Majibu kwa Nape, Ridhiwan Kikwete na wengine kuhusu elimu yangu na niliposoma

Binafsi ningependa Nape na riz1 watuwekee cv zao za elimu hapa, maana tutaona walivyobebwa waziwazi na wazazi wao au mafisadi.
 
Composed, poised, and polished!

Dogo wa Kikwete na Nape sidhani kama wanaweza kuandika kama alivyoandika Mnyika hapa!

The boy has just destroyed those two little boys... Nape and Ridhwani, wameshindwa kutumia nafasi za wazazi wao kujiendeleza kielimu na maarifa wameishia kuwa mediocre kwenye kila angle
 
Kweli tunaacha kujadali kuanguka kwa matokeo ya kidato cha nne nusu wana zero tunajadili elimu ya mnyika JJ ambaye ni mp? Tuwazungumzie wataalamu na wasomi hawa tunasaidiaje kundi kubwa kama hili kwamba je sababu ni mgomo baridi wa walimu baada ya kupuuzwa kwa mdai yao ndio kumepelekea matokeo haya? Nape na rizone hebu badilikeni basi tuache siasa za kuzinguana mtaani kunazidi kuwa noma tutazidi kupigana kabari bure.

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Je elimu ya JK na jinsi nchi inavyoendeshwa sasa inadhihirisha upeo wake wa kufikiria? Nafikiri tusiangalie haya mambo kwa macho yaliyovaa miavuli ya vyama vya siasa bali tujaribu kuwa objective kidogo!!
 
Kumbe Mnyika ni mhitimu wa kidato cha sita na si mhitimu wa chuo sikulielewa hili kumekua na upotoshaji wa muda mrefu ni bora umeliweka sawa.
 
sometimes kuacha hoja kama hizi kweny JF kunanifanya nijilulize, nini lengo la mod wa zamu kuiacha?? je anapenda diversion za kijinga ili watu waacha kujadili main agenda??

ni upeo mdogo wa uelewa wa msimamizi au nini

This should have been deleted right away
 
Wakuu Elimu ya Lukuvi umekaaje.
Mulugo Je.
Mnyika ni Zaid ya Mbunge.
Hii ni Hazina Kuu..
Mungu mbarik Mnyika
 
Please Ben, channel you intelligence and energy on more productive issues as you normally do best.

Forget these (two) spoilt brats. They only know two things in life i.e. 1) hedonizing and 2) maliwato.
 
Mkuu, kazi ya mbunge ni nini?

Vigezo vya kupima mbunge mzuri ni vipi?

Tuambie mbunge anayeng'ara katika bunge letu kwa vigezo vyako.

Mbunge mzuri ni yule anayeweza kutimiza ahadi alizotoa kwa wananchi wake.

Mbunge anayeng´ara anajulikana kwa kutembelea jimbo lake na kuona jinsi alivyozigeuza kero za wananchi kuwa historia.

Kama kuongea sana hata JOTI anaweza, tena Joti mahiri kweli katika kujielezea.
 
Kumbe Mnyika ni mhitimu wa kidato cha sita na si mhitimu wa chuo sikulielewa hili kumekua na upotoshaji wa muda mrefu ni bora umeliweka sawa.
 
Wewe mwanzisha mada ulipata A ngapi form IV!?

Bill gates, kwenye moja kati ya documentaries zake nilizowahi kuziona anadai kuwa aliondoka harvard law school kabla hajamaliza digrii ili apate muda mwingi wa kufanya mambo ya msingi ikiwemo kutengeneza program za komputa..pengine hii stori itamfundisha kitu mleta mada..ukizingatia kuna maprofesa wengi sana masikini nchi hii.
 
Kazi zipi ni kazi za mbunge?
 

Kwa hiyo Mnyika aliacha shule kukimbilia siasa? Si utakuwa ujuha!
 
Mkuu John Mnyika,

Hongera kwa ufafanuzi MZURI,

Kuna baadhi ya mambo yanayoshangaza

1. Bunge letu lina wabunge ZAIDI YA NUSU, wenye elimu ya mashaka( msingi na wachache sekondari na "kozi" fulani!), wengi wao wakiwa ni wa Chama Cha Mapinduzi, CCM.Hawa wajasemwa/kuulizwa/kuonwa ni wa ajabu na Katibu Mwenezi wa Chama chao.

2. Hoja ya elimu bila kuweka elimu ya mlalamikaji yaani @Nape Nnauye haina hantiki!

3. Mara kadhaa watu wamekuwa wakileta habari zisizo na msingi/uongo/uzushi...(SI Tetesi) na hawa wamekuwa wakiadhibiwa...Ingekuwa vyema utaratibu huo uendelee, yaani bila vithibitisho watu kama hawa wawe banned kuondoa upuuzi na kupunguza heshima ya JF.

4. Iwapo tutaendelea kujibizana na Nape Nnauye, ni upotezaji wa muda na kutafuta malumbano yasiyo na msingi, hapa anaweza kuja kusema "mlini-quote vibaya"!

