Majibu kwa Nape, Ridhiwan Kikwete na wengine kuhusu elimu yangu na niliposoma

Majibu kwa Nape, Ridhiwan Kikwete na wengine kuhusu elimu yangu na niliposoma

Mkuu it's true you don't dance songs played by other than your master, because you are a puppet on a string, dancing only to its master's tunes. Though now you claim you can see but I doubt if its beyond your nose. Your immature line of thinking is so much based on the PAPER MASKS behind which some of your comrades are hiding. The dubious ways in which those credentials were obtained, to you mean nothing. Imagine a person claiming to graduate his A level studies at Butimba or a graduate who is said to have been disqualified with his o level exams because he stole and was caught with examination papers or a graduate minister who doesn't remember that Tanzania is union of which two countries. Its ashame to see the offsprings of big shots, behind their paper masks being awarded positions in the government and your beloved party. Mheshimiwa Mnyika came in the open to declare that he did not complete his degree, clear and very honest. I say he is a man of integrity. Mkuu@ Chama I beg of you to put aside the cow dung mentality and give a praise when one deserves it. Last but not least in yr threads you have tended to show disrespect to our mothers and sisters, I don't believe that that is in line with your beloved party's policy.

I am master of my destiny! nobody own or control Chama; I always questions your IQ; are you here to defend Mnyika or to clarify his nonsense? The argument is did he graduate from UDSM? what do you want me to praise Mnyika for? All I have is advice! He should go back to school and finish his studies; I will praise him when he graduate; and let me be clear I am not here to speak for Nape Nnauye but I am not surprised with Nape Nnauye whatever he did was based on his determination and personal ego; I congratulate him for that! it was not an easy road but he made it! in my real life I have witnessed people who had division 0 and 4 in form 6 now they have masters degree; everything depend on choices; some people sit back and review what they did so it's very possible Nape Nnauye did the same thing that's why he has masters degree; you are wasting your time to question something you can't take it away from him; the only question I want to ask you what you have???? I know for sure you don't have a shit so the choice is yours; you either follow Nape Nnauye or Mnyika
 
Mlugo..!? Huyo ambaye hajui hata chimbuko la Tanzania?

Inanihuzunisha sana kuona una-define IQ kuwa ni = kumaliza chuo. Inaonyesha jinsi gani hujui maana ya IQ na hilo ndilo linalowapa shida watu wengi... Ok, unasema mkoa wa Dar unaongoza kwa kununua mitihani; then, with that, tu-disqualify basi kwa muda, kiwango cha elimu kama criteria ya kupima IQ na tuanze kusimamia factors zingine kama uelewa, speed ya kufikiri na kuchambua mambo, uwezo wa kuweka application ya facts katika really life..n.k.

Kuna watu wengi sana ambao wana IQ kubwa kuliko hata Professors and hawakufanikiwa kumaliza shule. Sasa unavyomuweka Mlugo na Mnyika kwenye meza moja na kusema Mlugo ni zaidi ya Mnyika..!! Unanipa shida kidogo... Labda wanajamvi wenzangu mnisaidie..

Labda kukusaidia kidogo maana ya IQ:

IQ - a measure of a person's intelligence as indicated by an intelligence test; the ratio of a person's mental age to their chronological age (multiplied by 100)

Kishuzi usichafue hali ya hewa hapa tunajadili madai ya Mnyika na kiwango chake cha elimu sasa kama unataka tuwafanyie malingano kati ya MINyka na Mlugo fungua thread tuyadili bila wasiwasi wowote!
 
Last edited by a moderator:
Ridhiwani na huyo shoga yako chama nyie wote ni wapuuzi....mh.jj mnyika hakusema amemaliza chuo....kusema amesoma chuo miaka 3 si kuwa amesena alimaliza.wewe ridhiwani na kumaliza kwako chuo lakini kichwani ni mweupe na mtupu kama baba yako.wewe na baba yako hata muunganishe akili zenu bado hamuwezi kuwa na akili kama mh.jj mnyika.nyie ndio wapuuzi #1 hapa Tanzania. ...wajinga kabisa.

Unajua kuna wakati kujibishana na mtu hayawani ni kazi sana sasa wewe kwa mtazamo wako hivi huyu Mnyika kama kweli angekuwa na akili nini kilimfanya apoteze miaka 3 na asihitimu? na ninavyojua mimi degree Tanzania inasomwa miaka 3 hata kama ingekuwa ni miaka 4 bado alikuwa amebakiza mwaka 1 mmoja tu ni nini hasa kilichomfanya aache kama sio upungufu wa akili? Nina uhakika pale UDSM hakupata nafasi ya kununua mitihani; yaani graph yake kielimu imeanguka mwambieni aseme ukweli nini kilimkimbiza UDSM!
 
