John Mnyika
Mh. Mbunge swali uliloulizwa na Nape jibu lake ni dogo sana; sidhani kama ulikuwa unahitaji kurasa nzima kulijibu; jibu lake lingekuwa hivi "elimu yangu ni kidato cha sita nilijiunga Mlimani kusomea BBA sikubahatika kumaliza"; nina uhakika hapo ungeeleweka zaidi; na inasikitisha sana kuona kijana kama wewe unajinyima haki yako ya kusoma kwa kigezo cha kuitumikia siasa na hili dai lako la kudai eti utarudi kusoma siku CCM ikitoka madarakani ni wazi umeamua kutokusoma kwa makusudi CCM haiondoki madarakani leo wala kesho; pamoja na kwamba unadai elimu haihusiani na kazi zako ni wazi umeamua kutupotosha kwa makusudi; elimu ya darasani ina umuhimu wake tena mkubwa sana; usiwadanganye vijana wa jimbo lako wakaacha kusoma kwa kutumia vigezo ambavyo havina msingi; ushauri wa bure wakati unaendelea na majukumu yako kama mbunge endelea na masomo; utaona ni jinsi inakusaidia kujenga hoja zako kisiasa.
Chama
Gongo la mboto DSM
Mkuu chama hakuna haja ya kusoma mavitu mengi wakati huyatumii hatutaki Mnyika aende tena darasani kwani Elimu aliyo nayo inawazidi hata maprofessor wezi wa CCM mimi namfananisha Mnyika na Steven JobHakuna hoja yoyote iliyojengwa na John Mnyika alichofanya ni kutafuta sympath; inashangaza sana mbona vijana wenzake kina Tundu Lissu; Zitto wamemaliza vyuo na wanaendelea na mapambano kama wanavyodai; hata mtu wangu wa deals Lema amemaliza elimu yake; sasa sielewi anachokiongea John Mnyika hata hao akina Mugabe pamoja na kuwa walikuwa wanapigana vita vya msituni kutafuta uhuru Southern Rhodesia bado walijizatiti kwenye elimu pamoja na walikuwa kwenye mazingira magumu bado walisoma na kuhitimu; ni vyema sana kama mh. John Mnyika angekuja na jibu honest; sio tu kwetu hata kwake yeye mwenyewe.
Chama
Gongo la mboto DSM
CC Ritz, Precise pangolin
Nape elimu ya madarasa wapi.Naye Nape atuambie form fourr aliapta division ngapi.Maaana elimu ipo kwenye kidato cha nne huku juu form six au vyuoni hamna kitu. Maana mtu ukimaliza form four ukafaulu vizuri ukienda vyuo vya wenzetu ambavyo vipo kibiashara zaidi na haviangalii ubora wa elimu unaweza kurudi na PHDUkweli siku zote unamuweka mtu HURU. Asante sana Mnyika. Haya sasa njoo nape utueleze kati ya Mnyika na wewe nani ana akili zaidi. Mimi naona Mnyika kaelimika ila Nape unaweza kuwa na elimu ya madarasa
afterall nchi hii kwa muda mrefu imekuwa ikujengwa na wasiosoma na kubomolewa na wasomi!
Mkuu chama hakuna haja ya kusoma mavitu mengi wakati huyatumii hatutaki Mnyika aende tena darasani kwani Elimu aliyo nayo inawazidi hata maprofessor wezi wa CCM mimi namfananisha Mnyika na Steven Job
Ni kweli mkuu akina Nepi wana uwezo mdogo sana wa kufikiri!! Ni wahusika wa Didas MASABURI alivyosema!? Hawana hata uwezo wa kujieleza kama alivyofanya Kamanda Mnyika hapa!!!!!!Kujibizana na Nape ni kupoteza muda,kwanini ashihoji elimu ya pr.maji marefu au De sanga? Hii yote inaonyesha jinsi baadhi ya viongozi wa ccm walivyo kosa hoja!
Kujibizana na Nape ni kupoteza muda,kwanini ashihoji elimu ya pr.maji marefu au De sanga? Hii yote inaonyesha jinsi baadhi ya viongozi wa ccm walivyo kosa hoja!
kweli kama ndiyo tunatofautiana katika kuelewa kiasi hiki basi nchi hii tutakuwa maskini mpaka mwisho.