Nakumbuka kuna uzi mmoja huko nyuma tena mwaka huu huu niliandika kuhusu mapungufu makubwa ya Idara husika hasa kwa Watendaji wake wa sasa na jinsi wanavyokuwa recruited ila nilichoambulia ni lawama, kashfa na matusi japo baadhi nashukuru Mungu walinielewa na bahati nzuri leo kile kile nilichojaribu kukizungumzia na madhaifu yake kimejidhihiri huko nchini Malawi na sasa tunaanza kutafutana.
Muwe mnaheshimu mawazo ya Watu humu kwani kuna wengine japo hawapo humo Kwenu Kikazi lakini Umossad wao ulianzia tokea wakiwa tumboni bado hawajazaliwa na wanaweza wakawa wana ujuzi wa haya mambo pengine hata kushinda mlioajiriwa humo.
Mkuu naungana kabisa na Wewe tena kwa 100% kuwa kama hizo Njemba za Kiudukuzi zingekuwa imara wala wasingekamatwa hivyo na jambo la aibu sana. Bado nasisitiza kuwa mabadiliko makubwa sana yanahitajika kufanyika katika hiyo idara hasa kuanzia ngazi ya kugundua Kipaji, Kumfunza na kumfanyia Uchunguzi wa kina ( Vetting ) na kuimarisha kule Vyuoni mwao wanakopikwa.