Last edited by a moderator:
Huna lolote muongo mkubwa wewe. ..nani asiyejua kuwa wewe ni ridhiwani kikwete? Hata ulivyomjibu mh.j mnyika hapo juu ni jibu tosha kuwa wewe ni ridhiwani.na kugraduate kwako chuo kikuu na shoga yako mohamed jamalee yule mhindi mwenye maduka k'koo bado kichwani wewe ni mweupe pee kama karatasi..hata kuongea English huwezi kama baba yako kikwete. Heshima ni kuheshimiana..ukiheshimu wenzako na wewe utaheshimiwa.ukileta ujuwaji kisa mtoto wa rais ambaye hakushinda huo urais tunakupa ngumi za uso.muwacheni mh.jj mnyika maana hana maneno na mtu.yuko busy kuwatumikia wananchi!!!!
Duh! Nijuavyo ni kwamba dogo mnyika hajaoa,,, nashangaa kwa nini!!!!
Wewe ni miongoni mwa wanawake mnaofaa kuwa MKE WA MNYIKA.... Unampenda hadi mumeo uliyenaye anajua!!!!
Pole kwani nyie hamumjui mnyika. Ni mjinga tu huyo dogo na ni kibaraka wa MANGI MBOWE.
 
Ccm hoooiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii! Nape chinnniiiiiiiiiiiiiii, prince mtoto wa jk je? Kaficha sura
 
I am master of my destiny! nobody own or control Chama; I always questions your IQ; are you here to defend Mnyika or to clarify his nonsense? The argument is did he graduate from UDSM? what do you want me to praise Mnyika for? All I have is advice! He should go back to school and finish his studies; I will praise him when he graduate; and let me be clear I am not here to speak for Nape Nnauye but I am not surprised with Nape Nnauye whatever he did was based on his determination and personal ego; I congratulate him for that! it was not an easy road but he made it! in my real life I have witnessed people who had division 0 and 4 in form 6 now they have masters degree; everything depend on choices; some people sit back and review what they did so it's very possible Nape Nnauye did the same thing that's why he has masters degree; you are wasting your time to question something you can't take it away from him; the only question I want to ask you what you have???? I know for sure you don't have a shit so the choice is yours; you either follow Nape Nnauye or Mnyika


Mkuu it's your IQ that is most questionable. You claim thats you are not here to speak on behalf of anybody, but there you go, clarifying on their behalf, justifying their misdeeds and praising them. Surely a puppet on a string dancing to its master's tunes. I am not defending anyone, what I expressed was a statement of fact. Mheshimiwa Mnyika is a man of integrity, unlike your comrades who forged their way through. I am not sure if you are not of the same caliber. Mkuu it's not a wise Idea to blow your own trumpet, othewise you might be mistaken for a fool. Lastly with your immature line of thinking if you are a graduate, than my great grand father was Napoleon the Great!!!!!!!
 
Ccm hoooiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii! Nape chinnniiiiiiiiiiiiiii, prince mtoto wa jk je? Kaficha sura

Hahaha hahaha hahaha hahaha hahaha hahaha hahaha Hahaha hahaha hahaha hahaha hahaha hahaha hahaha hahaha hahaha hahaha hahaha
 
Nilikuwa katikati ya kazi jimboni nikaambiwa kwamba kuna mwito humu wa Nape na Ridhwan kutaka nieleze elimu yangu. WanaCCM walianza suala hili kwa ari, nguvu na kasi mpya niliposema kwamba nchi imefika hapa ilipo kwa sababu ya udhaifu wa Rais Kikwete, uzembe wa Bunge na upuuzi wa CCM.

Nikapuuza, naona sasa limeibuka tena kwa ari, nguvu na kasi zaidi baada ya yaliyojiri bungeni kuhusu hoja binafsi niliyowasilisha bungeni kuhusu maji na mkutano wa hadhara wa tarehe 10 Februari 2013 na masuala ambayo niliipa Serikali wiki mbili kuyatolea majibu ama sivyo nitaongoza maandamano ya wananchi kwenda Wizara ya Maji kutaka uwajibikaji na hatua za haraka.

