Majambazi 13 wauawa Kibiti, wakutwa na Bunduki 8 pamoja na Pikipiki 2

Majambazi 13 wauawa Kibiti, wakutwa na Bunduki 8 pamoja na Pikipiki 2

Hell no. .that shouldn't be the way!
Washukiwa hawatakiwi kuuwawa hata kidogo.....

Kazi ya police ni ku enforce law and order na sio judgement......

Tukiwaachia police uhuru huo... Tumekwisha.

Hili ni kwa Usalama wetu sote, Hakuna Chama Wala Ushabiki kwenye mambo kama haya......
Ni kazi nzuri wamepunguza idadi ya majambazi angalau uhalifu utapungua pia eneo hilo, Pongezi kwa askari wetu.
Mkuu upande wa pili; walikuwa wanarushiana risasi na majambazi hao... kwa bahati mbaya na yule aliyewapeleka alikufa kutokana na majeraha hizi ndizo taarifa tata na tete zinazoleta mashaka! ila "walishasema" kazi ya Polisi ni ipi mkuu!? Polisi wamepewa bunduki...
Mungu ibariki Tanzania.
 
Kuna jambo moja wangetusaidia kutuelewesha. Siku hizi kila mhalifu anayewapeleka polisi maeneo ya tukio kuwaonyesha wengine wako wapi naye anaishia kufa katika mapambano "kwa kujeruhiwa na kuvuja damu nyingi"
Jee huwa anapowapeleka huko halindwi ili asidhurike?
Toilet paper....not useful anymore.

Kama mapambano ya kushtukiza ni kila mtu analinda uhai wake. Huyu muonyeshaji hakuwa na silaha ya kujilinda lazima angedhurika mapema.

Hiyo taarifa ya polisi imejitosheleza sana. Ndio maana inasema kuna Fulani na Fulani waliobaki! Kuna waliofanya mauji ya askari n.k it means they talk na waliongea yote kabla hawajafikishwa Muhimbili. Bahati mbaya tu damu ziliwaishia kabla ya kupatiwa matibabu.

Sent from my Device.
 
Wametambuaje majina yao na walipambana kwa risasi. Au wakati wanakufa walitaja majina yao? Au waliweka parade kijinini wakawatambua?? Maana hata mtu mwenye maumivu ya risasi hawezi kukupa majina full

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wameua basi!? Hamna lolote ... eti siku zote wanawauwa hamna miili tunayoiona wala nini.... hizo silaha tu tunaoneshwa ingekuwa kweli tungeoneshwa na miili ya hao watu..

MAIGIZO YANAENDELEA
Hivi mnataka miili ya nini? Mpige nayo picha au? Acheni kuwa kama Tomaso. Ya nini kuonyesha miili iliyopigwa au kujeruhiwa vibaya na risasi kwenye media? Kama hamuamini wameuawa basi subirini wafufuke
 
Siro anajifanya hadi adress yake ipo ikwiriri.

Kweli watu wanajua kumkamata mkulu masikio
 
Hongera sana jeshi la polisi, hongera sana kamanda Sirro kwa kazi nzuri mliyoifanya.
Ushauri; Hizo picha za wahalifu waliobakia zitolewe haraka sana kwenye vyombo vya habari ili wananchi wapate fursa ya kulisaidia jeshi la polisi.
Tunataka amani kwa maendeleo ya taifa letu.
 
Ni kweli waliouawa walikuwa majambazi!!?
Hapana! Walikuwa ni viongozi wa dini wanaomiliki silaha za moto. Si ndivyo mnavyotaka kujibiwa? Kama hawakuwa majambazi, walikuwa wanafanya nini na bunduki 8? Au walikuwa walinzi wa msituni?
 
Ualifu huwa haulipi una mwisho mbaya utakuta hao walidanganywa na waganga wa kienyeji kuwa hawatokamatwa wakaamini sababu ya kutokuwa na elimu,na kudanganywa na picha za kwenye vidio.Hongera jeshi la polisi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Si vibaya kuwaondoa Duniani Watanzania 13 wanaotishia usalama wa Watanzania 50,000,000.
Kazi njema sana.. Waliofanikisha zoezi hili wazawadiwe kila mmoja angalau Tsh 10,000,000 za motisha.. Najua nchi ina pesa za kutosha za bajeti ya ulinzi na usalama...
 
Kuna jambo moja wangetusaidia kutuelewesha. Siku hizi kila mhalifu anayewapeleka polisi maeneo ya tukio kuwaonyesha wengine wako wapi naye anaishia kufa katika mapambano "kwa kujeruhiwa na kuvuja damu nyingi"
Jee huwa anapowapeleka huko halindwi ili asidhurike?
hapa hata mimi huwa nashangaa, iweje walie nae (polisi) watoke salama ila aliye wapeleka auawe

kwamba wadunguaji huwa wanamuona yeye tu huu ni uongo dhahiri
 
Back
Top Bottom