Umenijibu vizuri sana, swali la Nyongeza kwa kuwa matumizi ya umeme yameongezeka tofauti na zamani na kwa maana hiyo mapato ya serikali pia yameongezeka na mimi naamini kabisa serikali inatakiwa kufanya projection sijui kwa kiswahili nini na ndo maana kuna sensa zinafanyika kujua idadi ya watu na makazi ya hao watu ili huduma za jamii ziendane na ongozeko la watu au na mahitaji ya watu, Kwa nini serikali haikuona kama MW600 hazitoshi kwa kipindi hiki tulichonacho na hata hizo MW300 ambazo hazijaanza kuingia kwenye grid ya Taifa nazo pia hazitatosha hata kama zitaingizwa leo kwenye gridi ya Taifa kama walivyojenga shule za kata(Ingawa shule zote za kata zimejengwa kwa nguvu ya wananchi)?
Kuhusu ukame hiyo naona ni kuhamisha magoli, Naomba ufanunuzi kama ukame umeanza 2007 kwa nini walijenga mitambo ya IPTL?
Poitless!!2005 Kikwete, aah kisha maliza muda wake. Mchagueni Slaa ambae anashindwa hata kutatua mgogoro wa madiwani watatu na Mbunge mmoja.
Serikali inayoendesha mambo yake kwa kutegemea watabiri ni serikali ya ajabu sana,sasa wanaoisapoti tutawaitaje?Soma post #45 kwa miradi iliyopo. Halafu kawalaumu watu wa weather-forecast waliosema kuwa hakuna matatizo ya mvua mpaka mwisho wa 2011.
IPTL a.k.a Richmond!!Ndio mdudu gani huyo?
Serikali inayoendesha mambo yake kwa kutegemea watabiri ni serikali ya ajabu sana,sasa wanaoisapoti tutawaitaje?
Halafu dada Faiza naomba tukupe likizo ya malipo.Kusudi utupe sisi wazalendo nafasi ya kuchambua vizuri hekima za humu jamvini.Hivi huoni aibu kumfuata nzi?Ebu jaribu kufuata nyuki bwana.
Chonde chonde mimi mdogo wako tena si ajabu mwanao wa pili.Naomba ujaribu basi kuiga busara kama hauna kabisa.
Heli miye muongo, kuliko kuwa kilaza.Ina maana wewe ni muongo.
Hayo ya juu sikujibu kwani ni pumba tuu, au hujui kuwa huwezi tuu kuushusha umeme mkubwa kila kijiji? lazima uwe na substations?
Hilo la mwisho ni very simple, gas inaweza kusafirishwa na mabomba yakaongezwa na au kutumia transport ya gas trucks mpaka bomba kubwa litapokuwa tayari.
Jamani hebu kuweni, kidooogo mna appreciate yafanywayo, hivi miaka 80 (80 Years) 600MW na miaka 3 (3 Years) 300MW na tayari zaidi ya 2,000 signed and projects have started. Hivi kuna nini ambacho mnashindwa kuelewa? Au ndio majina tu yanawatatiza?
Soma post #45 kwa miradi iliyopo. Halafu kawalaumu watu wa weather-forecast waliosema kuwa hakuna matatizo ya mvua mpaka mwisho wa 2011.
Data unazileta cye twazijua toka wewe ujaijua JF.In auditing there z smthn fraudulent known as "Window dressing data" sasa kwenye siasa nacho kipo.Data zisizo na uwiano kulingana na hali halisi nazo tunaziita "Window dressing data" na kwa mtu mwelewa hawezi tegemea kutengeneza hoja kulingana na data kama hizo. Hivi unadhani kuibadili IPTL iwe ya gas na kuibua mradi wa asili ya IPTL Mwanza ni utimamu kweli?Unajua huu co wakati wa kushangilia goli moja wakati tumeshafungwa saba na dakika tisini zinabisha hodi.Mwenye busara hu appreciate kazi za watu si kutwa Kikwete hajafanya hiki, hajafanya kile.Data zipo mbona hamzijibu? mnanikurupukia mie, mie naleta data za uhakika. Leteni zenu! achana namimi kabisa tena, wewe jibizana na hoja zangu tu.
Rais Kikwete: Mimi nasema hivi yeye si Mbunge atoe maarifa yake tu; anayo maarifa gani na anapendekeza kitu gani. Kwa sababu toka Uhuru mabwawa tuliyotengeneza ni Kidatu MW200, Mtera MW80, Kihansi MW 165 mimi nilipokuwa Waziri wa Nishati, pale Pangani tumeongeza.Sasa ufikirie kwamba toka Uhuru tumeweza kuzalisha umeme wa MW600, lakini toka 2009 mpaka Disemba mwaka huu tutakuwa tumeongeza MW300!
Wakuu heshima mbele,
Yafuatayo ni mahojiano kati ya Rais Kikwete na Mwandishi wa BBC Bw. Omar Mutasa huko Afrika Kusini ambako Rais Kikwete alikuwa anaendelea na ziara yake ya Kiserikali.
BBC: Kuna njia kama umeme wa jua, umeme wa kutokea ardhini wa mvuke, kwanini serikali haitafuti njia mbadala kuzalisha umeme kwa njia hizo?
Rais Kikwete: Nasema hivi, hata umeme wa jua lazima ujenge, umeme wa mvuke lazima ujenge, si kitu cha mwezi mmoja. Nasema huo ndio ukweli wenyewe na wakati mwingine na nyinyi mjifunze hayo mambo ya kitaalamu kulikoni kuuliza tu hivi hivi. Unajua ungekuwa na wewe unauliza kwa hoja - unajua kwamba hiki kitu hiki ingekuwa umeme wa jua miezi miwili tu upo - tungeweza kufanya hivyo.Sisi sasa hivi kwa mfano tunajiandaa kuzalisha umeme wa kutumia Upepo, pale Singida. Tuna mwaka wa tatu sasa tuna mipango na Wakorea wa Kusini, umeme haujakuwepo. Kwa hiyo nasema hayo ni maelezo rahisi. Wanasema mbona jua lipo? katengeneze umeme wa jua kama jua lipo! (kicheko).
MWISHO.