Kwa mara nyingine tena zinafanyika jitihada za kuhamisha wananchi kwenye mjadala kwa kumshambulia mtoa hoja badala ya hoja, sasa ili turejee kwenye mijadala ya msingi ni muhimu niweke kumbukumbu sawa kuhusu masuala kadhaa kama yalivyoombwa.

Elimu yangu sio siri, nimegombea ubunge mara mbili mwaka 2005 na 2010 na mara zote nimeeleza kuhusu suala hili; Nape na Ridhwan wangetumia tu elimu yao wangetafuta kwenye mitandao na kukuta majibu wanayoyatafuta. Nieleze kwa muktasari tu; nimesoma shule ya msingi Mbuyuni Dar Es Salaam (nilikuwa mwanafunzi wa kwanza kwa mkoa wa Dar es Salaam).

Nilichaguliwa kwenda Shule ya Sekondari ya Ilboru wakati huo ikiwa ya vipaji maalum, sikwenda; wito ulinituma kwenda Seminarini. Nilisoma Franciscan Seminary Maua (FRASEMA) mpaka kidato cha nne; nilipata daraja la kwanza; nikiwa na alama A katika masomo tisa.

Ningeweza kwenda shule yoyote ya Serikali ya kidato cha tano na sita yenye mchepeo ambapo ningeutaka; lakini niliamua kubaki Dar es Salaam shule ya Tambaza kwa sababu nilitaka kusoma huku nikiendelea na harakati ambazo nilizianza kabla.

Hapa ndio ilikuwa chanzo cha mimi kuingia kwenye kazi ya kuhamasisha mabadiliko kwenye mimbari nje ya utumishi wa madhabahuni. Tukio lililobadili mwelekeo wa maisha yangu, mwaka 1998 nikiwa kidato cha nne; nimesoma na tumeanza mitihani tukatangaziwa kwamba mitahani yote imefutwa baada ya kuvujishwa.Tukarudishwa nyumbani kipindi hicho nikaenda kwenye mafungo kujitafakari kwenye mkoa mmoja nikarejea Dar es Salaam nikakutana na wanaharakati kadhaa wa asasi zisizo za kiserikali; maelezo kuhusu ufisadi yalinifanya nione nina wajibu kwa nchi yangu, nikarejea Seminarini kufanya mitihani nikiwa na fikra tofauti.

Matokeo yakatoka nimefanya vizuri, kwa mifumo yetu mibovu ya wakati huo kwa mara ya pili tena Serikali hii inayoongozwa na CCM haikutambua vipaji na nikapaswa niendelee kujilipia ada mwenyewe kama ilivyokuwa kwa ngazi nyingine za elimu zilizotangulia; hapa nikakata shauri kwamba nitatumia uwezo na uadilifu wote ambao Mwenyezi Mungu amenijalia kuwezesha mabadiliko katika taifa letu.

Nikaamua kuacha kwenda kwenye shule za bweni mikoani na kubaki Dar es salaam nisome Tambaza huku nikiendelea na kazi za harakati; wakati huo nikihamasisha masuala ya ukombozi wa vijana nchini. Pamoja na kusoma kutwa huku nikifanya kazi nilipata daraja la pili katika kidato cha sita.

Taasisi nilizoanzisha au nilizoongoza katika kipindi hicho na kazi nilizofanya sio siri na zinapaswa kujieleza zenyewe kwa matendo badala ya maneno. Katika kipindi hicho, wakati huo kukiwa hakuna Mfuko wa Elimu wala Bodi ya Mikopo nikashiriki katika ushawishi wa mabadiliko ya kimfumo; nilikwenda Dodoma, tukakutana na wabunge na mawaziri nikawasilisha mada “Towards a more functional education in Tanzania”, wakati huo nikiwa mwanafunzi wa Sekondari.

Kati ya wabunge waliosikiliza mada niliyoiwaisilisha wakati huo sasa ni Rais Jakaya Kikwete ( Ridhwan ukiwa nyumbani unaweza kumwuliza maoni yake aliyotoa siku hiyo kuhusu ugharamiaji wa elimu na suala la mauaji ya mwanafunzi wa Iyunga Michael Sikupya). Nilipotoka kwenye mkutano ule Dodoma mwishoni wa miaka ya tisini, nilikata shauri kwamba mwaka 2005 nitagombea Ubunge hii ni baada ya kushudia aina ya wabunge waliokuwepo.

