Mkuu chama,
Msome vizuri kwenye ili bandiko lake ndiyo utajua upuuzi wa John Mnyika,
Anajisifia kuwa alikuwa mwanafunzi bora Dar es Salaam nzima, waliomchagua ndiyo hao hao anawaita wapuuzi.
John Mnyika, anaulizwa elezea elimu yako anasema amesoma Chuo Kikuu miaka mitatu, ananikumbusha siku moja naangalia Fox News alikuwa anahojiwa Bill Gates kuhusu elimu yake alisema wazi sikumaliza chuo.
Hakuna sehemu aliyosema nimesoma Harvard Univesity miaka mitatu.
Kuna upuuzi mwingi sana kaandika Mnyika.
Mbona unaongea vitu ambavyo havi-make sense ? Hivi kama mwanafunzi amekuwa wa kwanza analazimika kuwasifia waliotamka yeye ni wa kwanza ?.....Yeye amefanya vizuri mtihani wake na baada ya matokeo kuwa processed akaonekana ni wa kwanza. Sasa unataka walioprocess matokeo wasifiwe !?...Wametimiza wajibu wao na wanalipwa mishahara kwa kufanya hivyo, mwanafunzi amepeform na amepewa haki yake. Kwa mfano kama mimi nimefanya vizuri na kufaulu mitihani yangu ya chuo kwa mfano, halafu wakufunzi wangu wakanipa marks nzuri (hawawezi kuwa na choice nyingine kama ni waadilifu), siku wakifanya upumbavu (in future) nisiwaseme kwa sababu tu walinipa stahiki yangu !?
Halafu kama Bill Gates amesoma miaka mitatu halafu hataki kuisema hiyo miaka yake aliyokuwa chuo, sasa unataka Mnyika amuige Bill Gates i.e. aangalie kwanza Bill Gates amesemaje kuhusiana na swala hilo halafu na yeye aige !..Ina maana ungekuwa wewe ndio ungefanya hivyo !?....Mnyika na Bill Gates ni watu wawili tofauti, wote wanafanana(kwa maana kwamba hawakumaliza elimu ya chuo kikuu), lakini kila mmoja anaichukulia hali hiyo tofauti (kwa mfano Mnyika ana mpango wa kusoma in the future wakati Bill Gates nadhani hana)...Sasa kama Mnyika ameamua kusema kwamba alisoma chuo miaka mitatu (na ni ukweli) tatizo lake nini !...Besides, kama ulimwona Bill Gates siku hiyo kwenye hiyo interview moja na hakutaja huko kusoma kwake chuo, una uhakika gani kwamba in the past hakuwahi kuitaja hiyo miaka aliyosoma chuo ? Halafu kwenye hiyo interview umesema Bill Gates amesema hakumaliza chuo, hivi kama huyo aliyekuwa anamfanyia interview angemuuliza kwa mfano, "Havard ulisoma miaka mingapi ?" wewe unafikiri asingetaja idadi ya miaka aliyosoma Havard ?