Majaribio ya SGR Dar mpaka Morogoro yakwama, Vichwa havijakamilika kutengenezwa

Yaani miaka minne vichwa hawajakamilisha kuvirepair? Maana haya mabehewa ni used scrap ambayo wameyapiga tu rangi tena kwa bei kubwa kuliko ya mapya!
 
Mkakati namba moja nikusitisha vibali vya huduma mbadala; kwahiyo mtakua hamna option zaidi ya kupanda rejea mwendokasi Dar!
 
Kipindi fulani nilikuwa napenda kudandia tren nakaa kwa wale klina. Yule klina alikuwa akisema, treni ya abiria ilikuwa ni kwa ajili ya kutoa huduma lakini TRC hawapati faida kabisa kupitia kubeba abiria. Treni yenye faida ni ile ya mizigo.

Sasa tukija kwenye hoja ya SGR. Mimi nilikuwa najua kwamba kazi mojawapo ya serikali ni kutoa huduma za kijamii, na huduma mojawapo ni miundombinu ya usafirishaji haijalishi inapata faida au la!

Kwahiyo, hiyo SGR hata kama itabeba watu ni sawa tu ili Wanzania wawahi mishe zao kwa sababu tunalipa kodi katika vyanzo mbalimbali. Pia, tuna madini na rasilimali nyingine kibao.

Kwani sisi Watanzania hatutakiwi kutumia vitu vizuri jamani? mpaka mizigo tu?

Kwani huko India nchi yenye mtandao mkubwa wa reli duniani wanasafirisha mizigo tu?

Kama ikiwezekana SGR ijengwe na kuunganisha mikoa yote Tanzania ili Watanzania wafurahie kodi zao wala haina shida!

Sent from my Infinix X612 using JamiiForums mobile app
 
Ni ngumu na haiwezekani kujenga nchi nzima Katika mfumo wa SGR sababu ni, Gharama ni kubwa, Matunzo (Maintainance), Tija(Profitability). Hizi tunazojenga tumejikamua sana, maana hakuna nchi katika Africa ina SGR kuzidi Km 1200 plus. SGR ndefu kwa Africa ipo Morroco(kama km 700), Egypt chini ya km 300, Ethiopia - Djibout chini ya Km 600, Kenya haitumii Umeme. Tanzania SGR ni km 1,900plus, kwa urefu inazizidi SGR za Turin - Milan Italia, London - Paris, London - Munich kama miradi yote itaisha. Kujenga SGR unaitaji nchi yenye roho ngumu, maana zipo nchi zina mafuta lakini hazijengi.
 
Aisee! Kazi ipo! Yetu macho

Sent from my Infinix X612 using JamiiForums mobile app
 
Kwan ni kosa dar kulisha mikoa mingjne ,sasa wasipo jega barabara ama reli watapitia wapi sasa .Kwan madini hayapo mikoa mingjne ni mpaka congo.sasa kama barabara zinaharibka upande mmoja huoni umuhimu wa reli? Hii nchi n kubwa tuwe serious
Rudi nyuma uelewe tulipoanzia kutofautiana, itakusaidia sana kuliko kuanzia hapa
 
Upo sahihi kabisa.
 

Inaonesha hufanyi biashara nenda kigogo tu pale kaangalie watu wanavo pack mizgo yao watu wanafanya biashara wanaagiza mizgo mingi tu.
 
Nimepanda treni ya kutoka kigoma kwenda dar hivi karibuni, tabora behewa la kwenda mwanza lilikuwa ni moja tu. Yani angalau treni ya mpanda inajaza lakinj sio ya mwanza !
Halafu ondoa makasiriko na watu wa dar haikusaidii!
Na vile vile anatakiwa ajue kuwa hiyo hiyo treni ya mwanza zilikuwa kwa wiki mara mbili ila kwa sasa moja imeondolewa kwasababu hakuna abiria wa kutosha sasa unapoteza lita 2000 kwa abiria 70?
 
Inaonesha hufanyi biashara nenda kigogo tu pale kaangalie watu wanavo pack mizgo yao watu wanafanya biashara wanaagiza mizgo mingi tu.
Kigogo ni mizigo inayotoka dar kwenda mikoani. Niambie Kanda ya ziwa inapoelekea Sgr kuna mizigo gani itakayoweza kusustain behewa za sgr
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…