Majambazi 13 wauawa Kibiti, wakutwa na Bunduki 8 pamoja na Pikipiki 2

Majambazi 13 wauawa Kibiti, wakutwa na Bunduki 8 pamoja na Pikipiki 2

Watu 13 wanaodaiwa kuwa wahalifu wameuawa na Askari wa Jeshi la Polisi. Watu hao wamekutwa na Bunduki nane, Pikipiki mbili pamoja na Begi moja la nguo.

Tukio hilo limetokea katika maeneo ya Tangibovu Kijiji cha Milaweni, huko Kibiti Mkoani Pwani.
View attachment 562464 View attachment 562465
View attachment 562467
View attachment 562466
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Operesheni Maalumu za Jeshi la Polisi, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Liberatus Sabas kuhusiana na tukio la kuuawa wahalifu 13 katika majibizano ya risasi baina ya Polisi na wahalifu hao katika eneo la Tangibovu, Kijiji cha Miwaleni Kata ya Mchukwi, Tarafaya Kibiti.Chini ni silaha 8 aina ya SMG pamoja na vifaa vingine zilizopatikana katika majibizano hayo.
Chanzo: Jeshi la Polisi Tanzania(Ukurasa wa Twitter)
--------------

UPDATES..

Orodha ya Majina ya wahalifu 7 kati ya 13 waliouawa leo na Jeshi la Polisi eneo la Tangibovu ktk Wilaya ya Kibiti mkoani Pwani
1be4dcb1030cefec4c7b5919ad64b788.jpg

Tarehe 09.08.2017 majira ya saa 21:00 Hrs (saa tatu usiku) katika mapori ya kijiji cha Rungungu mtuhumiwa akiambatana na Askari Polisi alikwenda kuonyesha Ngome ya watuhumiwa wenzake aliokuwa anashirikiana nao kufanya uhalifu.

Baada ya kukaribia eneo la tukio ulitokea upinzani mkali wa majibizano ya risasi jambo lililopelekea hata Abdallah Abdallah Mbindimbi @Abajani kujeruhiwa na risasi sehemu mbalimbali za mwili wake.

Kufuatia majibizano hayo, Askari Polisi walifanikiwa kuwajeruhi wahalifu 12 (kumi na mbili. Jitihada zilifanyika kuwapeleka Hospitali majeruhi wote 13 (kumi na tatu) ingawa baadae walifariki dunia kwa nyakati tofauti wakipelekwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kutokana na kuvuja damu nyingi zilizosababishwa na majereha ya risasi sehemu mbalimbali za miili yao. Miili ya marehemu imehifadhiwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Jijini Dar es salaam.

Ndugu Wanahabari
Watuhumiwa 7 (Saba) kati ya 13 (kumi na tatu) waliopoteza maisha kutokana na majibizano ya risasi wametambuliwa kuwa ni:

1. Hassani Ali Njame
2. Abdallah Abdallah Mbindimbi @ Abajani
3. Saidi Abdallah Kilindo
4. Abdulshakuru Mohamed Ubuguyu
5. Issa Mohamed Mseketu mtawa
6. Rajabu Thomas roja
7. Mohamed Ally Kadude @Upolo
Miili 6 (sita) iliyobaki haikuweza kutambulika mara moja hivyo utambuzi utaendelea huko ilikohifadhiwa Hospitalini DSM.

