Majibu ya hoja za uzi kwanini ardhi ya Mbagala haina thamani nitajibu humu

DAR inavituko Sana. Miaka miwili Sasa nipo Kaskazini ya Dar es salaam ngoja nikupitishe Maeneo hatari na kukabwa nje nje

1.Kawe Mzimuni uswaz Sana pameachwa mbali Sana na Mbagala yote kwa Ujumla.

2.Tegeta kwa Ndevu eneo la Msichoke ni hatari na ukabaji ni Jambo la kawaida hakuna Barabara za kupita mavi hovyo hovyo kutapakaa mitaani Miguu ya kuku na utumbo kawaida Sana.

3.Tegeta Machinjoni mpaka Uwanja wa Panga ni hatari tupu hapafai kwa Maisha ya binadamu vibaka ni Wengi wanakaba mpaka Mchana.

4.Kunduchi Mtongani ni Uswazi hasa hata viwanja Bei rahisi Sana no value at all. Huko Panya road normal Sana.

5.Bunju Usalama yaani ni Vituko tupu hapo wamechanganyika Malofa na wanaojiweza

6.Mbweni Maputo huko ni hovyo sijawahi Maisha ya ajabu Kama hayo hapa Dar es salaam.

7.Msasani Maandazi Road Kama unataka kwenda shoppers hakika nawaambieni Mbagala Ipo juu Sana kuliko Hilo eneo yaani ni chafu Sana muda wote linanuka tope na vinyesi.

8. Kinondoni Shamba yaani ni Uswahilini iliyopitiliza Hali ya kawaida.

9.Mwananyamala kuanzia kwa sindano,kidile,Manjunju, Mama Zacharia mpaka kutokea Tandale yaani ni Takataka tupu hayo yanayozungumziwa Mbagala ni nafuu Sana kuliko hayo maeneo yaani Mautumbo ya kuku ,vyoo kuzibuliwa hovyo, Pombe za kienyeji tena zilizolala siku tatu mpaka wiki zipo Mwananyamala.

9.Nenda Mikocheni A maeneo ya nyuma ya Choppers plaza hutoamini macho yako yaani ni Uswahilini huwezi amini macho yako kukabwa na kuvunjiwa ni kawaida Sana.
 
Mbagala hakuna kiwanja cha 5mil hata chamazi sasa hivi hakuna kiwanja cha 1.5mil..
Kwa sasa mbagala hauwezi kupata kiwanja labda ununue nyumba ubomoe
Frem kupanga rangi tatu kwa ajili ya biashara laki tano kwa ufupi sikuamini mpaka nilipoona Mtu anasaini Mkataba wa Mwaka kwa Milioni sita .
Maisha yanaenda mbio sana
 
Frem kupanga rangi tatu kwa ajili ya biashara laki tano kwa ufupi sikuamini mpaka nilipoona Mtu anasaini Mkataba wa Mwaka kwa Milioni sita .
Maisha yanaenda mbio sana
Rangi 3 kuna mzunguko mkubwa sana wa biashara, frame kuwa 500k kwa mwezi ni sawa kabisa
 
Jamaa ni mfanya biashara kariakoo,complains zake ni kila siku alikuwa anavamiwa na wezi,so he decides to shift to Boko!
Sasa jiulize .Ukabaji wa Boko magengeni umeisha lini.

Jiulize Panya road Kawe Mzimuni jekule ni mbagala.

Je kule Kunduchi Panya road ni Mbagala? Swali Panyaroad kule Tebata ni Panya Road ?

Upanyaroad kule Macongo ni Mbagala.

Kwa Hali ya Dar es salaam kila Wilaya inayo Maisha bora na hovyo hovyo hakuna anayeweza kusema Wilaya Ipo best.
 
Uko sahihi mkuu,that could be a puzzle?
 
