Majaribio mawili ya Israel kulipiza kisasi kwa Iran yameshakwama ndani ya wiki moja. Hasira zake zinaishia Gaza

Majaribio mawili ya Israel kulipiza kisasi kwa Iran yameshakwama ndani ya wiki moja. Hasira zake zinaishia Gaza

Webabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2010
Posts
8,870
Reaction score
14,258
Tangu Iran iishambulie Israel haijafika wiki moja.

Ndani ya muda kwa hasira ilizokuwa nazo Israel na namna ilivyovuliwa nguo hadharani tayari imejaribu kutaka kurudisha kipiga lakini hatimae ikashindikana.Sasa inatarajiwa itakuwa siku ya Jumatatu ijayo.

Katika kipindi hicho cha ndani ya wiki moja Israel imeona isikae kimya bali iongeze nguvu kwa mnyonge wake Gaza.

Baadhi ya vikosi vya Israel vilivyoondoshwa Gaza vimerudjishwa kuendelea kupiga maeneo ya kaati ya Gaza ilipo kambi ya Nusreita ambapo watu zaidi 100 wameshauliwa .

Mara baada ya shambulio kutoka Iran, viongozi wakuu wa Israel walisema hawana tena tarehe maalum ya kuingia Rafaha.

Hata hivyo katika siku chache zilizopita mashambulizi kutoka angani kwa eneo hilo ndio yameongezeka na kupelekea watu wengi kufa wakiwemo watoto,akinamama na wazee.

Israel aborted two planned retaliatory strikes against Iran: Sources

Israeli tanks push back into northern Gaza, warplanes hit Rafah

1713427783693.png
 
They will hit them where it hurts in an appropriate time.
Hakuna shaka watapiga tu kama tulivyojua Iran nao wangepiga.
Muhimu wakishapiga nini kitafuata.Itakuwa ndio mwisho au ni mwendelezo tu wa mzozo wa dunia nzima.
 
Iran awe makini sana muda huo , hizo za kupeleka vikosi Gaza ni kumpoteza maboya, tena siku zijazo unaweza kuzuka mzozo fake kati ya netanyahuna mawaziri wakimlaumu Netanyahu kuwa tusijaribu kuipiga Iran kwamba Iran ataiangamiza Israel ili Iran aendelee kujipiga kifua .
 
Hali ni ngumu kwa Israel.Hakuna ujanja wa kumlaumu Netanyahu wala vikosi fake.
Kila kitu kwa Israel kwa sasa ni kweli tupu.
 
Katika kipindi hicho cha ndani ya wiki moja Israel imeona isikae kimya bali iongeze nguvu kwa mnyonge wake Gaza.
Mara hii Gaza ya Hamas imegeuka mnyonge wa mazayuni. Makubwa haya. Hamas wameshindwa kuwalinda?

Baadhi ya vikosi vya Israel vilivyoondoshwa Gaza vimerudjishwa kuendelea kupiga maeneo ya kaati ya Gaza ilipo kambi ya Nusreita ambapo watu zaidi 100 wameshauliwa
Hii hatari sana maana roho 100 kufariki si jambo dogo. Lakini chanzo cha yote haya ni nini? Dhambi, ubaguzi na kujimilikisha Mungu

Mara baada ya shambulio kutoka Iran, viongozi wakuu wa Israel walisema hawana tena tarehe maalum ya kuingia Rafaha.

Hata hivyo katika siku chache zilizopita mashambulizi kutoka angani kwa eneo hilo ndio yameongezeka na kupelekea watu wengi kufa wakiwemo watoto,akinamama na wazee.
Hii ni mipango yao, wanaweza kusema wanataka kumbe hawatltaki. Tuwaachie wenyewe ila tuzidi kuomba vita iishe maana si askari wa Hamas au Wazayuni wanaojuta na kuuawa kwa wingi
 
Mara hii Gaza ya Hamas imegeuka mnyonge wa mazayuni. Makubwa haya. Hamas wameshindwa kuwalinda?
Ni kweli ndiye mnyonge wake.Kwa Iran lazima ajiulize maswali kwanza
 
Back
Top Bottom