Sio sababu ya kufanya kama hao ambao hawawezi kamwe kujitikeza na kujitaja mana wanajua kuwa walilolitenda sio jambo jema.
Hatutaki mtu au Chama kitakachozidisha au kujenga mpasuko zaidi badala ya kutuleta pamoja kama Taifa.
Mungu anapompa mtu ukuu na utawala juu ya watu ana makusudi ya kuleta mabadiliko katika nyakati.
Kama tutaiondoa CCM halafu tuleta Chama chenye watendaji wenye hulka ile ile basi tutakua tumeruka mkojo tukakanyaga mavi.
Utofauti wa Mh .Magufuli na mtangulizi wake ndicho kilichoifufua CCM.
No matter kama anafanya vizuri au laa.
Chadema ikiingia ikaiga mbinu hizi hizi za CCM basi itatawala awamu moja tuu.