Majibu ya Dr. Masau wa THI kwa maswali mbalimbali

Majibu ya Dr. Masau wa THI kwa maswali mbalimbali

Asante kwa message yako.
Nilikuwa sijui mtandao wenu hadi majuzi nilipoongea na Mr. Mstsimbe na kuniambia kuhusu suala hilo. Baada ya hapo nilifanikiwa kuingia kwenye mtandao wenu na kukuta mambo mengi sana.

Kifupi ni kuwa nisingependa kujiingiza kwenye malumbano au majadiliano yenu na wala sipingi nyie kuendelea na mijadala yenu na hasa kwa vile wote siwajui na mnatumia majina ya kuficha. Lakini kwa ufupi ni kuwa:

1. Nimekwenda Texas Heart Institute wakati huo nimeshakuwa Registered na Medical Council of Tanganyika in 1995 as a Thoracic and Cardiovascular Surgeon baada ya kuwa nimesomea Shahada ya Udhamili katika Upasuaji wa Kifua, Moyo na Mishipa ya Damu (Masters of Medicine in Thoracic and Cardiovascular Surgery) na kufanya kazi Muhimbili katika fani hiyo hadi nilipokwenda Texas mwishoni mwa mwaka 1996.

2. Nilikuwa sponsored na University of Texas Health Science Center-Houston kwenda Texas Heart Institute kwenye Cardiovascular Surgery Fellowship Program. Nilikuwa Texas Heart Institute kwenye hiyo program kuanzia January 1997 hadi June 2000 na katika kipindi hicho nilishiriki katika kufanya operation za upasuaji wa moyo zaidi ya 1800 (vielelezo vyote vipo).

Kwa mujibu wa maelezo yake hapo juu,mimi kama MD student;

(a)Nakubali kuwa Dr.Masau ni surgeon katika field husika-maana ka specialize katika masters course yake.

(b)Alifanya uamuzi wa busara kwenda kushiriki hiyo fellowship,natumai kuwa ilimuongezewa uwezo kiutendaji zaidi,ukizingatia MUHIMBILI asingeweza kupata hiyo nafasi kwa sababu haikuwa na kitengo hicho cha upasuaji ndio maana wagonjwa walikuwa wakipelekwa India.

(c)Ushauri wangu kwa Dr.Masau/Serikali:Kama hiyo fellowship ilikuwa ni ya kushiriki tu kama vile tunavyofanya tukiwa medical college,na kwa sababu Tanzania hakuna practising seniors katika hiyo field (kama niko sahihi) basi kungepatikana fursa ya wewe kwenda kufanya internship in a hospital under supervision ya seniors kama vile tufanyavyo tukiwa internship kuongeza uwezo wa kuchezesha mkono,inajulikana kuwa pamoja na kuhitajika medical theories,kufanya kwa mikono yako ni muhimu sana katik hii fani ya medicine hususwan ya surgery,na ndio maana ili uwe na medical college lazima uwe na affiliated hospital(najua Dr analifahamu sana hili kuliko pengine mimi).

Serikali ingemsaidia hili,ingeleta taswira ya uzalendo kiasi hata tulioko huku ughaibuni tungefikiria siku moja kurudi Nyumbani....lakini kwa namna hii.....dah...anyway,nyumbani ni nyumbani.

Kama ningejua kuwa una fursa,basi ningekushauri ukafanye PhD kabisa...nafikiri ingekuweka katika position nzuri zaidi,watu wengi wa kawaida wangetuliza ""mtima"" juu yako,maana wanaposikia upasuaji moyo...inashtusha kidogo,tushazoea kuona watu wanaenda India.Hapa serikali ingekuwa na nafasi kubwa ya kufanya haya kama ingekuwa inajali watu wake,maana nina hakika sisi tungerudi na kufundishwa na Dr,Masu na kuparactice THI badala ya kufikiria kwenda Texas.

(d)Hata hivyo,kama ni sahihi kuwa 6 kati ya wagonjwa 10 wanaotibiwa THI wanapona,si mbaya sana...ingawa bado inahitajika juhudi za makusudi kabisa,hususwan za mkono mrefu wa serikali kuongeza hadi kufikia angalau 8/10...,maelezo yake yanaonesha yuko exposed sana katika hii field.kwa maana anatambulika na association nyingi sana duniani,kupitia kwake serikali ingeweza kuona namna gani tungewezanufaika naye.

Ni maoni yangu tu.....
Niwieni radhi pale nilipokosea
 
Bado inatutia uoga.....ban

Kuna thread ilikuwa na heading "GT, MAU MAU .. banned" siioni.

Do we need a "Dialogue Concerning The Two Chief World Systems" ?

