Majibu kwa Nape, Ridhiwan Kikwete na wengine kuhusu elimu yangu na niliposoma


AshaDii uko sahihi kabisa lengo kubwa la Nape ni kutumia ujinga wake alionao ili kuwafanya
watanzania kujadili mambo yasiyo na tija kwa Taifa na kujadili watu,na kuacha mambo ya msingi
na ya manufaa kwa Taifa"


 
cha msingi nini unawafanyia wananchi kama huna unachowafanyia wananchi huna maana
Kama shule yako iwe ndogo au kubwa lakini ukaleta manufaa kwa wananchi basi wewe ni mtu utakayethaminiwa na wananchi au jamii au taifa husika
 

Maelezo yangu yalilenga jinsi CV ambavyo inatumika globally. Nikiwa mkweli kwenye hii discussion ya CV nitakuwa judgemental kitu nilikuwa nakikwepa. Lakini basi tuendelee.

1. Wanzilishi wa mjadala wa CV ni CCM(Nape) kwa lengo la kumdiscredit Mnyika. Ndiyo maana nao imelazimika CV??? zijadiliwe. Kwa nini CCM walileta mjadala huo ni kwa sababu viashiria vyao vya utendaji katika siasa za maji taka ni CV. Ndiyo maana kuna watu ndani ya CCM wana Phd ilihali hawana elimu hiyo. Kwa Mnyika ilikusudiwa kutoa picha ya mtu aliyedanganya elimu yake kwa hiyo alipata ubunge kwa udanganyifu na sisi humu JF tushadidie bila kupewa vigezo na visharia vya kumpima na kumhukumu Mnyika. Hizo ndizo siasa za maji taka. Yalimpata Salum A. Salum kuwa si Mtanzania, Bashe, Ulimwengu orodha ni ndefu.

Kwa hiyo kwa CCM ni majadiliano valid

2. Sisi tunaojadili ni wazi tunajadili kishabiki kupingana bila hoja na lengo. Hapa nasisitiza majadiliano haya ni muhimu kukabiliana upande mwingine; na ni afya kwa wanaJF kuwa "informed" na information siyo lazima iwe accurate, valid na achieving kwenye mazingira haya.

3. Tunawajadili CV zao pamoja na kuwa wako kwenye nafasi zao kwa sababu upande mmoja ulitaka kutujulisha kuwa Mnyika ni muongo kadanganya elimu hafai. Siyo kuwa hoja za Mnyika zina mapungufu gani.

Mimi ni muumini wa JF CV yangu ni ya M&E kwenye utendaji (performance). Cha kwanza naangalia malengo target/objective; mbinu/strategies, resources/rasilimali na matokeo kufikia malengo. Cha pili naangalia kitu kinaitwa crisis management uongozi na usimamizi wa mkanganyiko.

Kifupi CCM wana mikanganyiko mingi ambayo wanafanya kila njia kuisimamia/kumanage. Wana lengo la kuonyesha jitihada zao lakini kwa kuwapaka matope wengine. Wanazo resources kwa mikakati hiyo hata kama hawatathmini kabla matokeo yatakuwaje.

Mnyika naweza kusema kifupi anafanya anachokiamini kwa rasilimali aliyonayo kwa lengo la kwenda kinyume na yanayofanywa na CCM. Hapo kuna mgongano lazima hoja hata za CV ziletwe public.

Mimi naona ni healthy informed discussions; tunanufaika sana na hizi discussion tunaokuwa na access nazo. Wananchi wengi hawana access ya hizi discussion ingawa sisi tuna majukumu ya kuwashirikisha na kinachoendelea kwenye hizi discussions ili tuwa"equip" kufanya maamuzi kuhusu wanayoambiwa na wanayoshirikishwa. Kwa sababu wananchi hata kama hana elimu lakini ana uwezo (IQ) ya kupima hata kwa hisia.

