DOKEZO Maji ya kuoshea maiti yanayo lalamikiwa kutumika kuhifadhia samaki yanauzwa kwenye maduka ya dawa za asili, Serikali imulike huko

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Ninao SPIRITUAL, so ukiutaka nitakupa, kama ambavyo UCHAWI, upo lakini hauthibitiki mahakamani.

Akili za kibinadamu Zina mipaka.

Sijui kama nimekujibu sawasawa.
Aisee ???!!! Kwa mtindo huo.... Dah! hujaumbwa kwa sura na mfano wa Mungu. Yaani ninamaanisha tumia Akili zako zote hadi uone basi umeshindwa ndio uanze kuingia mambo ya Kiroho.
Ni ukweli usiopingika kwamba akili za binadamu zina mipaka na ni vyema na busara kufika kwanza kwenye hiyo mipaka ndipo sasa uanze kujiongeza. (Samahani lakini kama nimekukwaza)
 
Nafikiri hii ndo hoja nzito yenye logic. Serikali muache siasa kwenye maisha ya watu.

Ila ili swala pia la maji ya maiti kuhifadhia samaki ndo nimelijua leo, hakika limenivuruga, ingekuwa ni sheria yangu wote hawa wanastaili kunyongwa tu, huwezi mlisha binadamu mwenzako vitu vya hovyo kisa upate faida.
Labda hayo maji yatumike kishirikina, lakini sidhani yana kitu chochote cha kuweza kusaidia samaki wasiharibike haraka maana ni maji tu kama maji mengine.......tofauti ni kwamba yametumika kuoshea maiti. Ni sawasawa na mtu akwambie maji uliyooga yakabaki unaweza kuyatumia kuhifadhia samaki na yanaweza kusababisha kansa. Tatizo ngozi nyeusi tunapenda speculations tu na story za vijiweni ambazo hazina msingi wowote wa kisayansi.​
 
Madawa ya maiti yananuka kisenge yakiwekwa kwenye fish lazima ujue tu
K

kwaiyo mheshimiwa alielisemea hili alikurupuka hakufanya utafiti wa kina, manake hadi mtu kusema kuna hamsini ya ukweli, labda tuseme wanachanganya na vitu vingine kuondoa harufu.
Mawazo yako Mkuu
 
Sgang wanakomeshwa. Hawajali kuwa samaki Victoria wanaleta foreign currency Kwa kiasi kikubwa ktk Nchi?
Wanakomeshwa na nani? Mbona unataka kupenyeza hoja za kisiasa tena kwenye uzi huu wenye mustakabali wa Afya zetu sote?
 
K

kwaiyo mheshimiwa alielisemea hili alikurupuka hakufanya utafiti wa kina, manake hadi mtu kusema kuna hamsini ya ukweli, labda tuseme wanachanganya na vitu vingine kuondoa harufu.
Mawazo yako Mkuu
Yaweza kuwa boss ila labda pia hajafanya tafiti ni hypothesis zake tu
 
Salaam,

Tafiti zinaonesha kwamba wagonjwa wengi wa Saratani wamekuwa wakitokea Kanda ya Ziwa jambo ambalo linapelekea Serikali kuhangaika kutafuta sababu kwanini Kanda ya Ziwa?

Jana nimeona Mh Makamu wa Rais akiwa hospitali ya Bugando ameeleza moja ya sababu inayopelekea takwimu za saratani kuwa juu Kanda ya Ziwa ni watu wanaotumia maji ya kuoshea maiti kuhifadhia samaki.

Nimeona niijulishe Serikali kwamba moja ya wateja wakubwa wa maji haya ni waganga wa kienyeji na maji haya yanauzwa kwenye maduka ya dawa asili.

Ili Serikali ifanikiwe kudhibiti usambaaji wa biashara hii nashauri wahakikishe masoko yote pamoja na mochwari ambapo ndipo yanapotoka wanadhibiti vinginevyo tatizo hili litaendelea.

Asante.
---

View attachment 2356409
Picha: Sehemu ya gazeti iliyoandika habari hii

Baada ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania DK. Phillip Mpango amesema ongezeko kubwa la ugonjwa wa saratani katika mikoa ya kanda ya ziwa unatokana na baadhi ya watu kutumia maji ya yanayotumika kuoshea maiti pamoja na dawa aina ya Cloroform inayotumika kuhifadhi samaki.

DK. Mpango alizungumza hayo wakati wa uzinduzi wa jengo la wagonjwa wa saratani katika huspitali ya rufani ya kanda Bugando jijini Mwanza, jengo ambalo limejengwa kwa gharama ya shilingi bilioni 5.6.