Are the mods overly jumpy? Is JF overly policed?

dialogo.gif
 
Mtikila pamoja na Umoja wa makanisa walisema wangemfanyia fundraising lakini nadhani ingepatikana nguvu toka Chama kikuuu cha upinzani (CHADEMA ) bas najua kuwa rent ingekuwa ishalipwa na sasa hivi tunajadili mengine
Hao Chadema mwenyekiti wao ana madeni,wangefanya fundrising kumlipia madeni Mwenyekiti wao kwanza......
 
Asante kwa message yako.
Nilikuwa sijui mtandao wenu hadi majuzi nilipoongea na Mr. Mstsimbe na kuniambia kuhusu suala hilo. Baada ya hapo nilifanikiwa kuingia kwenye mtandao wenu na kukuta mambo mengi sana.

Kifupi ni kuwa nisingependa kujiingiza kwenye malumbano au majadiliano yenu na wala sipingi nyie kuendelea na mijadala yenu na hasa kwa vile wote siwajui na mnatumia majina ya kuficha. Lakini kwa ufupi ni kuwa:

1. Nimekwenda Texas Heart Institute wakati huo nimeshakuwa Registered na Medical Council of Tanganyika in 1995 as a Thoracic and Cardiovascular Surgeon baada ya kuwa nimesomea Shahada ya Udhamili katika Upasuaji wa Kifua, Moyo na Mishipa ya Damu (Masters of Medicine in Thoracic and Cardiovascular Surgery) na kufanya kazi Muhimbili katika fani hiyo hadi nilipokwenda Texas mwishoni mwa mwaka 1996.

2. Nilikuwa sponsored na University of Texas Health Science Center-Houston kwenda Texas Heart Institute kwenye Cardiovascular Surgery Fellowship Program. Nilikuwa Texas Heart Institute kwenye hiyo program kuanzia January 1997 hadi June 2000 na katika kipindi hicho nilishiriki katika kufanya operation za upasuaji wa moyo zaidi ya 1800 (vielelezo vyote vipo).

Kwa mujibu wa maelezo yake hapo juu,mimi kama MD student;

(a)Nakubali kuwa Dr.Masau ni surgeon katika field husika-maana ka specialize katika masters course yake.

(b)Alifanya uamuzi wa busara kwenda kushiriki hiyo fellowship,natumai kuwa ilimuongezewa uwezo kiutendaji zaidi,ukizingatia MUHIMBILI asingeweza kupata hiyo nafasi kwa sababu haikuwa na kitengo hicho cha upasuaji ndio maana wagonjwa walikuwa wakipelekwa India.

(c)Ushauri wangu kwa Dr.Masau/Serikali:Kama hiyo fellowship ilikuwa ni ya kushiriki tu kama vile tunavyofanya tukiwa medical college,na kwa sababu Tanzania hakuna practising seniors katika hiyo field (kama niko sahihi) basi kungepatikana fursa ya wewe kwenda kufanya internship in a hospital under supervision ya seniors kama vile tufanyavyo tukiwa internship kuongeza uwezo wa kuchezesha mkono,inajulikana kuwa pamoja na kuhitajika medical theories,kufanya kwa mikono yako ni muhimu sana katik hii fani ya medicine hususwan ya surgery,na ndio maana ili uwe na medical college lazima uwe na affiliated hospital(najua Dr analifahamu sana hili kuliko pengine mimi).

Serikali ingemsaidia hili,ingeleta taswira ya uzalendo kiasi hata tulioko huku ughaibuni tungefikiria siku moja kurudi Nyumbani....lakini kwa namna hii.....dah...anyway,nyumbani ni nyumbani.

Kama ningejua kuwa una fursa,basi ningekushauri ukafanye PhD kabisa...nafikiri ingekuweka katika position nzuri zaidi,watu wengi wa kawaida wangetuliza ""mtima"" juu yako,maana wanaposikia upasuaji moyo...inashtusha kidogo,tushazoea kuona watu wanaenda India.Hapa serikali ingekuwa na nafasi kubwa ya kufanya haya kama ingekuwa inajali watu wake,maana nina hakika sisi tungerudi na kufundishwa na Dr,Masu na kuparactice THI badala ya kufikiria kwenda Texas.

(d)Hata hivyo,kama ni sahihi kuwa 6 kati ya wagonjwa 10 wanaotibiwa THI wanapona,si mbaya sana...ingawa bado inahitajika juhudi za makusudi kabisa,hususwan za mkono mrefu wa serikali kuongeza hadi kufikia angalau 8/10...,maelezo yake yanaonesha yuko exposed sana katika hii field.kwa maana anatambulika na association nyingi sana duniani,kupitia kwake serikali ingeweza kuona namna gani tungewezanufaika naye.