Ndugu Wanahabari
Vielelezo mbalimbali vilipatikana katika eneo la tukio, kama ifuatavyo:
S/N
KIELELEZO
UTAMBUZI
SILAHA, RISASI NA MABOMU
1.
SMG = 5
Mali ya Jeshi la Polisi tukio la kupora Silaha Askari huko Mtengeni – Jaribu Mpakani

2.
Anti Riot Gun 38mm = 2
Mali ya Jeshi la Polisi tukio la kupora Silaha Askari huko Mtengeni – Jaribu Mpakani

3.
SAR = 1
Mali ya Jeshi la Polisi tukio la kupora Silaha Askari Polisi huko Stakishari Jijini Dar es Salaam

4.
MAGAZINI = 2
Mali ya Jeshi la Polisi tukio la kupora Silaha Askari huko Mtengeni – Jaribu Mpakani

5.
Risasi za SMG 158
Mali ya Jeshi la Polisi tukio la kupora Silaha Askari huko Mtengeni – Jaribu Mpakani

6.
Bomu la kurusha kwa mkono = 1
Uchunguzi dhidi ya Bomu hilo unaendelea

7.
Mabomu ya kutuliza ghasia = 4
Mali ya Jeshi la Polisi tukio la kupora Silaha Askari huko Mtengeni – Jaribu Mpakani

VIELELEZO VINGINE

8.
Pikipiki = 2
Pikipiki hizi zilitumika kuwasafirisha wahalifu hawa kwenye utekelezaji wa matukio ya uhalifu maeneo mbalimbali

9.
Vitenge na Nguo mbalimbali
Vitenge na nguo mbalimbali viliporwa baada ya kufanya tukio la kumuua Diwani wa Zamani wa Kibwiwi

10.
Begi = 1
Liliporwa baada ya kumuua Mtendaji wa Kijiji cha Mangwe

Ndugu Wanahabari
Kwa mujibu wa taarifa za utambuzi wa vielelezo vilivyopatikana eneo la tukio na utambuzi wa baadhi ya miili ya watuhumiwa waliofariki inaonyesha kuwa walishiriki matukio ya uhalifu maeneo mbalimbali kama ifuatavyo:
1. Kuua OC CID na Watumishi 2 (Wawili) wa Idara ya Maliasili katika tukio la Jaribu Mpakani – Wilaya Kibiti
2. Kuua Askari Polisi 8 (Nane) katika tukio la Mkengeni – Wilayani Kibiti
3. Kuua Trafiki 2 (Wawili) katika tukio la Bungu “B” – Wilaya ya Kibiti
4. Kumuua Diwani wa Zamani CCM katika tukio la Kibwibwi – Wilaya ya Kibiti
5. Kuua Afisa Mtendaji, Mwenyekiti wa Mtaa na Mkulima katika tukio la Kijiji cha Mangwi – Wilaya ya Kibiti

Ndugu Wanahabari
Wito wangu kwa Wananchi ni kuhusu mambo muhimu yafuatayo:

a. Wananchi wote nchini kuondoa hofu ya kwamba eneo hili si salama. Nawaomba wananchi waendelee kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi na kwa kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu. Aidha nawaomba wananchi kutoa taarifa mara moja kwa Jeshi la Polisi wanapohisi kuna jambo lolote wanalolitilia mashaka.

b. Natoa wito kwa wananchi wa mkoa wa Pwani, hususani maeneo ya Mkuranga, Kibiti na Ikwiriri, kuendelea na shughuli zao mbalimbali za kujiletea maendeleo. Nawasihi kwa dhati kabisa waendelee kutupatia taarifa zitakazosaidia kumaliza kabisa uhalifu kwenye eneo hili. Nitumie fursa hii kuwashukuru sana wananchi wa maeneo ya Mkuranga, Kibiti na Ikwiriri kwa ushirikiano mnaotupatia ambao umesaidia sana kuwadhibiti wahalifu.

c. Mamlaka za Hospitali, Zahanati, Vituo vya Afya, Maabara za Afya ya Binadamu na Maduka ya Kuuza Dawa za kutibu Binadamu zijiepushe na utaratibu wa kutoa matibabu kienyeji au kificho kwa watu waliojeruhiwa bila kufuata taratibu za kisheria ikiwemo kupata taarifa ya Polisi “kupitia Fomu maalum ya kuruhusu matibabu (maarufu kama PF. 3)”. Wahalifu wakijeruhiwa ni lazima watafute matibabu.

