DOKEZO Maji ya kuoshea maiti yanayo lalamikiwa kutumika kuhifadhia samaki yanauzwa kwenye maduka ya dawa za asili, Serikali imulike huko

DOKEZO Maji ya kuoshea maiti yanayo lalamikiwa kutumika kuhifadhia samaki yanauzwa kwenye maduka ya dawa za asili, Serikali imulike huko

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
This is a very cheap argument, maji ya kuoshea maiti yana uhusiano gani na kutokea saratani.......do you have any mechanism behind.

Labda tuseme unamaanisha kemikali inayotumika kuhifadhi maiti, mfano formali, .hivi inaingia akilini utumie formalin kwenye samaki na isilete usumbufu kwa watu wanaohusika na wateja kwa kupiga chafya au kuwashwa machoni? Hizo kemikali are very pungent ukiifungua kidogo tu hapawezi kukalika.

Kama swala ni saratani inasabbishwa na hivyo vitu kutumika kuhifadhia samaki, logic inaonyesha kwamba case za saratani zingekuwa nyingi mikoa ya mbali na Mwanza maana ndo watatumia zaidi samaki waliohifadhiwa kuliko Mwanza ambako tutategemea watu wengi wanatumia samaki fresh ambao hawajahifadjiwa na kitu chochote.
Hawa watu wanajaribu kupotosha kiini cha saratani kuwa juu huko Mwanza sijui kwa maslahi ya nani. Wafanye utafiti wenye mashiko, tatizo la saratani kuwa juu kanda ya ziwa ni kutokana na kemikali za migodini zinazoelekezwa kwenye vyanzo vya maji ikiwemo mito na kuishia ziwani. Haya ndo yaleyale ya tume ya Manyere kwamba samaki wa mto Mara walikufa kutokana na kuzidiwa na kinyesi na mikojo ya ng'ombe. Pathetic!!

Point
 
Mahospitalini kuna eneo maalumu, ya kuoshea maiti, na maji yake huyatililiki hovyo maana, huunganishwa na bomba ambo huenda kwenye karo.

Sababu za kutumia maji ya maiti kuhifadhia samaki ni zipi?
1. maji ya kuoshea maiti huganda kama barafu, hivyo samaki hawaharibiki.

2. Maji ya kuoshea maiti ukiyaweka kwenye samaki, hufanya samaki wapate soka haraka.

Tuache kuharibu kazi za watu, ni ajira hizi.
 
Viongozi wa kitaifa wanapaswa kuongea mambo kwa reference ya tafiti siyo porojo tu.

Maji ya kuoshea maiti ndiyo yapoje? Hao sato na sangara waliojaa kwenye bucha za Dar wote ni wa kanda ya ziwa.

Yaani iwepo cheap method ya kuhifadhi samaki Kanda ya ziwa halafu isitumike maeneo mengine yenye mito na maziwa!!

Hii argument hai-hold water mazee,angalau ile ya chemikali za migodini.
 
Napingana na VP hiki kitu sio kweli,samaki wa mwanza wanaliwa hata nje ya mwanza, hapa dar tunakula sana sato mbona hatuna saratani? VP unalishwa matango pori waambie wafanye utafiti tena, hivi jinsi fomalini invotoa harufu ungeweza kula samaki kweli?hebu tuwe wakweli wagonjwa wengi pale ORCI wanatoka kanda ya ziwa sababu sio hio, sababu kuu ni zebaki inayotiririka ziwani na kwenye mito, wananchi wanatumia hayo maji na ndio maana waathirika wengi ni kutoka kanda ya ziwa, nendeni ocean road mkajionee wenyewe acheni kumdanganya VP.
 
Hili la dawa za kuhifadhia maiti huenda kwa kiasi lipo niliwahi kulisikia na DRC pia samaki kutoka south Africa/ Namibia wakiitwa thomsoo na tilapia, lakini hili la kanda ya ziwa limafikirisha saana kuhusiana na mambo ya migodi l.

Huko north mara utafiti ule uliishia wapi?.
 
This is a very cheap argument, maji ya kuoshea maiti yana uhusiano gani na kutokea saratani.......do you have any mechanism behind.

Labda tuseme unamaanisha kemikali inayotumika kuhifadhi maiti, mfano formali, .hivi inaingia akilini utumie formalin kwenye samaki na isilete usumbufu kwa watu wanaohusika na wateja kwa kupiga chafya au kuwashwa machoni? Hizo kemikali are very pungent ukiifungua kidogo tu hapawezi kukalika.

