Inaaminika kuwa ugonjwa wa mabusha husababishwa na unywaji wa maji ya madafu. Madai haya hupata mashiko makubwa zaidi kwa kuwa tatizo hili huwapata wanaume wengi wanaoishi Mwambao wa Pwani ya Bahari ya Hindi, ambako madafu hupatikana kwa wingi.
Madai haya yana ukweli kiasi gani?
Madai haya yana ukweli kiasi gani?
- Tunachokijua
- Maji ya madafu hayasababishi kutokea kwa mabusha (Hydrocele) kama ambavyo jamii za watu wengi huamini.
Kwa hapa kwetu Tanzania, kung'atwa na mbu anayeeneza vimelea vya minyoo wa filaria kunaelezwa kuwa sababu kuu mojawapo inayopelekea kuwepo kwa tatizo la mabusha hususani maeneo ya Pwani na mwambao wa bahari ya hindi.
Pia, JamiiForums inatambua sababu zingine zinazoweza kusababisha kutokea kwa tatizo hili ambazo ni-
- Uwepo wa kitendo chochote kinachochochea tando zinazozunguka korodani kuzalisha maji kwa wingi kuliko kawaida
- Kupungua kwa ufyonzaji wa maji yanayozunguka korodani kwa sababu ya kuziba kwa mirija ya lymph (blockage of scrotal lymphatic system) au kuziba kwa mishipa ya damu inayosafirisha damu kutoka kwenye pumbu kwenda sehemu nyingine za mwili (blockage of scrotal venous system)
- Uwepo wa mapungufu kwenye ufyonzwaji wa maji ya mfuko wa korodani wakati wa ujauzito, pindi mtoto awapo tumboni
Maji haya huwa na faida za kupunguza stress kutokana na uwepo mwingi wa Amino acids arginine, hutuliza kisukari, husaidia kurejesha kiwango sahihi cha maji na chumvi kinachopotea kwa watu wanaofanya mazoezi pia huwa na kiasi kikubwa cha madini na virutubisho muhimu kwa mwili.
Tahadhari
Pamoja na faida hizi, watu wenye changamoto ya FIGO hawashauriwi kutumia maji haya kwa kuwa kwa kuwa huwa na kiasi kikubwa cha madini ya Potassium yanayoweza kumfanya apate hatari ya kuongezeka kwa chumvi hizi (Hyperkalemia), na hatimaye kuhatarisha maisha yake.