Majasusi wabobezi 8 wa Kitanzania wakamatwa nchini Malawi

Majasusi wabobezi 8 wa Kitanzania wakamatwa nchini Malawi

Nakumbuka kuna uzi mmoja huko nyuma tena mwaka huu huu niliandika kuhusu mapungufu makubwa ya Idara husika hasa kwa Watendaji wake wa sasa na jinsi wanavyokuwa recruited ila nilichoambulia ni lawama, kashfa na matusi japo baadhi nashukuru Mungu walinielewa na bahati nzuri leo kile kile nilichojaribu kukizungumzia na madhaifu yake kimejidhihiri huko nchini Malawi na sasa tunaanza kutafutana.

Muwe mnaheshimu mawazo ya Watu humu kwani kuna wengine japo hawapo humo Kwenu Kikazi lakini Umossad wao ulianzia tokea wakiwa tumboni bado hawajazaliwa na wanaweza wakawa wana ujuzi wa haya mambo pengine hata kushinda mlioajiriwa humo.

Mkuu naungana kabisa na Wewe tena kwa 100% kuwa kama hizo Njemba za Kiudukuzi zingekuwa imara wala wasingekamatwa hivyo na jambo la aibu sana. Bado nasisitiza kuwa mabadiliko makubwa sana yanahitajika kufanyika katika hiyo idara hasa kuanzia ngazi ya kugundua Kipaji, Kumfunza na kumfanyia Uchunguzi wa kina ( Vetting ) na kuimarisha kule Vyuoni mwao wanakopikwa.

Hakuna uthibitisho uliokwishatolewa kuwa hao waliokamatwa ni majasusi kutoka Tanzania,
Pamoja na hayo, hakuna idara iliyokamilika kwa 100%, mapungufu lazima yawepo, Mossad, CIA, KGB wote wanafanya makosa, na mengine ni makubwa tu ya kutia aibu Kama kuwa na Jenerali mkubwa katika jeshi ambaye ni jasusi wa nchi adui kwa takribani miaka 10!
Angalia mambo kwa upana kabla ya kuhitimisha na kudidimiza nchi yako
 
Wachinjwe tu...tabia za kispy hatupend sisi...tena wanabahat maana wangekamatwa na boko haram wangechnjwa kabsaa....
 
Tambua kuna wengine yawezekana hao waliokamatwa ni Wanafamilia wetu hivyo kupata taarifa zao ni jambo la Kisheria na la Kikatiba kabisa. Siku nyingine jaribu kuhifadhi kidogo ujinga wako hata kwa muda tafadhali! Mbona wale Makomandoo Wetu ambao kimsingi huwa hawatakiwi kujulikana kivile kutokana na Unyeti wao ila Yule mmoja wao alipofariki Watanzania hatukufichwa na tuliambiwa kuwa alikuwa ni Leutenant Rajab?

Hakuna haja ya sisi kuwajua, jukumu langu mimi na wewe ni kulipa kodi na yeye(jasusi wetu) kulipwa mshahara na kufanya kazi yake mojawapo ni kulinda mipaka yetu kwa kujua majirani zetu wanafanya nini.

Wewe kama kuna mwanafamilia wako alikuambia yeye ni jasusi na akakuaga ameenda malawi kuwachunguza wasiliana nae kama hapatikani nenda ofisini kwake kamuulize bosi wake.

Sio sawa kutaka watu na kazi zao waanikwe kwenye jamii wakati wenyewe hawakutaka jamii ijue wanafanya kazi gani na sio sawa kuwaamini Malawi tusiburi taarifa za serikali yetu. Itatuambia tunachotakiwa kukijua
 
Ila kukamata majajuc 8 kwa wakat mmoja sizan kama n kweli

Ila labda maana cc watanzania vichwa vyetu hivii

Wanakamatwa Makomandoo wa Kiwango cha juu kabisa wa Marekani tena kama Kuku huko Afghanistan na Iraq tena wakiwa kuanzia 10 na wananywea itakuwa hawa Wadukuaji sijui Wadukuzi wetu Mkuu? Halafu labda nikusaidie tu ni kwamba siku zote medani za Kivita au Kijasusi kinachozingatiwa pale ni timing, strategy na target na hapa ndipo unaweza ukashangaa imekuwaje Mtu uliyekuwa unamwamini kabisa lakini kakamatika kirahisi? Tatizo Vijana wenu wa siku hizi mnaowaajiri Vichwani mwao wanachojua ni kula tu bata, kubandua mademu na kuwahi kutupia mipcha yao kuwa leo yupo hapa mara kule na kujisahau wakati ukiwa katika mission tena very risky kama hiyo waliyopewa concetration inatakiwa iwe at the maximum level. Na kumbukeni pia kuwa Wamalawi baada ya sisi kuwaonyesha ile Mikwara yetu pale Uwanja wa Uhuru wakati Mama Joi akiwa madarakani nina uhakika walienda katika the drawing board na kuanza upya kupanga mikakati ya kupambana na sisi Kiusalama na Kiulinzi ili waweze kutukabili pindi kikinuka au tukilisanua.

