Majibu kwa Nape, Ridhiwan Kikwete na wengine kuhusu elimu yangu na niliposoma

Ndugu yangu Mnyika kaza buti endelea na harakati zako za kuwakomboa Wanyonge hadi kieleweke. juhudi zako unazozifanya bungeni tunaziona, na manyanyaso unayoyapata tunayaona. tunakupa pole sana. achana na hao akina Ridhwani kwani yeye ni msanii kama baba yake. pia Nape hana lolote. badala ya kuzijibu hoja na kutekeleza yale aliyowahidi Wananchi anakazana kulumbana na CHADEMA. Kwa vile viongozi wote wa CCM wameshindwa kazi na hawajui la kufanya ndo maana wanaparamia hata majabali. Achana nao.
 
kwa kweli mheshimiwa mnyika wewe ni kichwa , haupaswi hata kuendelea na shule kwani ni vema wakutunuku tu Doctrate kwani uwezo wako ni mkubwa muno; hao wanaoongea hvyo ni kwa sababu tu wanajiuliza mbona uwezo wako mkubwa sana ukizngatia ni bado kijana mdogo sana, achana nao watajibeba 2015 sisi tumewachoka hasa huyu jamaa anae itwa nape jamani mwenzenu personally simpendii kupindukia.

waulize hao wenye ma phd wamefanya nini wambie elimu cyo cheti ni uwezo kichwani, mbona waliowengi hatareport zao wanatengenezewa tuu? angalia mfano kawambwa ni Doctrate lakini mutathimin amefanya nn kpndi chote hki zaid ya kupotezea malengo wanafunzi wetu tu, jamani ccm hatuwapendi muelelewe hilo tumewachoka jamaniiiiiiiiiiiii

mwisho; mnyika wewe ni kichwa na utazd kuwa kichwa zaidi ya hapo. be blased na mungu akuongoze. Amina
 
You got good head John, uwezo wako katika kujenga hoja na kutetea wananchi wa Ubungo na Taifa kwa ujumla ni wa zaidi ya mwanasiasa, baadhi yetu hatukuwa na wasiwasi na elimu yako, bali tulikuwa na uhakika wa hoja zako 'cause we knew you since high school and we' re still appreciate ur efforts. Taifa hili linahitaji vijana wenye mitazamo chanya ya kimaendeleo kama unayoionyesha.
 
[h=5]Nimeitoa FB Myika njoo, najua wewe high class huendagi FB nimekuletea huku, nawe weka chako tumkome nyani usoni.....(mood tafadhali sana usiunganishe thread hii, pls pls)[/h]


Like · · Follow Post · 3 hours ago via BlackBerry





 
nimekusoma mkuu! we ni jembe la kizazi hiki hata hao wanaolopoka upuuzi wanalifahamu hilo. endelea kuwabuluza hao vilaza wa li chama la kijani.
 

Vyeti vya mzumbe bwana mbona viongozi wote wachakachuzi wa elimu ni wanakimbilia kusema wamesoma Mzumbe refer Kamala,Nchimbi,Mama Makinda,na huyu Nape Elimu zao hazilingani na uwezo wao wanauwezo mdogo mno wa kujenga hoja,na wasiwasi na elimu hizo.
 
Nimeitoa FB Myika njoo, najua wewe high class huendagi FB nimekuletea huku, nawe weka chako tumkome nyani usoni.....(mood tafadhali sana usiunganishe thread hii, pls pls)



Like · · Follow Post · 3 hours ago via BlackBerry


John Mnyika alipita masomo ya jioni hakumaliza hana cheti!!!!!!
 
Last edited by a moderator:

Kama kumaliza kidato cha sita ni kusoma sawa ila huyo mbunge wenu mtamkweza lakini ukweli ndio huo hana cheti; kweli upate A tisa O level ushindwe kusema kutoa matokeo yako ya kidato cha 6 zaidi ya kusema kapata div 2; na aweke tuone kama div 2 hakupata kutokana na B ya Bible knowledge; huyo mtuuuupuuuu kashindwa kusoma hata BBA tena masomo ya jioni msitake kututia kichefuchefu!
 
nikusaidie kidogo, Mh. mbunge hataki majibizano yasiyo na msingi hivyo kaamua kuwaeka kila kitu ili msiendelee kuuliza maswali, atakae uliza tena hapo basi huyo ni mbulula.

Hana cha kujibizana hana cheti hakumaliza chuo tena masomo ya jioni; lol!!!
 

Hapa hatuzungumzii ya bungeni tunajadili mtu aliyepata A Olevel lakini anaficha majibu yake kidato cha 6; hivi div2 ya kidato iliyotokana na Bible knowledge unaweza kujigamba nayo?
 
Kwa walio wahi kupita shule (sekodari) wanaelewa inahitaji uwezo wa juu kiasi gani kupata A 9. Hii ni zaidi ya kipaji maalumu. Nachelea kusema mheshimiwa Mnyika ndiye Mbunge Pekee katika bunge la sasa aliyefaulu sekoari kuliko wote

A tisa za kusaka mitaani? Watu wanaopata A O level kidato sita wanapiga A za kumwaga hebu tusaidieni hiyo div 2 aliyopata form 6 iwekeni matokeo yake tuone kama haitakuwa kichekesho
 

Aliye kwambia kusoma ni kuelimika ni nani wangapi wamesoma lakini hawana uwezo wa kupambanua mambo mfano huyo Nape mwenye elimu ya kuungaunga na asinge kuwa mtoto wa kiongozi kama mnyika hata hapo asinge fika mkuu.
 