Mwaka 2002 nilijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Es Salaam kusomea “Bachelor in Business Administration (BBA) kwenye programu ya jioni; nilifanya hivyo kwa kuamua kwa kuwa nilitaka nisome huku nikiendelea na kazi. Mkuu wa Programu hiyo wakati huo alishangaa sana kwa umri wangu (wakati huo shahada hiyo walikuwa wakisoma wazee watu wazima wafanyakazi) na matokeo yangu (kwa kuwa yaliniruhusu kwenda kuingia kusoma katika mfumo wa kawaida). Nikamweleza akanielewa kwamba sitaki kusoma kama wanachuo wengine wa kawaida, uamuzi wangu huo ulikuwa na gharama kwa kuwatafsiri yake ni kuwa nilipaswa kujisomesha binafsi.

Kwa hiyo mimi ni kati ya wale ambao hatudaiwi na nchi hii kwa maana ya kwamba sijawahi kuchukua ruzuku wala kusomeshwa na Serikali hii inayoongozwa na CCM; nimesoma kwa jasho la wazazi wangu na langu binafsi. Kwa hiyo, nijibu tu kuhusu elimu yangu ya juu kwamba nimesoma miaka mitatu Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam (mtu aliyosoma kwa kiwango hicho kwenye baadhi ya vyuo duniani hupewa associate degree).

Mwaka 2004 ikaanza misukosuko mbalimbali, mwaka huo ulikuwa ndio unatungwa muswada wa Sheria ya Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu, haya matatizo yanayotokea leo niliyatabiri wakati huo. Niliwasilisha mada kwa wanachuo kwenye ukumbi wa Nkurumah kuchambua udhaifu wa muswada huo na kupata maoni ya wanafunzi kuhusu marekebisho yanayohitajika; wanachuo wakapitisha azimio la kwamba muswada huo upingwe.

Kesho yake nikiwa Morogoro kikazi kukafanyika mgomo hatimaye wanafunzi wakapigwa na kukamatwa.Nakumbuka nilikatiza kazi niliyokuwa nafanya nikarejea kwa kuwa Chuo kiliweka sharti kwamba lazima wanachuo waache mgomo ndio waliokamatwa waachiwe. Wakati huo Serikali ya wanafunzi ilikuwa haisikilizwi, mimi na wengine wachache tukajitolea kuzunguka kampasi na hosteli zote kushawishi wanafunzi kurejea masomoni na wakafanya hivyo.

Serikali ya CCM ikatoa maelekezo kwamba kama tumeweza kuwafanya wanafunzi warudi, hata kama sikushiriki mgomo na sihusiki na masuala ya mikopo kwa kuwa ni mwanafunzi ninayejilipia mwenyewe lazima nisimamishwe; nikiwa mwanafunzi pekee wa BBA niliyesimamishwa wakati huo.

Nikarejea baada ya muda tayari kukiwa na mvutano kati yangu na utawala, mwaka 2005 nikaamua kugombea Ubunge wakati huo nikiwa mwanafunzi; mvutano ukaongezeka zaidi. Na utawala wa Chuo ukawa unapata mashinikizo mengi kutoka kwa Serikali na CCM; wengine wakipendekeza nifukuzwe, wengine nifelishwe na wengine nisiruhusiwe kuingia katika maeneo ya Chuo jioni masomoni kwa kuwa nitakuwa nafanya kampeni.

Nikawa katika mtanziko(dilemma) wa kuchagua ama kuendelea na masomo na kujitoa au kupunguza nguvu kwenye kampeni (mbinu nyingi zilitumika wakati huo, sio sehemu ya majibu yangu ya leo) au niendelee na kampeni. Nafsi yangu ikanituma kuamua kuandika barua yakuahirisha masomo, baada ya matokeo ya uchaguzi wa mwaka 2005 mazingira yalikuwa yamebadilika sana kuweza kurejea kumalizia mwaka au miezi michache iliyokuwa imebaki.

Mwaka 2006 nikiwa Marekani nilitafakari sana na kufikia uamuzi wa kuendelea na kazi hii ya kusimamia mabadiliko na kujiandaa na uchaguzi wa mwaka 2010. Mwaka 2010 niligombea tena na kushinda wakati huo huo nikiongoza kazi za kitaifa za kampeni makao makuu pamoja na Profesa Baregu na wengine; hakuna mahali popote nilipowadanganya wananchi kuhusu elimu yangu, kama nilivyoeleza hapo juu.