Kuna Watu humu mnasema tena kwa kudhihaki kabisa kuwa hiyo ni Propaganda yao tu Wamalawi ila mmesahau kuwa katika Medani zozote za Kivita Propaganda ni deadly psychological weapon ambayo kama ikitumika vizuri mnaweza kumshinda Adui kiurahisi mno na hii Silaha nchi nyingi kubwa huitumia na hasa nchi ya Marekani ila Wamarekani wakaiimarisha zaidi ambapo hufanya sana Propaganda lakini on the ground wanajipanga vilivyo kukukabili adui sasa Wewe ukizubaa tu na kuamini Propaganda zao utakuja kukuta Wanajeshi wao wote unakula nao Chakula cha mchana Ikulu kwako huku ukiwaamkia tu Shikamoo kila mara.
 
Sasa majasusi gani wanatembea kwa pamoja .
.au masomo waliyofundishwa hawakuzingatia ..ujasusi mission kama iyo inabid mtu ajifanye kuomba kaz hapo hapo na kujifanya mmalawi wa asili
....au ndio huwa hawasomi mossad wanavofanya kazi
Unaonekana unaelewa kiundani Mkuu.Funguka 100%
 
Sasa majasusi gani wanatembea kwa pamoja .
.au masomo waliyofundishwa hawakuzingatia ..ujasusi mission kama iyo inabid mtu ajifanye kuomba kaz hapo hapo na kujifanya mmalawi wa asili
....au ndio huwa hawasomi mossad wanavofanya kazi
Hili wazo lako limenisumbua sana tangia jana. Iweje wote wanane waende eneo la tukio kwa pamoja. Tena gazeti la malawi linasema wanakijiji ndio waliwastukia kutokana na kubeba kamera kubwa kubwa na kuwaripoti polisi.

Pia taarifa ya malawi inasema mgodi umefungwa. Kwamba wapelelezi wanaenda kuchunguza kama kuna matengenezo ya silaha za nyuklia kwenye mgodi uliofungwa nalo linashangaza.
 
c'est un concept difficile à définiret dont la portée exacte suscite maintes

Oya Shemeji na Wenzako mnaoandika Vifaransa vyenu nitawachenjia sasa hivi. Hebu acheni hizo bhana! Kama mnajua na ma hamu sana ya kuandika Kifaransa chenu hicho hebu kamsaidieni basi Koffi Olomide au Werrason au JB Mpiana kuandika nyimbo zake. Serious please acheni hiyo. Nifah sema na Mumeo tafadhali!
 
Hili wazo lako limenisumbua sana tangia jana. Iweje wote wanane waende eneo la tukio kwa pamoja. Tena gazeti la malawi linasema wanakijiji ndio waliwastukia kutokana na kubeba kamera kubwa kubwa na kuwaripoti polisi.

Pia taarifa ya malawi inasema mgodi umefungwa. Kwamba wapelelezi wanaenda kuchunguza kama kuna matengenezo ya silaha za nyuklia kwenye mgodi uliofungwa nalo linashangaza.

Nini kinashindikana hapo Mkuu na unabisha kitu gani? Natamani nifunguke zaidi muelimike ila naomba niishie tu hapa tafadhali na niwaacheni mkitiririka.
 
Ninachojiuliza wamekamatwaje wote pamoja,
 
Majasusi kama nyumbu au kondoo wote wanakaa au kutembea pamoja au hata kuonekana tu wakizoeana? Kama ni wa kitanzania itabidi serikali ipitie upya uaandaaji wa hawa wasalama wake. Ni kushindwa kwa hali ya juu sana katika jicho la kiusalama. Revisit revisit revisit.....
Wabongolala mnachotwa kirahisi kweli na propaganda!!
 
Ninachojiuliza wamekamatwaje wote pamoja,
 
Wachinjwe tu...tabia za kispy hatupend sisi...tena wanabahat maana wangekamatwa na boko haram wangechnjwa kabsaa....

Mungu akusamehe tu,

Mungu ibariki Tanzania na Mungu wabariki walinda mipaka yetu
 
Back
Top Bottom