Maji ni huduma ambayo Serikali inafeli vibaya mno, uhaba na mgao karibu kila mkoa japo mabilioni yanatumika. Rais Samia anashindwa wapi?

Nipo chanika hapa huu mwezi sasa maji hayatoki ,dawasa bora mngetuacha na maisha yetu tulishayazoea mmeleta mimaji yenu maji yamekuwa ya shida kuliko mwanzo..
 
Mimi niko Njombe mjini hii ni wiki 2 hakuna maji tunatumia ya mtoni ambayo sio salama kabisa
 
Consumption, population growth and climate changes put pressure on resource availability
 
Sawa tuchukulie mfano hiyo Rusumo HEP station ambayo ni run-of-the-river maji ya mto Kagera yakauke je, hiyo hiyo Rusumo hydropower station wataweza kuzalisha umeme?
Mkuu unapendekeza tuache kutumia maji ili tuwe na maji ya kutosha kuzalisha umeme? Umeme una source mbadala lakini sio maji.
 
Mimi niko Njombe mjini hii ni wiki 2 hakuna maji tunatumia ya mtoni ambayo sio salama kabisa
Njombe ni green country! Mnakosaje maji huko? Na watu wa Singida watasemaje? Hawa viongozi hawako serious.
 
Njombe ni green country! Mnakosaje maji huko? Na watu wa Singida watasemaje? Hawa viongozi hawako serious.
Kwa kweli inashangaza sana na hapo ni mjini Mkuu sio pembeni ya mjini hapana ni mjini kabisa hakuna maji wiki ya 2 sasa sasa sijui wale wa nje mji hali ikoje
 
Nimelipia huduma ya kuunganishiwa maji huu mwezi wa 3 bila bila,ukifuatilia unaambiwa vifaa havijafika...sasa kama Dar inachukua 3months kuunganishiwa maji,je huko Wilaya ya Tanganyika hali ikoje?
 
Ni aibu kubwa kwa raifa lilo na mito, maziwa na bahari kuwa na mgao wa maji.
 
Mbezi Makabe, Msakuzi,Msumi, Mpiji mpaka leo hakujawahi kuwa na maji ya Dawasco.
Umeme umefika kabla ya 2010, maji kuna watu wanauza na magari ndio wanawahonga DAWASCO wasilete maji maeneo hayo ili biashara yao iwe nzuri.
 
Wakati wabunge wa upinzani wakiongozwa na Mh Myika kuishauri Serikali kujenga bwawa la Kidunda Ruvu mkoani Pwani, waldhihakiwa sana na wabunge wa CCM.
Leo maji shida Dar kila mtu anahangaika.
Huku Mbezi Beach garden zimenyauka maji ya kumwagilia hakuna
Sasa maji yanatoka mara tatu kwa wiki, sasa tunaona hadi maboza ya maji kwa ajili ya matumizi ya ndani,
 
Aisee maji hata uku kwetu yanasumbua sana.
 
Nimelipia huduma ya kuunganishiwa maji huu mwezi wa 3 bila bila,ukifuatilia unaambiwa vifaa havijafika...sasa kama Dar inachukua 3months kuunganishiwa maji,je huko Wilaya ya Tanganyika hali ikoje?
Mkuu hivi bado unaletewa vifaa vya kuunganisha maji? Sie tuliacha siku nyingi tunanunua wenyewe. Vile vifaa vingi vya maji kwenye maduka ya vifaa vya ujenzi sio kwa ajili ya idara za maji za serikali, ni kwa ajili ya watu binafsi kujinunuia! Serikali kununua ilikuwa enzi za Nyerere
 
Wale mabwana wakubwa hata connector tu ya 2500 hawanaga kwenye stoo zao. Daaah! Hapo ndo huwa nachokaga
 
Kwa ujumla Serikali inafanya kazi nzuri sana hata hivyo kwa mtazamo wangu wanavyotumia Nguvu kubwa kusambaza maji; Wangetumia pia angalau robo ya hiyo Nguvu Kuhuisha vyanzo vya maji.

Sasa hivi vyazo vya maji (chemchem)vingi vimevamiwa na kuharibiwa kwa asilia kama 85% hivi; hivyo pamoja na kazi nzuri ya Serikali ya kusambaza maji mfano kwa 80% huku nyuma utakuta kama asilia 40% ya vyanzo vimeharibika maana yake imesambaza kwa 40%. Tukiendelea na huu utaratibu maji hayatakaa yatoshe badala yake tunakuwa tunapoteza Bilions bure!

Long-term plan:
1. Kila wilaya, Tarafa, Kata, Kijiji, Kitongoji kitambue maeneo yao yaliyokuwa na vyanzo vya maji ( Chemchem) Yaboreshwe kwa kuotesha miti inayo support maji nk yawekewe mipaka... Kwa gharama za Wilaya na husika na sio kuchukulia mchezo mchezo. Taasisi yetu ya SUA inaweza kutupatia miti stahiki
Mfano: Mimi nilipo zaliwa najua Chemchem zote tulizokuwa tunachota maji na naamini kabisa tukizipanda miti stahiki na kuzuia shughuli zote za binadamu; ndani ya miaka 10 tutakuwa na maji yakutosha

2. Walioekeza kwenye vyanzo rasmi vya maji (Chemchem) wapewe Viwanja mbadala bure na pengine findia kiasi ili watoke na pawekwe mipaka raski (hapa nasema chemchem sisemei mito)

3. Hawa wataalam wetu waweze kutofautisha mto na Chemchem/Chanzo cha maji. Unaweza kusikia wapo huko wilayani wanakimbizana na watu wanaolima karibu na mto huku Chanzo cha maji/chemchem inakauka wala hawaipi uzito. Yaani sisi watu weusi sijui nani katuroga....

4. Suala la kulinda Vyanzo vya maji (Chemchem) lisiachiwe idara ya maji pekee; namaanisha, Baada ya kuvitambua na kuviwekea mipaka/Utaratibu, migambo wanaweza kutusaidia kuvilinda
Pengine Bunge lipitishe Sheria maalum inayotekelezeka (Inayowahusu watu wa kawaida na matajiri

5. Maji yabakie huduma kwa mtu anayotumia kwa matumizi yake na sio BIashara

Inauma sana kuona watu wanajenga/ wanafanya miradi kibao kwenye vyanzo vya maji (Chemchem) WAZI WAZI tena kwa gharama kubwa ya kukausha maji na hakuna mtu anayechukua hatua!!!
 
Mkuu, Tanzania kuna miji mingapi ya Wamasai na Wahdzabe? Hicho ndio kisingizio? Kwanza tangu Wamasai wahamia Vigwaza njia ya Morogoro sijaona kama wamehama, miaka zaidi ya ishirini sasa
inasikitisha sana kuona mtu anamtazamo wa kizamani kama huo na cha kushangaza utakuta yupo RUWASA,mfano mzuri ni mradi wa maji wa ruwasa kijiji cha lopolun na lemishiri kata ya oloirien wilaya ya ngorongoro mradi umezinduliwa na mwenge lakini yamebaki mapambo tu hakuna usambazaji wa maji kwa wananchi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…