Nimeona ka Djibouti kapo strategically sana japo ni kadogo nadhani Kenya wakiamua kwa uchumi wao wanaweza kuwapiku despite of mataifa mengi ya dunia ikiwemo America, France, Japan n.k kuifanya ile nchi ni watchtower yao.
Sasa mkuu Kenya huwa anafanya biashara zake na nchi gani ukiitoa Uganda maana bandari ya Mombasa ina mapato makubwa kuliko ya DSM?
Wewe sasa ndio Mtu unayeuliza maswali ya maana Sana.
1)Ethiopia imeshajenga reli hadi Djibouti tena ya umeme kwa kutumia mkopo wa wachina, hakuna jinsi kwamba Ethiopia itaacha kutumia hiyo reli yao ili kupata pesa ya kulipa deni.
2)Hivi karibuni Ethiopia wamemaliza tofauti zao na Eritrea, hivyo kuifanya bandari ya Eritrea kuwa karibu zaidi kwa kutumia barabara endapo reli itapata matatizo, kwahiyo Ethiopia haina sababu wala mpango wowote wa kutumia bandari za Kenya.
3)Kenya kwa ujumla, uchumi wake upo mashakani Sana kwa sasa, uchumi wa Kenya ulijengeka Sana kwa kutumia udhahifu waemajirani wake, hasa Tanzania.
Miaka yote ya kipindi cha mwalimu Nyerere, Tanzania ilisimamisha shughuli zote za maendeleo ili kujikita katika ukombozi kusini mwa Africa, bandari zetu zilitumika zaidi kusafirisha shaba ya Zambia na mazao yetu hapa Tanzania, hasa mkonge, bidhaa za nchi zote kuanzia Uganda, Eastern DR, Rwanda, Burundi na bidhaa zote za Viwandani za Kenya(Kumbuka Kenya manufacturing Industry ilikua mikononi mwa waingereza by95%) zilisafirishwa kupitia Mombasa.
Sasa hivi hiyo hali imebadilika ghafla Sana, hasa baada ya kuingia Magufuli, Kenya imepoteza Mzigo wote wa Burundi, imepoteza 95% ya Rwanda, almost 60% wa DRC, na 30% ya mzigo wa Uganda, hii ndio sababu China wamekataa kutoa pesa za SGR baada ya kuona kwamba mategemeo ya Kenya kusafirisha mzigo wa Rwanda na DRC haupo tena, hivyo umuhimu wa SGR ya Kenya kiuchumi, umepungua Sana.
Sent using
Jamii Forums mobile app