Kama swala ni saratani inasabbishwa na hivyo vitu kutumika kuhifadhia samaki, logic inaonyesha kwamba case za saratani zingekuwa nyingi mikoa ya mbali na Mwanza maana ndo watatumia zaidi samaki waliohifadhiwa kuliko Mwanza ambako tutategemea watu wengi wanatumia samaki fresh ambao hawajahifadjiwa na kitu chochote.
Hawa watu wanajaribu kupotosha kiini cha saratani kuwa juu huko Mwanza sijui kwa maslahi ya nani. Wafanye utafiti wenye mashiko, tatizo la saratani kuwa juu kanda ya ziwa ni kutokana na kemikali za migodini zinazoelekezwa kwenye vyanzo vya maji ikiwemo mito na kuishia ziwani. Haya ndo yaleyale ya tume ya Manyere kwamba samaki wa mto Mara walikufa kutokana na kuzidiwa na kinyesi na mikojo ya ng'ombe. Pathetic!!
Umenena vyema mwanza hawahifadhi samaki..samaki wanaohifadhiwa ndio wanaouza mikoa ya mbali na mwanza.

Makamu wa rais kapotoswa naye kaingia king.

#MaendeleoHayanaChama
 
Vyanzo vya saratani (cancer) Kanda ya Ziwa vinaweza kuwa vingi iwapo utafiti wa kisayansi utafanyika.

Niliwahi kutahadharisha kuwa matumizi ya sumu katika uvuvi haramu na matumizi ya zebaki yasiozingatia usalama wa afya za viumbe na mazingira katika migodi ya madini pamoja na matumizi yasiyo sahihi ya kemikali za kuua wadudu waharibifu katika mimea ni moja wapo wa vyanzo vikubwa vya saratani kwani sehemu kubwa ya kemikali zinazotumika katika shughuli nilizozibainisha hapo juu uishia kuingia katika vyanzo vyetu vya maji tunayoyatumia na kuishia kuleta magonjwa mbalimbali ikiwemo saratani.

Nashauri utafiti ujikite huko pia na tetesi za matumizi ya kemikali za kuhifadhia maiti kutumika kuhifadhia samaki/nyama zisipuuzwe.

Pia ni vyema serikali ikajizuia kutoa taarifa zisizothibitishwa kisayansi ili kulinda soko la samaki na nyama kwa masoko ya ndani na kimataifa na kuzuia taharuki inayoweza kujitokeza kwenye jamii tukizingatia umuhimu wa kitoweo hicho katika mlo wa kila siku.
 
Enhe! Hapo tena..... Mkuu, tumewaamini na kuwapa kazi ya Utafiti baadhi ya Watanzania wenzetu na kuwaweka katika Taasisi zitakazohusika na shughuli hizo. Endapo itabainika au hata kuhisiwa kwamba Utafiti na Majibu ya Utafiti huo Vitachakachuliwa basi ni bora ku-outsource shughuli hiyo na mchakato wa kumpata mtafiti au Consultant iwe ni kwa njia ya Tenda.( Lakini bro. ujue ni gharama kubwa).
Naamini hawatatuangusha ndugu zao !!
 
Salaam,

Tafiti zinaonesha kwamba wagonjwa wengi wa Saratani wamekuwa wakitokea Kanda ya Ziwa jambo ambalo linapelekea Serikali kuhangaika kutafuta sababu kwanini Kanda ya Ziwa?

Jana nimeona Mh Makamu wa Rais akiwa hospitali ya Bugando ameeleza moja ya sababu inayopelekea takwimu za saratani kuwa juu Kanda ya Ziwa ni watu wanaotumia maji ya kuoshea maiti kuhifadhia samaki.

Nimeona niijulishe Serikali kwamba moja ya wateja wakubwa wa maji haya ni waganga wa kienyeji na maji haya yanauzwa kwenye maduka ya dawa asili.

Ili Serikali ifanikiwe kudhibiti usambaaji wa biashara hii nashauri wahakikishe masoko yote pamoja na mochwari ambapo ndipo yanapotoka wanadhibiti vinginevyo tatizo hili litaendelea.

Asante.
---

Kauli Makamu wa Rais kuhusu maji ya kuoshea maiti Kusababisha kansa

View attachment 2356409
Picha: Sehemu ya gazeti iliyoandika habari hii

Baada ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania DK. Phillip Mpango amesema ongezeko kubwa la ugonjwa wa saratani katika mikoa ya kanda ya ziwa unatokana na baadhi ya watu kutumia maji ya yanayotumika kuoshea maiti pamoja na dawa aina ya Cloroform inayotumika kuhifadhi samaki.