Kwa hiyo idara hizi ni muhimu sana kutoa ushirikiano ili kutuwezesha kuwakamata watuhumiwa maana baadhi yao wamekutwa na majeraha sehemu mbalimbali za miili yao na walikuwa wanaendelea kujitibia kwa kificho kwa kutumia dawa za hospitali.

Natoa wito kwa Mamlaka hizo kutoa taarifa mara moja kwa Jeshi la Polisi wanapoona ama kumbaini mtu ambaye ataonekana kuwa na majeraha na anatafuta tiba bila ya kufuata taratibu.

Ndugu Wanahabari
Napenda kuujulisha Umma kwamba wapo baadhi ya Watuhumiwa, Wafadhili na Washirika wa Uhalifu na Wahalifu wa ujambazi maeneo haya ambao bado hawajakamatwa. Jambo la kufurahisha ni kwamba taarifa zao zipo kwa Jeshi la Polisi nchini na zinaendelea kufanyiwa kazi ili waweze kukamatwa na kufikishwa kwenye mkono wa Sheria mara moja.

Natoa wito kwa wananchi ambao wanawafahamu watuhumiwa wafuatao kutoa taarifa katika kituo chochote cha Polisi ili waweze kukamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria.

Picha za watuhumiwa hao zitasambazwa kote nchini ili iwe rahisi kuwabaini. Majina ya watuhumiwa hao ni:
i.Anafi Rashid Kapelo @ Abuu Mariam
ii. Hassan Haruna Kyakalewa @ Abuu Salma @ Shujaa @ Dokta
iii. Haji Ulatule
iv. Shekhe Hassan Nasri Mzuzuri
v. Rashid Mtutula

Ndugu Wanahabari
Nimalizie kwa kusema kwamba uhalifu kwenye eneo hili ni suala la muda mfupi. Na tunaendelea vizuri sana. Hali ya usalama imeimarika sana eneo hili. Nazidi kutoa wito kwa wananchi kuendelea kuliunga mkono Jeshi la Polisi ili kufikia malengo yake ya kuzuia, kubambana na kutanzua uhalifu nchini.



Imetolewa na;

Simon Nyakoro Sirro
Inspekta Jenerali wa Polisi
IKWIRIRI
10.08.2017
Hongera mkuu kwa kazi nzuri sana ya kwako na ya jeshi lako la polisi na wananchi wanaotoa ushirikiano na nyie.Visisimizi vichache haviwezi kumuhamisha mwenye nyumba
 
Hivi polisi wakijeruhiwa ndio furaha yenu?
Risasi za majambazi za MCHANGA au maanake hata POLISI aliyejeruhiwa hakuna
Why kila mtu anaulizia kuhusu kutojeruhiwa kwao? So, baada ya majeraha ndio mtaamini utokeaji wa tukio. Yaani napata tabu sana kumeza hili
 
Hell no. .that shouldn't be the way!
Washukiwa hawatakiwi kuuwawa hata kidogo.....

Kazi ya police ni ku enforce law and order na sio judgement......

Tukiwaachia police uhuru huo... Tumekwisha.

Hili ni kwa Usalama wetu sote, Hakuna Chama Wala Ushabiki kwenye mambo kama haya......
Maana wao walikua wanafata Sheria..? Pambana na hali yako mkuu Yani waende kula Pesa ya serikali jela na mahakamani hapana warest in Peace tuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nadhani hujui unachokiandika, wewe ni mtanzania kweli? hayo majambazi unayatetea? tunakushangaa saana! Polisi tunawaunga mkono kwa asilimia mia kwa kazi nzuri na ngumu mnayoifanya.
cc. Mwigulu.
Hawa ndio wale magaidi acha kujisumbua

mchana toch ,usiku magogo tufanyaje?
 
