Maji ya kipindi cha Nuhu kutengeneza Safina yalienda wapi?

Labda nikuulize mleta uzi,,,kwan kuna mvua ipi iliyonyesha kabla ya ile ya wakat wa nuhu?
 
Badala ya kuwashangaa hao wengine mi nakushangaa wewe.
 
Yapo angani ,ukweli ni kwamba kiasi cha maji yaliyopo angani(mvuke na mawingu) ni kikubwa kuliko hata maji yaliyopo kwenye bahari zote na chini ya ardhi,kwa sababu kuna mawingu mengine yanayofanya giza na kumfunika Mungu.
 
Jibu sahihi ni kwamba hizo ni hadithi za kusadikika, hapakuwepo na kitu kama hicho.
 
Yapo angani ,ukweli ni kwamba kiasi cha maji yaliyopo angani(mvuke na mawingu) ni kikubwa kuliko hata maji yaliyopo kwenye bahari zote na chini ya ardhi,kwa sababu kuna mawingu mengine yanayofanya giza na kumfunika Mungu.

Aisee, nimeshindwa hata kucheka

Eti yanafanya Giza na kumfunika Mungu, Duuuh
 
Akili yako itakua haina akili,kwani ww toka uzaliwe mvua zilianza kunyesha enzi na enzi jiulize hayo maji toka miaka ya 1200 yanakwendaga wapi?
 
Nami naomba nikuulize,

Maji ya mvua ya El niño ya mwaka 1997/1998 yalienda wapi?
 
Maandiko ya biblia yametujenga katika kuishi kwa hofu ya Mungu.
Hivyo kitendo chochote cha kufikiri kinyume na maandiko kinatafsiriwa kama dhambi na kutomuogopa Muumba.
Vinginevyo endapo utajaribu tu kuiondoa hofu hiyo (ingawa ni dhambi) na ukarejea kusoma biblia basi utawacheka sana na kuwadharau watu wa kale kwa mambo mengi waliokuwa wakiyafanya.
Post za watu wengi hapa zinaonyesha ni jinsi gani hofu ya Mungu inavyoondoka kwenye mioyo ya wengi...
 
Ni sawa na mie ninavyowaza na kupata jibu kuwa huenda bustani ya Edeni ilikuwa Tanzania pale Ngorongoro crater kwa sababu hizi mbili kubwa... Kwanza tunaambiwa binadamu walikuwa wanaishi na wanyama enzi zile kwenye bustani.. hadi leo hakuna sehemu nyingine duniani ambapo wanyama wanaishi kwa amani na binadamu isipokuwa Ngorongoro crater, na ndiyo maana imekuwa kivutio cha watalii kutoka pande zote za Dunia.. Pili, hadi leo tunaambiwa kwamba Fuvu la binadamu wa kwanza lilivumbuliwa na Dr Leakey eneo la Olduvai Gorge,na kwa vipimo vya C14 kweli linaonekana ndio fuvu la binadamu wa kwanza.. hadi leo hakuna mwanasayansi yeyote duniani aliekuja na masalia yenye umri unaopita yale ya Dr Leakey.. na ukiangalia Olduvai gorge ni sehemu y huko huko Ngorongoro... Sasa hatuoni kuwa hilo fuvu ni la Adamu/ Hawa? kwa nini pale pasiwe ndo Bustani ya Edeni?
 
Neno la Bwana siyo hadithi za kusadikika hata kidogo, umeuliza swali la kiimani/kiroho bhasi uwe tayari kupata jibu la kiroho na siyo jibu la ulimwengu halisi, jibu ni kuwa maji ya gharika wakati wa Nuhu yalitoka ardhini na mengine juu mbinguni kama adhabu ya kuangamiza kile kizazi kichafu, hata hivyo baada ya mda alioupanga Bwana kuisha, maji yale yapo yalioingia kwenye vyanzo vya maji na mengine yaliingia chini ardhini.
 
Inasadikiwa kuwa nuhu aliishi miaka 950...anza kujiulizia hapo
 
Nuhuu alitumwa kwa watu wa kaumu yake(umma)wake.Hivyo adhabu ile ya gharika ilikuwa ni kwa mji alioishi nuhuu(a.s)kwa mujibu wa Quran
Hivi qaum mbili zishawahi ku exist kwa wakati mmoja? Kwa maana mitume su manabii wawili walikuwepo duniani na umma zao TOFAUTI?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…