DK. Mpango alizungumza hayo wakati wa uzinduzi wa jengo la wagonjwa wa saratani katika huspitali ya rufani ya kanda Bugando jijini Mwanza, jengo ambalo limejengwa kwa gharama ya shilingi bilioni 5.6.

Baada ya kauli hiyo, inadaiwa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mwanza, Jana jioni ilianza kugawa fedha kwa waandishi wa habari kuzuia stori hiyo isitoke kwenye vyombo vya habari.

Taarifa kutoka ndani ya ofisi ya mkuu wa mkoa zinadai, fedha hizo zilikuwa zikitolewa na Katibu wa mkuu wa mkoa, bwana Matia Levi.

Inaelezwa zaidi ya waandishi 20 walipokea mshiko huo ili habari hiyo isiandikwe, lakini waandishi walipokea na kutoa habari hiyo.

Hata hivyo Leo mchana, Chama cha Mapinduzi mkoa wa Mwanza kitazungumza na vyombo vya habari kuhusu taarifa hiyo na inaelezwa wamesikitishwa na kauli ya Makamu wa Rais.
Wamesikitishwa nini hao mafisi!!
 
Umenena vyema mwanza hawahifadhi samaki..samaki wanaohifadhiwa ndio wanaouza mikoa ya mbali na mwanza.

Makamu wa rais kapotoswa naye kaingia king.

#MaendeleoHayanaChama
Mtu mwenye PHD anapoargue kama muuza dagaa wa mwaloni!!!!
 
Kauli hii kutolewa hadharani na mtu mwenye hadhi ni hatari kwa ustawi wa soko na biashara ya samaki.

Niishie hapa labda ndio ripoti ya kisomi toka kwa watafiti.
 
Tahadhari hiyo imetolewa na Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango ambaye ameeleza kuwa matokeo ya uchunguzi wa awali uliofanywa na watalaam kuanzia mwaka 2021 umeonesha dawa za kuhifadhia samaki na maji ya kuoshea maiti ambayo hutumiwa na wavuvi kuvua Samaki ni chanzo cha Saratani.

Aliongeza kuwa Kanda ya Ziwa inaongoza kwa kuwa na wagonjwa wengi wa Saratani na kwamba watalaam wamechukua sampuli za damu kutoka kwa wananchi wa mikoa 8 ili kufanya uchunguzi.
 
Sasa si wachukue hatua haraka za kukomesha hilo suala! Kuna sababu gani ya kuharibu biashara ya kitoweo cha samaki wa Ziwa Victoria!

Au anataka tuhamie kwenye samaki aina ya migebuka kutoka kwao Kigoma?
 
Africa umaskini unatutesa sana tena sana, hatujali maisha ya wenzetu kwa sababu ya maslahi, hizi ndio athari za umaskini!
 
Samaki anayenunuliwa fresh kwa ajili ya kwenda kuliwa, unamwekea dawa ya kuhifadhi ili iweje........bei ya hao samaki ni kiasi gani hadi ugharamike kununua kemikali inayouzwa pesa nyingi na ambayo huwezi kuipata kirahisi.
Tatizo unazungumzia nadharia na siyo uhalisia.

Muuzaji wa samaki akiwa na samaki wake, hawi na uhakika samaki wake atanunuliwa siku hiyo au keshokutwa, au hata baada ya siku kadhaa. Hivyo anamwekea dawa, au kumtunza kwenye barafu ili asiharibike, na ili asipate hasara.

Siyo kweli kuwa samaki wote wanapovuliwa, hununuliwa siku hiyo hiyo. Kuna mtu ninayemfahamu, ambaye alikuwa anafanya biashara ya kununua samaki toka kwa wavuvi na kupeleka kiwandani, kuna wakati alikuwa akikaa na samaki hata wiki zima, kabla ya samaki wake kununuliwa na kiwanda. Na hiyo ilikuwa inatokea pale ambapo wamepatikana samaki wengi maeneo mbalimbali.

Tusiwe wabishi. Yawezekana siyo maji ya maiti au dawa za kutunzia maiti, lakini kuna mbinu mbalimbali zinazotumika kuwafanya samaki wasiharibike kabla ya kumfikia mlaji, na nyingine siyo salama kabisa kiafya.
 
Back
Top Bottom