Ni maoni yangu tu.....
Niwieni radhi pale nilipokosea

Hivi huyu MASAU hiyo title yake ya DR inamaanisha PHD ama Mganga??
maana inatuchanganya ,mimi nilikiri alienda USA kufanya phd kumbe sivyo ama inakua je?
 
Hivi huyu MASAU hiyo title yake ya DR inamaanisha PHD ama Mganga??
maana inatuchanganya ,mimi nilikiri alienda USA kufanya phd kumbe sivyo ama inakua je?

Kwanini ulifikiri ameenda kufanya PhD? Unafikiri anaitwa Dr. kwa sababu gani?
 
Imekuwa nongwa kwa Masau kutolipa kodi hummmm.
Mi nadhani iambie serikali ilipe kwanza madeni yote iliyonayo ya mishahara ya wafanyakazi mbali mbali kiasi kwamba mgomo unanukia.
Na ilipe hata wafanyabiashara wanaotoa service kwa hiyo serikali kama mfano wa wanaolisha mashule! ambao waliacha kupeleka vyakula mashuleni na mashule yakafungwa.
I doubt yatafungwa tena in near future maana kulipa kwa serikali yenu ni taabu.
Sasa hamjaiambia hii serikali ya kifisadi mnamshambulia mtaalamu Dr nanii.
Shame upon you.
 
kwani madaktari ili wawe madaktari wanahitaji shahada gani? BA, MA, au PhD????

Tanzania hata ma MA nao ni madaktari yani form 4 kaenda chuo sijui wanaitwa medical assistance.Lakini kwa Tz wote ni ma DR ,ndio maana mimi nashauri kama ni mganga hana PHD asiitwe DR tu ikakomea hapo inabidi patiwe kikolombwezo ,ili kimkolobweze zaidi nasisi tupate kukorombwezeka.
 
(((1. Nimekwenda Texas Heart Institute wakati huo nimeshakuwa Registered na Medical Council of Tanganyika in 1995 as a Thoracic and Cardiovascular Surgeon baada ya kuwa nimesomea Shahada ya Udhamili katika Upasuaji wa Kifua, Moyo na Mishipa ya Damu (Masters of Medicine in Thoracic and Cardiovascular Surgery) na kufanya kazi Muhimbili katika fani hiyo hadi nilipokwenda Texas mwishoni mwa mwaka 1996.

2. Nilikuwa sponsored na University of Texas Health Science Center-Houston kwenda Texas Heart Institute kwenye Cardiovascular Surgery Fellowship Program. Nilikuwa Texas Heart Institute kwenye hiyo program kuanzia January 1997 hadi June 2000 na katika kipindi hicho nilishiriki katika kufanya operation za upasuaji wa moyo zaidi ya 1800 (vielelezo vyote vipo). )))

Ndugu Mkamap.......
Kwa mujibu wa maelezo hayo hapo juu,Dr.Masau alikwenda kufanya fellowship programme ndani ya muda huo uliotajwa.Hakuna maelezo ya kuwa alikwenda kusoma PhD.
Dr.Masau anaitwa Doctor kwa maana ya mtabibu...na hii nafikiri yakubalika hata ikiwa mtu hana PhD katika field husika.
 
Nimesoma hii thread na nimegundua kuwa wengi wa wachangiaji hawataki kujituma hata kutafakari yale mawazo tofauti na ya kwao. Kuhani, Maumau na Sober wamefanya kazi nzuri ya kuelekeza huu mjadala katika upande sahihi na wala sio ushabiki. Tunapozungumzia tiba, hapa hakuna siasa, hakuna CCM wala CHADEMA, kama ni spade itaitwa spade na wala si vinginevyo.

Mimi sina wasiwasi na usomi wa Daktari Masau pale Muhimbili na huku Uchina, Japokuwa facts zinasema amewahi kuishi Texas lakini hajawahi kuwa Daktari aliyekuwa na mamlaka ya kufanya shughuli za kidaktari kwa mujibu wa sheria za Texas. Endapo, by implication alijionesha kuwa ni Daktari aliyekuwa anapractise huko Texas basi alikuwa anadanganya, kwa hiyo ni kinyume na miiko ya kazi yake.

Pili, Masau kama daktari alipaswa kuonesha kiwango cha juu cha tabia njema na uaminifu. Endapo kama aliingia mkataba halali na NSSF kwa ajili ya pango (rent) alitakiwa alipe kwa wakati bila kulimbikiza. Aidha, ni vema Daktari Masau aoneshe mahesabu yake ya kila mwaka kama alikuwa anawithhold fungu la rent ambayo iko kwenye dispute. Ili kuthibitisha kuwa yeye ni mtu wa tabia njema basi ni vema wakati kesi yake ipo mahakama angeli-deposit hicho kiasi cha pesa anazodaiwa katika akaunti ya mahakama kuonesha kuwa nia yake ni njema na pesa zipo. Kinyume cha hapo kama hizo pesa hazipo basi suala la uaminifu limemtupa mkono na anafungua milango ya watu kutaka kujua na mengine zaidi.