Gud watu wa kibiti wawe na amani tena...
Lakini polisi wamenichekesha kidogo yaan waliwajeruhi majambazi kibiti afu wanawakimbiza muhimbili kwa matibabu yaan kibiti hakuna hospitali karibu sasa mtu anavuja damu atoke kibiti mpaka afike muhimbili mzima kweli
 
Gud watu wa kibiti wawe na amani tena...
Lakini polisi wamenichekesha kidogo yaan waliwajeruhi majambazi kibiti afu wanawakimbiza muhimbili kwa matibabu yaan kibiti hakuna hospitali karibu sasa mtu anavuja damu atoke kibiti mpaka afike muhimbili mzima kweli
Mkuu hujaelewa tu? [emoji2] [emoji2]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hell no. .that shouldn't be the way!
Washukiwa hawatakiwi kuuwawa hata kidogo.....

Kazi ya police ni ku enforce law and order na sio judgement......

Tukiwaachia police uhuru huo... Tumekwisha.

Hili ni kwa Usalama wetu sote, Hakuna Chama Wala Ushabiki kwenye mambo kama haya......
Kwa hiyo polisi ndo wanatakiwa kuuwawa? Hata hivyo wameeleza majibizano ya Risasi ndo yaliyowasababishia majeraha wakafariki wakiwa njiani kwenda hospital.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hell no. .that shouldn't be the way!
Washukiwa hawatakiwi kuuwawa hata kidogo.....

Kazi ya police ni ku enforce law and order na sio judgement......

Tukiwaachia police uhuru huo... Tumekwisha.

Hili ni kwa Usalama wetu sote, Hakuna Chama Wala Ushabiki kwenye mambo kama haya......
Halkuw lengo lao kuwauwa,,, ndo maana walwaahisha hospital

Sent from my PTM-Z-mini using JamiiForums mobile app
 
Wanapeleka watu kule na kuwapiga risasi na kuwawekea bunduki na silaha halafu wanajitekenya kuwa tumeua majambazi kibiti. Ndio tatizo la afrima uongo mwingi kwa kuogopa kufukuzwa kazi. Kwani unafukuzwa kazi pasipo hata kuchunguza kosa. Hakuna majambazi ambao tunaambiwa ni waliobobea na wamepata mafunzo nje leo hii wakae pmj. Watu wanapelekwa kibiti wanauwawa then polisi wanasingizia majambazi wa kibiti. Tusubiri muda utasema ndio polisi tanzania
Nonsense

Sent from my PTM-Z-mini using JamiiForums mobile app
 
Hell no. .that shouldn't be the way!
Washukiwa hawatakiwi kuuwawa hata kidogo.....

Kazi ya police ni ku enforce law and order na sio judgement......

Tukiwaachia police uhuru huo... Tumekwisha.

Hili ni kwa Usalama wetu sote, Hakuna Chama Wala Ushabiki kwenye mambo kama haya......
ndemwaaa..kwenye majibizano ya risasi kama hayo...na mashine walizonazo unafkir unashka kuku....JUST MURDER DEM


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hongera sana kamanda,picha na taarifa ndizo zinazozidi kuimarisha imani kati ya police na wananchi kwamba jeshi letu linapambana kutupigania na tushirikiane kutoa taarifa.
 
mie bado nasubiri motive ya hicho kikundi cha MKIRU. Hadi sasa serikali imeweka 3 motives; dini (JPM na Mwigulu wamehusisha na mashehe wa uamsho), siasa (CUF/CHADEMA wamehusishwa kwa nyakati tofauti na ugaidi. Sasa serikali ituwekee na ushahidi which is which motive sie wananchi tuishike maana kwa kila motive moja ambayo serikali imeitaja ina socio-economic and security impact zake
 
Pongezi nyingi kwa polisi wetu kwa kazi nzuri baada ya muda mrefu wa usumbufu na mauaji kibiti! hatimaye angalau tumaini linarudi!!!
Lakini huwa najiuliza, hivi wale panyarod 1000 waolikamatwa Dar kipindi kile waliishia wapi??
 
Back
Top Bottom