Baada ya kauli hiyo, inadaiwa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mwanza, Jana jioni ilianza kugawa fedha kwa waandishi wa habari kuzuia stori hiyo isitoke kwenye vyombo vya habari.

Taarifa kutoka ndani ya ofisi ya mkuu wa mkoa zinadai, fedha hizo zilikuwa zikitolewa na Katibu wa mkuu wa mkoa, bwana Matia Levi.

Inaelezwa zaidi ya waandishi 20 walipokea mshiko huo ili habari hiyo isiandikwe, lakini waandishi walipokea na kutoa habari hiyo.

Hata hivyo Leo mchana, Chama cha Mapinduzi mkoa wa Mwanza kitazungumza na vyombo vya habari kuhusu taarifa hiyo na inaelezwa wamesikitishwa na kauli ya Makamu wa Rais.
Propagation
 
Aisee ???!!! Kwa mtindo huo.... Dah! hujaumbwa kwa sura na mfano wa Mungu. Yaani ninamaanisha tumia Akili zako zote hadi uone basi umeshindwa ndio uanze kuingia mambo ya Kiroho.
Ni ukweli usiopingika kwamba akili za binadamu zina mipaka na ni vyema na busara kufika kwanza kwenye hiyo mipaka ndipo sasa uanze kujiongeza. (Samahani lakini kama nimekukwaza)
Naheshimu mawazo Yako.

Naomba unitofautishie kati ya
1. Maono. 2. Ndoto na chanzo chake na 3. Ulimwengu wa ROHO.
 
Watu wengi hawachemshi maji ya kunywa, mboga zinamwagiliwa na madawa ya kuulia wadudu na wanunuzi hawaoshi vizuri na hata ukiosha sumu inaingia kwenye mboga.
Utafiti wa kina ufanyike hasa kwenye vyanzo vya mito ili tujue kama hakuna sumu inayopelekwa mpaka kwenye hiyo mito na hatimaye kuingia ziwani.
Tukisema tuache kula samaki wa Ziwa Victoria tunawapa faida wakenya na waganda maana watavuna sana na sisi tunabaki maskini.
 
Labda hayo maji yatumike kishirikina, lakini sidhani yana kitu chochote cha kuweza kusaidia samaki wasiharibike haraka maana ni maji tu kama maji mengine.......tofauti ni kwamba yametumika kuoshea maiti. Ni sawasawa na mtu akwambie maji uliyooga yakabaki unaweza kuyatumia kuhifadhia samaki na yanaweza kusababisha kansa. Tatizo ngozi nyeusi tunapenda speculations tu na story za vijiweni ambazo hazina msingi wowote wa kisayansi.​
Yah!!! Hata mimi kama kuamini ningeamini hivyo ni swala la ushirikina,

sasa tukija kwa jamii zetu vile zinapenda kuendekeza mambo ya kishirikina kuna uwezekano mkubwa sana haya mambo yanafanyika aiseee,

Kuna kipindi nilishuhudia kwa macho yangu watu wakiwa na ndoo wakichota maji kwenye fukwe za ziwa, ilikuwa jioni ya saa mbili. Mwenyeji akaniambia, asubuhi kuna maiti imeonekana hapo ufukweni, sasa hayo maji wanaenda kuchanganya kwenye Chakula ili kuvutia wateja.
Nilichoka.
 
Sawa vegetarian, sikutishi. Omba tu na Kila kiti kitakuwa sawa.

Nmekumbuka kiti, Mahindi usinunue unga, nenda nunua Mahindi halafu yaoshe mwenyewe ndo usage unga, Kuna dawa ya kuzuia wadudu kubungua pia husababisha saratani.

Ndugu vegetarian, hujiulizi APPLE linatoka south Afrika linakaa container zaidi ya mwezi Bado unalikuta fresh???
Tuwekane sawa hapa, apple 🍎 zinatuhumiwa kuhifaziwa kwa "dawa ya kuhifazia maiti" je na hayo maji kazi yake ni ipi hasa? Kuhifazi au ni "shirika " mpango shirikishi wa kuvuta wateja?
 