Mwisho, ninatoa wito kwa wataalam wetu wazidi kujitokeza kwa wingi kuanzisha asasi zao binafsi lakini kwa kuwa na mipango itakayokuwa endelevu na itakayozingatia pamoja na mambo mengine taratibu zote ikiwa ni pamoja na kuangalia basic business ethics na kufanya risk analysis. Tusijibweteke kwa kufanya mambo kiholela na yanapokwenda kombo tunaanza kutaka huruma, ulimwengu huo ulikwishapita.

Nilipoandika posting yangu hiyo hapo juu nilikuwa nina matumaini makubwa kuwa Daktari Masau atajitokeza walau kutuonesha mahesabu ya mwaka ya THI ili iwe rahisi kupata ukweli kulikoni kubuni mambo.

Hata hivyo ninapenda kwa wakati huu nitafakari nanyi JF memba wenzangu juu ya kodi ya serikali / rental withholding tax ya kuanzia kipindi ambacho THI ilianza kupanga kwenye majengo ya NSSF.

Je hii kodi (itokanayo na deni ambalo halijalipwa) imeweza kukusanywa na kuwakilishwa kunakohusika au kama bado ni vipi mamlaka zinazohusika zimechukua hatua za kuidai kodi yetu?
 
Tanzania hata ma MA nao ni madaktari yani form 4 kaenda chuo sijui wanaitwa medical assistance.Lakini kwa Tz wote ni ma DR ,ndio maana mimi nashauri kama ni mganga hana PHD asiitwe DR tu ikakomea hapo inabidi patiwe kikolombwezo ,ili kimkolobweze zaidi nasisi tupate kukorombwezeka

Hayo maandishi mekundu ndugu mkamap sio kweli kabisa. Kwa wananchi wa vijijini wanaelewa ili mradi wewe unatiby basi unaitwa DR.

Kwa ujumla title ya DR. inatumika kwa watu waliosoma na kufuzu mafunzo yafuatayo
1. Udaktari wa tiba ya binadamu [Doctor of Medicine, (M.D)]
2. Udaktari wa tiba ya wanyama [Doctor of Veterinary Medicine (BVM)]
3. Udaktari wa falsafa [Doctor of Philosophy (PhD)]
4. Udaktari wa Sayansi [Doctor of Science (D.Sc.)]
5. Aina nyingine zinazofanana na no. 3 & 4 ni kama vile Doctor of Engineering (D. Eng., Doctor of Technical Science (D. Tech. Sc.) n.k kutegemeana na jinsi chuo kikuu husika au nchi inavyotambua shahada za juu.
6. Pia kuna Udaktari wa heshima kama Doctori Honoris Hausa

Kwenye namba 1 & 2 ukihitimu shahada ya kwanza tu unapata sifa ya kutumia title ya Dr.(English) au DK. (Kiswahili)

Kwenye namna 3, 4 & 5 lazima kwanza uwe na MSc au M.A degree ndo ufanye hizo programme ili upate kuitwa Dr.

Kwenye namba 6, udaktari wa heshima, kila chuo kinachotunuku shahada ya heshima kina vigezo vyake na sababu za kutunuku.
 
vyote hivi ni chuki wala usikate tamaa Dr. Masau. haya yanaotokea yanakatisha tamaa wataalam wengine kuja kuwekeza nchini. serikali ilikuwa inataka huu mradi uwe chini yao ndio maana wanampiga vita Dr.
 
Imekuwa nongwa kwa Masau kutolipa kodi hummmm.
Mi nadhani iambie serikali ilipe kwanza madeni yote iliyonayo ya mishahara ya wafanyakazi mbali mbali kiasi kwamba mgomo unanukia.
Na ilipe hata wafanyabiashara wanaotoa service kwa hiyo serikali kama mfano wa wanaolisha mashule! ambao waliacha kupeleka vyakula mashuleni na mashule yakafungwa.
I doubt yatafungwa tena in near future maana kulipa kwa serikali yenu ni taabu.
Sasa hamjaiambia hii serikali ya kifisadi mnamshambulia mtaalamu Dr nanii.
Shame upon you.

serikali yetu hailipi hata waalimu mishahara ya waalimu acha madeni ya nje. nongwa inakuwa kwa THI?
 
Back
Top Bottom