Maji ya kujaza Bwawa la Nyerere yatatoka wapi?

Maji ya kujaza Bwawa la Nyerere yatatoka wapi?

Kwa mabadiliko haya ya Tania nchi, Je? Bwawa la Nyerere huko Selous litajaa maji kweli, alafu baada ya muda gani?.

Mwenye data za kitaalam atutoe wasiwa isijekuwa tunafanya politik huku hela inaenda na upepo.

Vinginevyo tujiimarishe kwenye gesi na makaa ya mawe pamoja na renewable energies bila kujali kelele za COP26.

Tujixoeze kuwa wakweli hata kama tunaona ukweli haupendezi.
Kwa mvua hizi za kuunga unga kwa kamba huenda likajaa kwa mwaka mmja badala ya miezi 6 inayotakiwa..
 
Kwanini lisijae wakati sahv kuna mvua

Haya leteni kizingizio kingine wazaa wa mipango

Ova
 
Soon mgao utakua historia tuendelee kumtakabal Allah. Hakuna kiongozi anaeombea shida watu wake.
 
Litajaa lakini linahitaji plan wakielekeza maji yote ya mto watu watakufa njaa, watenge hata miaka minne yakulijaza kidogo kidogo.
 
Watu wa dili wanaumbuka mvua zinapiga usiku kucha
Wapi zinakopiga usiku kucha? Mvua Ni za kuunga unga na Kama unadhani zinapiga usiku kucha Lima bila hesabu afu uje hapa mwezi wa 4..

Mpunga tuu hatuna uhakika Kama tutaivisha kwa mabonde yetu yanayoyegemea mvua
 
Litajaa vzr tu..hata usiwe na hofu..wasiwasi wangu je ukuta ni imara je kweli umeme utadhlishwa hizo megawat 1500??

#MaendeleoHayanaChama
MW 2100 mkuu! Kama Mtera iliyojengwa mwaka 1986 inauwezo wa kuzalisha MW 80 miezi 7 atakama mvua haijanyesha ndiyo Nyerere Dam lishindwe kuzalisha MW 2100 mwaka mzima atakama mvua hazijanyesha!
 
Ukimskiliza chande midaa kwenye space inaonekana gesi nayo ni miyeyusho kwenye mambo ya impact ya hali ya hewa so maji ndo kila kitu kwa nchi zetu hizi labda tuhamie kwenye nyukilia
 
Kwanini lisijae? Hayo maji yote yanayoingia baharini yashindwe kujqza hilo bwawa?Tanzania haina shida ya maji bali shida ya akili na ufahamu...pamoja na ukame wa muda mrefu hizi mvua zinazonyesha sehemu kubwa ya maji bado yanaingia baharini

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Swala sio mvua kuanza Bali Ni mvua za kiwango gani?

Kama zimeanza mbona Ruvu haijai ili Kuondoa changamoto ya maji Dar?
Topic ni Bwawa la Nyerere kinajitegemea mto Rufiji.

Kuhusu DAWASA inayotegemea mto Ruvu, huku kwetu ni wiki Sasa maji yanatoka vizuri tu.
 
Back
Top Bottom