Ukiangalia mradi wa Nyakato wa MW60 ambao ni wa Mafuta mazito, na mradi wa IPTL ambao ni kuibadilisha mitambo badala ya mafuta mazito itumie gas, hapo unashindwa kuelewa kama hawa watu akili zao zinafanya kazi vizuri au ni mambo ya 10%, IPTL iko Tegeta ambapo ni kama 20km kutoka bandarini mmeshindwa kwa sababu ya gharama, leo mnataka mjenge Mwanza ambapo ni zaidi ya 1000km kutoka bandarini kuna nini hapo?
Mradi wa Shinyanga-Buzwagi na mradi wa Musoma-Nyamongo ni miradi ambayo inaenda mgodini lakini Migodi inachangia asilimia ngapi kwenye pato la Taifa, na kama kusingekuwa na hiyo migodi huwezi ona mradi huo unajengwa, na afadhali basi wangekuwa wanajenga substation katikati ya miradi ili kuwapatia wananchi wanaopitiwa na hiyo miradi umeme.
Kuna kipindi nilienda mgodi wa Buhemba umeme umefika Buhemba lakini wanavijiji wa njiani wanaangalia nyaya tu zinapita juu, hata miradi ya maji watu wanashuhudia mitaro inachimbwa kwa ajili ya kuweka mabomba tu, wanavijiji hawafaidiki na chochote, kwa hali kama hiyo hata kama kuna hujuma zitafanyika kwenye hiyo miradi wananchi hawezi kuwa walinzi kwa hakika.
Miradi mingi uliyotaja inaongelea kutumia gas, kuna jamaa yangu anafanya PAE anasema gas ya kutosha kwenye reservoir ipo ila namna ya kuisafirisha na itosheleze mitambo yote inayojengwa ndo hamna, hakuna bomba lililojengwa zaidi ya lililopo ambalo tayari limekuwa saturated, mambo ni magumu kuliko unavyofikiria ndugu FF.
Kingine naomba ufafanuzi kwa nini mitambo ya Aggreko ilizimwa?