SI KWELI Maji ya madafu yanasababisha ugonjwa wa Mabusha

SI KWELI Maji ya madafu yanasababisha ugonjwa wa Mabusha

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Inaaminika kuwa ugonjwa wa mabusha husababishwa na unywaji wa maji ya madafu. Madai haya hupata mashiko makubwa zaidi kwa kuwa tatizo hili huwapata wanaume wengi wanaoishi Mwambao wa Pwani ya Bahari ya Hindi, ambako madafu hupatikana kwa wingi.

EB7027ED-C4AB-48F2-B575-DF672279656C.jpeg

Madai haya yana ukweli kiasi gani?
 
Tunachokijua
Maji ya madafu hayasababishi kutokea kwa mabusha (Hydrocele) kama ambavyo jamii za watu wengi huamini.

Kwa hapa kwetu Tanzania, kung'atwa na mbu anayeeneza vimelea vya minyoo wa filaria kunaelezwa kuwa sababu kuu mojawapo inayopelekea kuwepo kwa tatizo la mabusha hususani maeneo ya Pwani na mwambao wa bahari ya hindi.

Pia, JamiiForums inatambua sababu zingine zinazoweza kusababisha kutokea kwa tatizo hili ambazo ni-
  1. Uwepo wa kitendo chochote kinachochochea tando zinazozunguka korodani kuzalisha maji kwa wingi kuliko kawaida
  2. Kupungua kwa ufyonzaji wa maji yanayozunguka korodani kwa sababu ya kuziba kwa mirija ya lymph (blockage of scrotal lymphatic system) au kuziba kwa mishipa ya damu inayosafirisha damu kutoka kwenye pumbu kwenda sehemu nyingine za mwili (blockage of scrotal venous system)
  3. Uwepo wa mapungufu kwenye ufyonzwaji wa maji ya mfuko wa korodani wakati wa ujauzito, pindi mtoto awapo tumboni
Kwa maana hiyo, maji ya madafu hayana uhusiano wowote na kutokea kwa busha

Maji haya huwa na faida za kupunguza stress kutokana na uwepo mwingi wa Amino acids arginine, hutuliza kisukari, husaidia kurejesha kiwango sahihi cha maji na chumvi kinachopotea kwa watu wanaofanya mazoezi pia huwa na kiasi kikubwa cha madini na virutubisho muhimu kwa mwili.

Tahadhari
Pamoja na faida hizi, watu wenye changamoto ya FIGO hawashauriwi kutumia maji haya kwa kuwa kwa kuwa huwa na kiasi kikubwa cha madini ya Potassium yanayoweza kumfanya apate hatari ya kuongezeka kwa chumvi hizi (Hyperkalemia), na hatimaye kuhatarisha maisha yake.
Loh mkuu!

Busha ni moja ya dalili za filariasis( matende). Ugonjwa unaosababishwa na minyoo iitwayo filaria ambayo huenezwa na mbu jamii ya Culex.

Watu wa maeneo ya pwani wanaathirika zaidi na huu ugonjwa kwa sababu hawa mbu wanapatikana kwenye huo ukanda.
 
Aina hiyo ya mbu culex huzaliana kwa wingi sehemu zenye vifuu vya nazi au madafu, kama tunavyojua vifuu vya nazi au madafu hutunza maji yaliyotuama kwa muda mrefu hivyo ni sehemu rahisi na salama kwa mbu kuzaliana kwa wingi.
 
Wakuu katika misele ya hapa na pale huku mtaani nimekutana na mjadala, je ni kweli matumizi ya madafu yanaweza kuwa chanzo cha ngiri maji au mabusha?
dsc02489.jpg
 
Back
Top Bottom