Nimekulia kinondoni Toka mwaka 1992 naijua DAR ndani-nje watu wengi wanadharau mitaa tunayoishi ya mbagala bila kujua undani wake na ukiona MTU anaponda mitaa yetu ya mbagala ujue hiyo ni WAKUJA HAPA MJINI...
Nimegundua wengi hapa jukwaaani wamekuja mjini Kwa fuso za nyanya ndiyo maana hawajui kitu kuhusu DAR
 
Rangi 3 kuna frem mpaka za mil 1
Mbande kuna frem za laki 6
Naishi mbagala chamazi mkuu huku nimejenga Toka Toka 2013 na siwezi kwenda kuishi wilaya nyingine zaidi ya temeke hasa huku mbagala..nafurahia Sana maisha yetu ya chamazi huwa nikienda mitaa yangu ya zamani kinondoni wanakuta ndugu zangu hasa wajomba zangu na mama zangu wadogo jinsi walivyochoka ni sifa Tu za kuishi kinondoni kwenye nyumba zao za urithi tena zimechoka.
Fusra za maisha zilizopo mbagala hauwezi kufananisha na sehemu nyingine hapa Tanzania
 
Hii kama noma Anyway haya[emoji3][emoji2]
 
Hata Reginald Mengi alikiri kulala na mbuzi na Ng'ombe nyumba moja

Haohao waliotoka kulala na ng'ombe walisafiri na Ng'ombe mpaka Dsm kisha wakaja kununua maeneo yenu na kuwekeza kisha wakawaajiri ninyi waswahili

Sasa ninyi mmebakiwa na maneno mengi na majungu tu [emoji23]
 
Bill Lugano my brother I miss you. Ngoja nikupigie simu, nimeona private jet yako ile mpya Gulf Stream imeegeshwa, najua tu upo nchini kwa mapumziko kidogo. Let me holla at you
 
Hilo Swala halihitaji akili kubwa,eneo linaweza kupanda thamani kutokana na mipango,vitegauchumi,sera za serikali,Tanga Mtwara zote Zina bahati lakini mbona ni Dar ndio imeendelea sana(inachangia 80% kwenye Pato la nchi).
Kabla ya kujengwa UDOM,na tamko la serikali kuhamia Dom,Dom ilikuwa ya kawaida ardhi bei Chee,sasa hv,haishikiki)
 
Ulishawahi kumsikia mengi akitoa kashfa kwa watu fulani?
Uko Kijiji kwenu mmeacha maendeleo gani?
 
Mimi mwenyewe nyumbani ni mwenge baada ya kuona fursa nimehamia mbagala mbande wale jamaa zangu niliowaacha mwenge sasa hivi wapo wapo wanapiga day works maduka ya nguo sio kwamba hawajasoma wamesoma vzr tu ila bado wana mentality mbovu kuhusu mbagala.
Wanadhani mbagala ya miaka hiyo ndio hii hii ya leo, mbagala imejitosheleza kwa kila kitu % kubwa mahitaji yote watu wanamaliza mbagala hawaendi k/koo ....
1-stend kubwa kabisa ya mwendo kasi ipo mbagala
2-branches zote za bank zipo mbagal
3-Mzunguko wa pesa mbagala ni mkubwa kuliko mbezi,goba,kimara,mwenge,ubungo,sala sala
4-miundombinu bora kabisa umeme,maji,huduma za afya
5-ni rahisi zaidi kufika ktk ya mji
6-tuna kiwanja bora kabisa cha mchezo cha azam
 
Ninachojua kuna Watu wana Maisha mazuri wanaishi huko Mbagala Kunakodharaulika kuliko hata Waishio Oysterbay, Masaki, Mikocheni, Upanga, Kijitonyama, Mbezi Beach, Goba, Sala Sala, Kigamboni, Tegeta na Mbweni.
Kuna mwamba anaishi buza ana landcruiser,BMW,landrover discover,pembeni terous,Noah,hilux,gorofa magari ya biashara ndo usiseme.
Mtu ana ghorofa inaukuta mrefu,wanangu nilosoma nao baadhi wapo kijitonyama wanna chumba kimoja kila mmoja πŸ™‚πŸ™‚πŸ™‚
 
tunakusbir mtetezi wanaishusha hadhi sana mbagala au Texas
 
Tuko pamoja Saanaa jirani yangu karibu Sana chamazi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…