Naamini wananchi wa Jimbo la Ubungo walinichagua kwa uwezo na uadilifu wangu, na walijua pia kwamba nilikuwa Chuo Kikuu cha Dar es salaam kwa miaka mitatu. Naamini elimu ni kitu muhimu sana kwa kiongozi, lakini wapo wenye elimu kubwa ya vyeti lakini hawajaelimika na wapo wenye elimu ndogo sana ya vyeti lakini wanaelewa mkubwa wa kutimiza majukumu yao ya uongozi.

Tangu mwaka 2012 na 2013, nimekuwa kwenye mtanziko mwingine na viongozi wangu ndani ya chama wanafahamu; niliomba kuachia majukumu mengine yote katika chama ili nibaki na ubunge peke yake niweze kuwatumikia wananchi wakati huo huo niendelee na masomo zaidi ya elimu ya juu katika fani inayoendana na kazi ninayoifanya ya sasa na matarajio yangu ya baadaye.

Hata hivyo, kwa mwelekeo huu wa Serikali na CCM leo nieleze tu kwamba nikifanya hivyo itakuwa faida zaidi kwa watawala tunapoelekea mwaka 2015; hivyo, nimeamua kama nilivyoamua mwaka 2005; kwamba nitarejea masomoni baada ya CCM kuondoka madarakani na Tanzania kupata Serikali mpya itakayoongozwa na CHADEMA. Kwa sasa nitaendelea kujisomea kila siku ninapopata wasaa kwa kuwa elimu haina mwisho.

Wakili Ridhwan katika maandiko yake amefanya rejea ya suala Kihiyo wa CCM Temeke, nashauri arejee kwenye hukumu ya kesi ile na marekebisho ya sheria yaliyofanywa na Serikali yaCCM kuwalinda wabunge wake vihiyo baada ya hukumu.

Mifano hailingani kwa sababu mimi sijatoa maelezo ya uongo popote. Lakini hata kwa wabunge wa CCM wanaotoa maelezo ya uongo wa wapiga kura, marekebisho hayo yamewawekea wigo wa mianya yakutokea mahakamani. Zamani fomu zakuogembea zilikuwa na mahali pa kujaza elimu ya mgombea, sasa kipengele hicho kimeondolewa. Hivyo, suala la kughushi na kutoa taarifa za uongo haliko kama ilivyokuwa awali, isipokuwa kesi inaweza kufunguliwa ya ukiukwaji wa kawaida wataratibu za kampeni kwa kuwashawishi wapiga kura kwa taarifa za uongo (ndani ya ule muda wa kisheria wa kesi kufunguliwa ambao ulishapita).

Halafu ni jukumu la mlalamikaji sio tu kuthibitisha kwamba uongo ulitolewa bali uongo umeathiri vipi matokeo. Ndio maana leo kuna vihiyo wengi tu wa CCM ndani ya Bunge lakini ni vigumu kuwabana kwa mfumo wetu wa sasa. Baada ya majibu hayo marefu, naamini sasa Nape unaweza sasa kurejea kwenye kujibu; Elimu ya Mnyika ina uhusiano gani na CCM kuahidi kwenye ilani yake na kushindwa kutekeleza kwamba ifikapo mwaka 2010 asilimia 90 ya wananchi wa mijini ikiwemo Dar essalaam watakuwa wanapata maji safi na salama? Ridhwan kwa kuwa umeweza kufanya rejea unaweza pia kueleza ni kwanini Rais Kikwete mwaka 2011 aliahidi kuwa tatizo la maji Dar es Salaam litakuwa historia mwezi Februari 2013 lakini mwezi huo umefika na matatizo bado ni makubwa?

JJ


Ridhiwani kikwete ni janga kubwa la taifa.
 
Unajua kuna wakati kujibishana na mtu hayawani ni kazi sana sasa wewe kwa mtazamo wako hivi huyu Mnyika kama kweli angekuwa na akili nini kilimfanya apoteze miaka 3 na asihitimu? na ninavyojua mimi degree Tanzania inasomwa miaka 3 hata kama ingekuwa ni miaka 4 bado alikuwa amebakiza mwaka 1 mmoja tu ni nini hasa kilichomfanya aache kama sio upungufu wa akili? Nina uhakika pale UDSM hakupata nafasi ya kununua mitihani; yaani graph yake kielimu imeanguka mwambieni aseme ukweli nini kilimkimbiza UDSM!