Sina uhakika kama nimekuelewesha ila naamini discussion ya CV ya Mnyika kwangu mimi imenifundisha mengi yenye faida. Kwa mfano wote wameonyesha walivyojitahidi kukamata elimu hata kama ni bora elimu. Wote wameji"expose" na kulinganishwa kiutendaji. Na wote wamesimamia malengo yao kwenye taasisi zao.

Imenipa fursa adhimu kubaini mikakati mufilisi ya CCM kwa watu binafsi wacha Mnyika orodha ni ndefu. Kwa mtazamo tu nimeona kama mikakati hiyo imeimarisha sana upande uliotuhumiwa na watu binafsi walioshambuliwa. Ingawa lazima nikiri labda nao CCM wamepata return ya adventure yao.

Ukitaka tija katika suala hili itategemea mtu binafsi ana uelewa upi unaompa tools za uchambuzi zipi kwa lengo gani? Kwa hiyo hata wewe ukiona hazina tija potezea, mimi kwangu ni input muhimu ninayoipata bure juu ya wrong or rght strategies kuhusu Siasa za maji taka
 

No ndugu yangu ingawa simkubali Nape 100% na sitamkubali asilani, lakini mui muue haki yake mpe, elimu ya kuunga siyo lack of confidence ktk maisha, maana mtihani una mambo mengi, elimu haina mwisho so ukichomwa na mwiba lazima uungo'e ni mjinga pekee atakayeuacha ili umkumbushie machungu, so mtu akitetereka kwenye elimu asikate tamaa bali atafute jinsi ya kujiendeleza wengine wameanzia chini kabisa na leo ni maprofesa(siyo Maji Marefu) wa fani mbalimbali among other nice jobs.
 
Hapo naona kuna watu wenye historia inayofanana na nape u mnyika,hivyo nilazima watetee upande unaowahusu.
Ila mimi naona fundisho ni kuwa kama wazazi wako wana influence kwenye chama au serikalini mtoto wao atabebwa sana kielimu hadi afike mbali hata kama ni ZIRO BRAIN.kingine ni ukiingia kwenye siasa za upinzani ukawa mahiri ni rahisi kufanyiwa hujuma usifanikiwe KIELIMU,kibiashara au kikazi..
 
Naweza nikakubaliana na wewe katika mwanzo wa hoja yako na nikapingana na wewe kabisa katika mwisho wa hoja na ni kwa sababu..,msingi wa hoja yako ni mzuri lakini hitimisho lake ni baya. Nitakubaliana na wewe kuwa watoto wa watu wenye influence (sio tu kwenye chama au serikali lakini hata kwenye jamii-na hapo kwenye chama simaanishi CCM pekee bali chama chochote chenye jina popote) watoto wanakuwa na fursa pana zaidi katika kupata elimu, lakini na kuendelezwa hata pale wanaponasa na kushindwa mara kadhaa katika mitihani.

Lakini nakataa (kwa asilimia zote 100) kuwa mtu ambaye ni mahiri kwenye siasa za upinzani anafanyiwa hujuma ya KIELIMU na chama tawala ili kumdhibiti.,hilo halijawahi kutokea na wala msilihusishe suala la Mnyika na Mtazamo huo. Mnyika hakuondolewa chuo kwa sababu ya kushiriki katika Upinzani.,lakini kama hiyo haitoshi wapo viongozi ama wanachama wakereketwa wa Upinzani katika vyuo na sekondari zetu hata leo.,baadhi wakiwa ni walimu na baadhi wakiwa ni wakufunzi na watumishi katika taasisi hizo za Elimu lakini sijawahi kusikia kesi yeyote juu ya mtu kuondolewa Chuoni ama Shuleni kwa sababu ya kushabikia Upinzani. hilo linanifanya kupingana na hoja yako katika kipengele hiki cha mwisho.
 