Kwanza nianze kwa kuwashukuru Wakili Ridhiwan na Mh. Nape kwa kuibua hoja kuhusu Elimu ya Mh. Mbunge Mnyika kitu ambacho binafsi nilikuwa sikui na nilikuwa najiuliza sana Hivi Mnyika anaelimu gani hasa nikizingatia uwezo wake wa kuhoji( Reasoning capacity) Kitu ambacho naamini kwa watu ambao kweli wanamfahamu au kumuona tu bungeni inatosha kukubaliana nami kuwa Mh. Mnyika ni zaidi ya mbunge wa Ubungo kwani anawakilisha kwa maana halisi, na wala huhitaji kuhoji zaidi kuhusu elimu yake.

Pili, nirudi kwenu wakili Ridhiwan na Mh. Nape hivi kweli nanyi ni watanzania na wazalendo wakweli au mamluki? Badala ya kuhoji kuhusu elimu na uwezo wa wabunge na mawaziri ambao wapowapo tu kama hawapo kwani katika wizara zao maendeleo yamepigwa sindano za ganzi mf. Wizara ya Elimu kufelisha zaidi ya theluthi mbili yaani div. IV na 0 huyu ndio tujiulize alikuwa akifanyanini na vyeti alivyonavyo anaweza kuvitafsiri kuwa matendo? Kwani Matokeo ya mwaka jana yalitosha kumfanya afanye kitu ambacho kingefanya matokeo ya mwaka huu yasiwe hivi yalivyo. Lakini kwakuwa wengi wao huishia kusinzia tu wawapo ofisini, semina za msingi kabisa na bungeni, haya ndio matokeo yake.


Tatu, jiulizeni hata nahodha mwenyewe, vipi G.P.A yake, reasonable decision making etc? Kama rubani unapoona mambo yanaenda mrama, au unabaharia asiejua kuogelea vizuri mweche ajifunze kuogelea kwanza ndipo uambatane nae. Vipi majibu rahisi kiasi hiki kwa maswali magumu? Mfn waziri anasema sababu kubwa za kufeli kwa wanafunzi ni Kwanza uhaba wa walimu, pili ukosefu wa maabara na maktaba n.k. Kitu ambacho sikweli mfano Kuna shule zina kila kitu kinachotakiwa Mfano Korogwe girls ina maktaba nzuri, maabara, walimu wakutosha na idadi ndogo ya wanafunzi lakini bado wana div I-0, div II- 5, div III- 4, div IV-19 na fld 25 kwa darasa lenye wanafunzi 54 hapa napo kuna upungufu huo aliousema Mh. waziri Kawambwa? Anasahau kuwa alichagua wanafunzi ambao aliwaongezea alama kubwa tu katika ufaulu wao kujiunga kidato cha kwanza na wengi wao hawajui hata kuandika majina yao.
Lakini pia mtihani wao ni wa kuchagua jibu hata hesabu washafanyiwa wao wanachagua jibu sahihi tu.

Nne, nami pia sasa najiuliza kwanini Elimu ya Tanzania isiingie kwenye maajabu ya dunia? Mwanafunzi anaefeli anaongezewa alama iliafaulu, mathalani mwanafunzi asiejua kuandika hata jina lake anafaulu mfn. darasa la saba na kadato cha pili.

Mwisho, Najiuliza hivi ni usomi wa namna gani huu ambao hadi msomi mwenye Phd kama Mh. Kawambwa hajui umuhimu na heshima ya kujiudhuru?
Niseme tu katika nchi yetu kuna vitu vingi vyenye maslahi kwa taifa vinavyotakiwa kuhojiwa nikianza na uzalendo na utendaji wa baadhi ya viongozi wetu na vitu wanavyovifanya, mauaji yanayoongezeka hasa yanayohusisha imani, Na kubwa kabisa ni ufisadi usiomithilika likini bado nahodha anawachekea tofauti na enzi za mwl. Nyerere. Hojini hivi basi kwakuwa nyinyi mpokaribu kabisa na wahusika.
 
nape na riz one shame on you mmejidhalilisha sana kwa kuparamia mwamba!
 
Mzumbe University ni kama Pombe ya Ngomani yeyote anaweza kwenda pale akajiregister, akaendelea na shughuli zake then baada ya miaka miwili anarudi kuvaa joho.
 
hongera kamanda mnyika kwa kuondoa wingu hili naamini watanzania wanatambua uwezo wako katika kusimamia mambo ya msingi na hili ni muhimu zaidi katika kipindi hiki cha harakati za kulikomboa taifa hili pia uwezo wako darasani ni elimu tosha kwa wengine wote waiokuja na hoja mfu ya elimu yako hongera sana kamanda tupo nawe hadi kieleweke.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…