Kwa hiyo unafikiri kwamba mtu aliyesoma chuo miaka kadhaa, halafu akaacha anakuwa hana akili !?. Mbona ameeleza kwa nini hakumaliza, na mbona sababu zinaeleweka vizuri tu. Kila mtu ana malengo yake katika maisha na mara nyingine mtu analazimika kuacha vitu vingine vya muhimu (kama elimu) wakati fulani fulani ili atimize hayo malengo kwa sababu mara nyingine anakuwa hawezi kupata vyote, wako watu wengi tu ambao wamefanya hivyo, Mimi pia nimewahi kufanya hivyo, na nina akili za kutosha...Mwingine ni Bill Gates unataka kusema naye hana akili ?!.
 
By Monja;
Hahahahaaa! Nape bhana, jamani watanzania nape asiudanganye uma kuwa amesoma, ukweli ni kwamba, nape alisoma ngudu secondary mkoani mwanza wilaya ya kwimba kata ya ngudu na alifika kidato cha pili tu na kufukuzwa shule ndipo alipokataa kabisa kusoma na hivyo kuingizwa kwenye siasa na baba yake mzee Nape wa ccm mpaka leo hajawahi kusoma sehemu yoyote ama ndani au nnje ya nchi, ushahidi ni pale shuleni ngudu secondary niliposoma miaka ya 2005 hadi 2008 hata mama yake anaitwa mama Mhina anaisi hapo ngudu anafanya kazi halmashauri ya kwimba hata yeye sijui kama amesoma kumwezesha kufanya kazi halmashauri,inahitaji uchunguzi na hatua kali zichukuliwe.
 
hahahahaaa! Nape bhana, jamani watanzania nape asiudanganye uma kuwa amesoma ukweli ni kwamba, nape alisoma ngudu secondary mkoani mwanza wilaya ya kwimba kata ya ngudu na alifika kidato cha pili tu na kufukuzwa shule ndipo alipokataa kabisa kusoma na hivyo kuingizwa kwenye siasa na baba yake mzee nape wa ccm mpaka leo hajawahi kusoma sehemu yoyote ama ndani au nnje ya nchi, ushahidi ni pale shuleni ngudu secondary niliposoma miaka ya 2005 hadi 2008 hata mama yake anaisi hapo ngudu anafanya kazi halmashauri ya kwimba hata yeye sijui kama amesoma kumwezesha kufanya kazi halmashauri,inahitaji uchunguzi na hatua kali zichukuliwe.
 
By Monja;
Hahahahaaa! Nape bhana, jamani watanzania nape asiudanganye uma kuwa amesoma, ukweli ni kwamba, nape alisoma ngudu secondary mkoani mwanza wilaya ya kwimba kata ya ngudu na alifika kidato cha pili tu na kufukuzwa shule ndipo alipokataa kabisa kusoma na hivyo kuingizwa kwenye siasa na baba yake mzee Nape wa ccm mpaka leo hajawahi kusoma sehemu yoyote ama ndani au nnje ya nchi, ushahidi ni pale shuleni ngudu secondary niliposoma miaka ya 2005 hadi 2008 hata mama yake anaitwa mama Mhina anaisi hapo ngudu anafanya kazi halmashauri ya kwimba hata yeye sijui kama amesoma kumwezesha kufanya kazi halmashauri,inahitaji uchunguzi na hatua kali zichukuliwe.

Mkuu kwa mtaji huu wa viongozi wa namna hii maendeleo yetu ni ndoto ya mbali.
 
Thanks for complimentary but that will not stop me from speaking my minds; truth must be told no matter what!!!!

hata mkiunganisha akili za viongozi wa CCM wote hamuwezi kumfikia kamanda JJ
 
Kumbae degree kaz bwana,m najiona sijaridhika na degree yangu kumbe mheshimiwa mnyika hana?
 
Kumbae degree kaz bwana,m najiona sijaridhika na degree yangu kumbe mheshimiwa mnyika hana?

Mkuu wenye kupata degree kwa jasho lao na kwa uhalali, wapo kimya, tatizo waliozipata kimangumashi, wao huonyesha dharau kwa wengine, na hujinadi kwa mbwembwe nyingi za kila aina ilimradi wasomeke ni wasomi. Mkuu weka kabisa tangazo kwenye paji la uso kutangaza degree yako.
 
Maisha ya shule ni safari ngumu! Mnyika uvumilivu ulimshinda! Eti mpaka cdm iingie madarakani ndipo akamilishe chuo. Ni aibu.
 
JJ
nimefurahi, kwa jinsi ulivyopangilia maelezo yako dhidi ya shutuma zilizokuwa zinaelekezwa kwako; ni hakika Nape na Ridhiwan kama waliipitia kisawasawa watakua hawana hoja tena.
 
Back
Top Bottom