Pili, Kwa elimu yao Nape Nnauye na Ridhiwan wangetueleza wamefanyia nini TAIFA na siyo CCM. Yaani, hivi Taifa linaweza kuwakumbuka kwa jambo/mambo yapi?

Again, Hongera Mh. John Mnyika, it was narrative, long but not tiring!And have to say it was good creativity to write in this way than in CV format as others have wished!
 
Last edited by a moderator:

Nadhani una chuki binafsi..Hakuna ambaye hajui kuwa mnyika =wabunge 50 wa chama kile kikubwa...
 

Mheshimiwa Mnyika, we ni rafiki yangu, tumesoma wote Tambaza. kama rafiki ninapenda uwe na mafanikio zaidi ya haya, lakini pia kusema ukweli ni muhimu bila kuingiza siasa, ukweli ni kuwa hukuwa umechaguliwa kujiunga form five kwenda shule yoyote ya serikali, na hii inatokana na makosa, yaliyofnywa na Maua Seminary wenyewe kwa kutokupeleka, form zako wizarani... hivyo Tambaza uliingia kama second selection, maana ulichelewa kureport pia, hiyo pia iliwakuta mabinti kadhaa kutoka kwa shule hizo, kama kifungilo na nyingine. Ukweli unabaki kuwa mazingira ya Tambaza sio mazuri kwa mtu aliyezoea kutafuniwa kama huko Maua, kuweza kupenya kiurahisi, ndo maana wengi wa waliotoka shule kama hizo za kifungilo, seminary waliambulia div 4 au three, wachache sana walipata two, sina uhakika kama mnyika alipata div II, kama ulivyoeleza, hata hivyo nakuamini kuwa huenda ulipata marks hizo, though i knew kuwa ulipata division three.
Ukweli mwingine ni kuwa ilikuwa shida sana kwa mwanaume kwa wakati ule mwenye div III, au hata two ya mwisho kuwa admitted mlimani kwa government sponsorship maana criteria ilikuwa Ni a minimum of C na D, yaani at least points 5.5 kwa maana G.S ni points 0.5, hivyo nina Imani kuwa Mnyika hakuwa anaqualify kujiunga UDSM, halafu pia course ambazo walikuwa wakichukua watu wenye marks za chini mainly walikuwa FASS (PSPA na Socilogy), hivyo basi ukawa umepata wadhamini ambao, kama sikosei yalikuwa mashirika ya kidini, na katika course hiyo ya jioni ya BBA ulikuwa na Marafiki wengine wawili kutoka Tambaza, na ulikuwa ukiishi Mabibo.
Hata hivyo katika harakati za wewe kujiunga na kuendelea na masuala yako ya chuo bado ulikuwa Mwana CCM, hadi baada ya Muda ulipojiunga CHADEMA, na hatimaye kugombea Ubunge.
Ni ukweli usiopingika kuwa uamuzi wako wa kutokuendela na masomo ulikuwa zaidi juu ya masuala ya kisiasa na si kwasababu ya mizengwe, maana kuna watu wengi ambao walishawahi kufukuzwa vyuo na wengine kudisco kabisa lakini sasa wana PhD.
Ombi langu kwa wanasiasa si kila jambo linahitaji kuendeshwa kisiasa, tujipe Muda tujadili maendeleo ya Taifa, Maana kama leo tutasema tunaacha kusoma kwa ajili ya siasa kesho watoto wetu watasema wanaacha kusoma kwasababu wanataka kucheza soka, mwingine kuwa mwimbaji, na kwasababu hana Muda kwasababu soko litamtupa mkono then hataki hata kusomea huo Muziki ambao ndo anaona unalipa. Kwasababu kwa ulimwengu wa Leo it is not only about Experience but also, Qualification matter. Kama kuna tatizo kwa Accredited institutions kutoa competency based education and training hilo ni tatizo jingine lakini halitoi umuhimu wa QUALIFICATIONS. I stand to be corrected. No personal conflicts
 
Duh! Mnyika bwana! Yaani wenzio tunaangaika labda siku moja tutaweza kuja kuongea hoja kimpangilio kama ufanyavyo wewe kumbe unataka kutupasua msamba tu! Duh, kumbe ni Mi-"A" uliyojaza ndiyo inayokupa uwezo huo! Kweli wewe ni Nouma!
 
kweli kuna watu tulichagua wabunge smart,
kama unatumiaga captain morgan niambie nikufanyie mpango
 
Afadhali. Lakini Mkuu John Mnyika,napmba niulize maswali madogo mawili ya uelewa:

Kwanza,ufaulu wako kidato cha sita ulikuwaje pale Tambaza?

Pili, uliahirisha masomo yako UDSM;lini utamalizia?
Asante.
mbona ameshajibu kwenye post yake? Amesema form 6 alipata division 2, na masomo atamalizia pale CCM itakapotoka madarakani!
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…