Labda hayo maji yatumike kishirikina, lakini sidhani yana kitu chochote cha kuweza kusaidia samaki wasiharibike haraka maana ni maji tu kama maji mengine.......tofauti ni kwamba yametumika kuoshea maiti. Ni sawasawa na mtu akwambie maji uliyooga yakabaki unaweza kuyatumia kuhifadhia samaki na yanaweza kusababisha kansa. Tatizo ngozi nyeusi tunapenda speculations tu na story za vijiweni ambazo hazina msingi wowote wa kisayansi.​
Hapa ni ishu za kishirikina hasa mvuto.. Hayo maji lets say lita moja yatafanyiwa manuizi na kuchanganywa na madawa mengine kisha po ndio yataenda kutumika na hicho kiasi kinaweza kuhudumia zaidi ya hata tani moja kwakuwa yanatumika kidogo Sana kwa kila mzigo

Haha hivyo hili ni jambo geni kuyatumia kama mvuto kwakuwa kwenye kaliba ya uchawi haya maji ni kitu mfu na huwa yanatumika kuharibu na kufisha na si kutengeneza

Sent from my LM-V500N using JamiiForums mobile app
 
Brother, sio kila samaki unayemkuta pale kamanga,mbugani au mwalo wa mswahili ni fresh..hawa wachuuzi wa samaki wamebuni mbinu nyingi za kuwafanya samaki kuwa fresh muda wote na hiyo mbinu huweza pia kutumiika....je wajua kwenye masoko ya mwanza wapo samaki (sato/sangara) wa kufugwa...tena wengi tu...na kama huna uzoefu huwezi wajuaaa
 
Salaam,

Tafiti zinaonesha kwamba wagonjwa wengi wa Saratani wamekuwa wakitokea Kanda ya Ziwa jambo ambalo linapelekea Serikali kuhangaika kutafuta sababu kwanini Kanda ya Ziwa?

Jana nimeona Mh Makamu wa Rais akiwa hospitali ya Bugando ameeleza moja ya sababu inayopelekea takwimu za saratani kuwa juu Kanda ya Ziwa ni watu wanaotumia maji ya kuoshea maiti kuhifadhia samaki.

Nimeona niijulishe Serikali kwamba moja ya wateja wakubwa wa maji haya ni waganga wa kienyeji na maji haya yanauzwa kwenye maduka ya dawa asili.

Ili Serikali ifanikiwe kudhibiti usambaaji wa biashara hii nashauri wahakikishe masoko yote pamoja na mochwari ambapo ndipo yanapotoka wanadhibiti vinginevyo tatizo hili litaendelea.

Asante.
---

View attachment 2356409
Picha: Sehemu ya gazeti iliyoandika habari hii

Baada ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania DK. Phillip Mpango amesema ongezeko kubwa la ugonjwa wa saratani katika mikoa ya kanda ya ziwa unatokana na baadhi ya watu kutumia maji ya yanayotumika kuoshea maiti pamoja na dawa aina ya Cloroform inayotumika kuhifadhi samaki.

DK. Mpango alizungumza hayo wakati wa uzinduzi wa jengo la wagonjwa wa saratani katika huspitali ya rufani ya kanda Bugando jijini Mwanza, jengo ambalo limejengwa kwa gharama ya shilingi bilioni 5.6.

Baada ya kauli hiyo, inadaiwa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mwanza, Jana jioni ilianza kugawa fedha kwa waandishi wa habari kuzuia stori hiyo isitoke kwenye vyombo vya habari.

Taarifa kutoka ndani ya ofisi ya mkuu wa mkoa zinadai, fedha hizo zilikuwa zikitolewa na Katibu wa mkuu wa mkoa, bwana Matia Levi.

Inaelezwa zaidi ya waandishi 20 walipokea mshiko huo ili habari hiyo isiandikwe, lakini waandishi walipokea na kutoa habari hiyo.

Hata hivyo Leo mchana, Chama cha Mapinduzi mkoa wa Mwanza kitazungumza na vyombo vya habari kuhusu taarifa hiyo na inaelezwa wamesikitishwa na kauli ya Makamu wa Rais.
Kuna upotoshaji mkubwa sana umefanyika hapo, hayo maji yenyewe kuyapata ni shughuli hasa na ukifanikiwa huwezi pata ndoo nzima

Sent from my LM-V500N using JamiiForums mobile app
 
Hapa ni ishu za kishirikina hasa mvuto.. Hayo maji lets say lita moja yatafanyiwa manuizi na kuchanganywa na madawa mengine kisha po ndio yataenda kutumika na hicho kiasi kinaweza kuhudumia zaidi ya hata tani moja kwakuwa yanatumika kidogo Sana kwa kila mzigo

Haha hivyo hili ni jambo geni kuyatumia kama mvuto kwakuwa kwenye kaliba ya uchawi haya maji ni kitu mfu na huwa yanatumika kuharibu na kufisha na si kutengeneza

Sent from my LM-V500N using JamiiForums mobile app
Tatizo linakuja pale mtu anapoyahusisha na saratani kuongezeka kanda ya ziwa, hii inakuwa sawa na story ya mtu aliyeiokota kijiweni. Tukimuuliza ni vitu gani au kemikali gani alizobainisha kwenye hayo maji na namna yanavyoweza kusababisha saratani hawezi jibu...
 
Amekurupuka period!

Back
Top Bottom