dah, kweli mkubwa ametamka mchele
 

Tutofautishe kati ya kusoma na Kuelimika
Kuna watu wengi wamesoma iwe kwa kuunga unga kama Nape au kwa mikato waijuayo wenyewe na wakawa na Masters hata PHD lakini bado kabisa hawajaelimika.
Lakini kuna watu wengine ambao wanaweza kuwa wana madarasa ya chini hata darasa la saba lakini wamesoma na kuelimika
Watu geneous kama Mnyika ni moto mara moja wana akili inachemka hata kama hajapata Masters ni suhala la muda tu.
Mtu mwenye bongo inachemka utamwona tu hata anapojenga hoja au kusemea jambo fulani si mtu wa kubebwa na kuonewa haruma.
Nape kaungaunga na kuugaunga ndani yake kuna ujanja ujanja , shule ulifeli na unaiukia pahari na Masters akili umepata wapi ?
 
Kila nikipitia comments za hii thread bado naona mafunzo niliyodhani yatapatikana baada ya watu kutuliza akili na kufanya tathmini hayajapatikana.
 

mkuu hizi ndo maada ambazo zingesitahiki kujadiliwa hapa JF kama home of great thinkers. na sio yale mambo yenu ya udini na uchadema.
hizi zinajenga, na hata mtu anachangia unaona kabisa njia ya kufuata. lakini zile mada za ajabuajabu wakati mwengine mtu unaishia kukejeli na kutukana. this is real good.
kwenye mada; binafsi kuna watu ninaowafahamu walitaga kabisa lakini sasa hivi hawashikiki kielimu. vijana wasikate tamaa, hii ni changamoto iliyopo mbele yao wanachotakiwa sio kuikimbia bali kupambana nayo. mwisho wao ndo watakao ishinda hii changamoto. historia ina tuambia hovyo. penye nia pana njia.
 
Mojawapo wa watu wenye vipaji alikuwa ni Prof Mwandosya ambayo serikali ya Mwl ilimuangalia na kumuendeleza.
 
Jamani samaanini labda sijaelewa vizuri. Is there any Impact ya kujadili CV za mtu katika nchi maskini kama Tanzania?

Hapa cha kuangalia ni nani anafanya nini kwa ajili ya kuokoa Taifa letu na kwa mantiki hiyo Huyo mtoto wa kikwete nje ya box, kwasababu kwangu mimi mtoto wa kigogo luhanga hana faida yoyote tena hata akifa leo wala taarifa msinipe. Sio mnyika ambae akifa leo sisiemu waatatulipisha mpaka kodi ya kutembea barabarani

Acheni kumpa credit huyo mtu bwana hana manufaa kwa taifa wala faida yoyote kwa tanzania ijayo
 

Wengi wanashindwa kuelewa concern ya Mnyika and that is what pains me most..Mnyika anawakilisha kundi la watu wengi wenye uwezo kiakili lakini waliokwamishwa na mfumo kufikia malengo yao ya kielimu...Mnyika had at one time passed through very difficult moments katika maisha yake kwakuona watu ambao hawakuwa na uwezo lakini ambao hawana akili ya kuhoji wakiendelea kielimu bila vikwazo huku yeye kwakua bila kujua akili yake ya udadisi ndiyo iliyo mfanya kuingia katika matatizo na kushindwa kufikia malengo yake ya kielimu. Najaribu kuvaa viatu vya Mnyika kuona ni jinsi gani alivyo umizwa ki-psychology na mfumo husika usiokuwa na utambuzi kwa watu wenye malengo ambayo wameyaambatanisha na wakati huku wakiwa wenye vipaji vya ziada. Nafikiri baada ya kuona anakutana na vihunzi akaamua kushuka kwenye usafiri aliokuwa amepanda (University) ili awahi kufika kule alikopanga kufika (kubadili mifumo yenye vikwazo thru politics) akiwa bado na nguvu za kimwili na kiakili.....

Nilikutana na Mnyika one day and I asked him about his education I could easly read from his mind kuwa alikuwa anajambo moyoni mwake. Nami kwakumsoma haraka nikabadili topic lakini sasa naelewa kwanini ilikuwa vile....Amejibu maswali yangu mengi sana and I am so pained kuona kuwa Mnyika was forced to do what he did kwasababu ya mfumo mbovu. Jenerali Ulimwengu nakumbuka alishawahi tamka siku moja kuwa ni heri asingeenda shule maana ingesaidia kupunguza baadhi ya maumivu ya anayokumbana nayo kwakuona mambo yakifanywa yasivyotakikana na kwakua anaelewa ubaya wa mambo anapojaribu kuhoji anajikuta anaingia kwenye mapambano badala ya watu kuelewa makosa yao na kujirekebisha.....

Wengi wetu kwa namna moja ama nyingine tumeumizwa na system ya elimu ya Tanzania....
 
Kuna watu wanashindwa kuelewa kwamba: LEADERS ARE BORN NOT CREATED OR EDUCATED!!!
Unaweza ukasoma ukawa Professor,Doctor,Engineer,Lawyer n.k na bado usiweze kuongoza KIJIJI achilia mbali FAMILIA Yako ya mkeo na mtoto!

Zingatia hili:UONGOZI ni KIPAWA toka kwa Mungu. John Mnyika ni aina ya Viongozi wa aina hiyo. Hawahitaji kukaa darasani na kupata Digrii ndipo wawe Viongozi wa Watu!!!

Hebu chukulia mtu kama Doctor Emmanuel Nchimbi(Waziri wa Mambo ya Ndani-CCM) umlinganishe na Mbunge John Mnyika-CHADEMA kwa akili,hekima kujenga Hoja na Busara ndipo utajua kama Elimu inaweza kumsaidia mtu aliyezaliwa bila kipaji cha Uongozi!!!!
 

Kimsingi sioni kama suala hili lina ukweli wowote, siamini kama mfumo wetu wa Elimu unawanyima fursa wale ambao wanashiriki na kupigania siasa za kipinzani. Nimepitia mfumo huu wa Elimu na nimekuwa nikisoma pamoja na wale waliokuwa ni wafuasi wakubwa wa siasa za kipinzani na bado walimapewa fursa sawa na wengine, hakukuwa na hiki ambacho kinasemwa hapa.,na kwa bahati nzuri ni chuo hikohiko ambacho Mnyika amesoma.
 
Kuna maana gani ya kuwa na elimu ambayo haikusaidii kama Nape? Bora kuwa umeeleimika kama Mnyika na ukaamua na kufanya mambokama msomi kama Mnyika sasa sisi tunakazania tu elimu ya vitabu vya dadarsani hadi mnapeana udokta....kha
 
Sasa michango ya Mnyika na Nape ambaye amelazimisha shule unaionaje? Inafanana?
 
Basi vijana wa CCM jifunzeni kuomba doctrine vyuo kutumia TISS ili muzawadiwe sio kubaki na doctrine moja kama doctor slaa.
 

KaKa ninao ushahidi wa kutosha kuhusu kuhujumiwa kwa baadhi ya wahadhiri pale mlimani kisa siasa.kuna mwali
mu aliyewahi kuvuliwa promotion ya ukuu wa shule ya secondary kisa alishinda udiwani chadema,kunawafanyabiashara wanaokomomolewa kibiashara kwasababu ya kufadhili vyama .kuna watu wamefunguliwa kesi zisizo na kichwa kisa
siasa tu.hauko karibu na mambo ya ndani ya ccm ndio maana hUfahamu.kuna watu pia wametishiwa ishu ya uraia kuhusu siada.ninauhakika mnyika akirudi pale mlimani sasahivi atayahujumiwa tuu.ndio maana amewahi kusisitiza atajiendeleza baadae
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…