa taarifa mara moja kwa Jeshi la Polisi wanapohisi kuna jambo lolote wanalolitilia mashaka.

b. Natoa wito kwa wananchi wa mkoa wa Pwani, hususani maeneo ya Mkuranga, Kibiti na Ikwiriri, kuendelea na shughuli zao mbalimbali za kujiletea maendeleo. Nawasihi kwa dhati kabisa waendelee kutupatia taarifa zitakazosaidia kumaliza kabisa uhalifu kwenye eneo hili. Nitumie fursa hii kuwashukuru sana wananchi wa maeneo ya Mkuranga, Kibiti na Ikwiriri kwa ushirikiano mnaotupatia ambao umesaidia sana kuwadhibiti wahalifu.

c. Mamlaka za Hospitali, Zahanati, Vituo vya Afya, Maabara za Afya ya Binadamu na Maduka ya Kuuza Dawa za kutibu Binadamu zijiepushe na utaratibu wa kutoa matibabu kienyeji au kificho kwa watu waliojeruhiwa bila kufuata taratibu za kisheria ikiwemo kupata taarifa ya Polisi “kupitia Fomu maalum ya kuruhusu matibabu (maarufu kama PF. 3)”. Wahalifu wakijeruhiwa ni lazima watafute matibabu.

Kwa hiyo idara hizi ni muhimu sana kutoa ushirikiano ili kutuwezesha kuwakamata watuhumiwa maana baadhi yao wamekutwa na majeraha sehemu mbalimbali za miili yao na walikuwa wanaendelea kujitibia kwa kificho kwa kutumia dawa za hospitali.

Natoa wito kwa Mamlaka hizo kutoa taarifa mara moja kwa Jeshi la Polisi wanapoona ama kumbaini mtu ambaye ataonekana kuwa na majeraha na anatafuta tiba bila ya kufuata taratibu.

Ndugu Wanahabari
Napenda kuujulisha Umma kwamba wapo baadhi ya Watuhumiwa, Wafadhili na Washirika wa Uhalifu na Wahalifu wa ujambazi maeneo haya ambao bado hawajakamatwa. Jambo la kufurahisha ni kwamba taarifa zao zipo kwa Jeshi la Polisi nchini na zinaendelea kufanyiwa kazi ili waweze kukamatwa na kufikishwa kwenye mkono wa Sheria mara moja.

Natoa wito kwa wananchi ambao wanawafahamu watuhumiwa wafuatao kutoa taarifa katika kituo chochote cha Polisi ili waweze kukamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria.

Picha za watuhumiwa hao zitasambazwa kote nchini ili iwe rahisi kuwabaini. Majina ya watuhumiwa hao ni:
i.Anafi Rashid Kapelo @ Abuu Mariam
ii. Hassan Haruna Kyakalewa @ Abuu Salma @ Shujaa @ Dokta
iii. Haji Ulatule
iv. Shekhe Hassan Nasri Mzuzuri
v. Rashid Mtutula

Ndugu Wanahabari
Nimalizie kwa kusema kwamba uhalifu kwenye eneo hili ni suala la muda mfupi. Na tunaendelea vizuri sana. Hali ya usalama imeimarika sana eneo hili. Nazidi kutoa wito kwa wananchi kuendelea kuliunga mkono Jeshi la Polisi ili kufikia malengo yake ya kuzuia, kubambana na kutanzua uhalifu nchini.



Imetolewa na;

Simon Nyakoro Sirro
Inspekta Jenerali wa Polisi
IKWIRIRI
10.08.2017
 
Hayo majina naona yapo upande mmoja, tuanzie hapo

Sent from My GooglePixel using JamiiForums mobile app
kama mtuhumiwa kamtaja Juma kama mshirika wake ulitaka waongeze na John kuleta balance??? Hicho kichwa ulipewa ukitumie kwa mambo mengi sio kushikilia macho tu yakusaidie kutazama magari wakat wa kuvuka barabara
 
MUWE NA ELIMU HATA KIDOGO YA KIVTA HIVI UNAKUTANA GHAFLA NA MTU ANAANZA KUMWAGA RISASI MFULULZO UTAHANGAIKA KUMTEKA ILI UPATE TAARIFA AU UTAPAMBANA ASIKUUWE ILI UJIOKOE? MAANA YAKE NI KWAMBA KUNA WAKATI TAARIFA HAZINA UMUHMU KULIKO USALAMA WA ASKARI ALIYEKO FRONT
 
Hell no. .that shouldn't be the way!
Washukiwa hawatakiwi kuuwawa hata kidogo.....

Kazi ya police ni ku enforce law and order na sio judgement......

Tukiwaachia police uhuru huo... Tumekwisha.

Hili ni kwa Usalama wetu sote, Hakuna Chama Wala Ushabiki kwenye mambo kama haya......
Hivi kwenye hayo mapori si wamekuwa wakipita mara kwa mara walikuwa hawaonekani katika misako yao??? so wange wazunguka tu mpaka waka kosa pumzi na kuwaokota kama vifaranga na kuwauwa,katika majibizano ya risasi inaonekana upande mmoja haukuathirika kabisa ni mini hicho.Polisi wetu wawe na weledi,wange wakamata wakiwa hai Polisi wange pata taarifa nyingi sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom