Majibu ya Kikwete na BBC: Tumevuna tulichokipanda

Majibu ya Kikwete na BBC: Tumevuna tulichokipanda

Kilichofanywa na mafisadi kwa miaka 10 tu ni balaa,ukimwambi mtu mwenye akili timamu kuwa kuna serikali ipo madarakani kwenye nchi yenye vyanzo lukuki vya umeme kuwa ina mpango tena sio imekamilika yani mipango ya megawati 300,tena kwa serikali ya chama kilichokaa madarakani 50 years!!This is insane!!
 
Umenijibu vizuri sana, swali la Nyongeza kwa kuwa matumizi ya umeme yameongezeka tofauti na zamani na kwa maana hiyo mapato ya serikali pia yameongezeka na mimi naamini kabisa serikali inatakiwa kufanya projection sijui kwa kiswahili nini na ndo maana kuna sensa zinafanyika kujua idadi ya watu na makazi ya hao watu ili huduma za jamii ziendane na ongozeko la watu au na mahitaji ya watu, Kwa nini serikali haikuona kama MW600 hazitoshi kwa kipindi hiki tulichonacho na hata hizo MW300 ambazo hazijaanza kuingia kwenye grid ya Taifa nazo pia hazitatosha hata kama zitaingizwa leo kwenye gridi ya Taifa kama walivyojenga shule za kata(Ingawa shule zote za kata zimejengwa kwa nguvu ya wananchi)?

Kuhusu ukame hiyo naona ni kuhamisha magoli, Naomba ufanunuzi kama ukame umeanza 2007 kwa nini walijenga mitambo ya IPTL?

Soma post #45 kwa miradi iliyopo. Halafu kawalaumu watu wa weather-forecast waliosema kuwa hakuna matatizo ya mvua mpaka mwisho wa 2011.
 
Soma post #45 kwa miradi iliyopo. Halafu kawalaumu watu wa weather-forecast waliosema kuwa hakuna matatizo ya mvua mpaka mwisho wa 2011.
Serikali inayoendesha mambo yake kwa kutegemea watabiri ni serikali ya ajabu sana,sasa wanaoisapoti tutawaitaje?
 
Duh kweli mliotutangulia kiumri mmepitia mengi sana.Leo hii ndio natambua nini chanzo cha umaskini Tanzania .
#.Kwanza kabisa kuogopa kivuki chako ni dalili za kushindwa maisha yako,yaani wewe bora siku ipite tu.Tukimvua cheo cha urais basi hana tofauti na mtu anayeogopa kivuli.
#.Pili majibu mepesi kama haya yana mahala pake nako ni vijiweni ili kusukuma muda tu.
#.Tatu watanzania mlioshiriki kupiga kura na kumchagua huyu bwana walai mlaaniwe,ninyi hekima haiwastahili kabisa.Kwani ninyi ninyi ndio tulitegemea mumshahuri na kumkosoa huyu bwana .
#.Nne na mwisho tulioelewa somo basi tumfunze huyu bwana.Siki hizi wanatoa likizo za malipo basi tumpatie likizo na ajichagulie mwenyewe nchi ya kuishi tutamlipia tu ili bora tuiokoe nchi yetu na Watanzania wote.
 
Unajua haya majibu yake ya kipuuz ndiyo yanayopelekea hata baadhi ya mawaziri wake kumdharau, m2 km Sitta alishagamuona kuwa huyu mtu ni kanjanja ndiyo maana huwa anaitolea maneno ya kashfa sana hii serikali ya ****** na anajua hakuna wa kumfanya kitu chochote.
 
Serikali inayoendesha mambo yake kwa kutegemea watabiri ni serikali ya ajabu sana,sasa wanaoisapoti tutawaitaje?

Duhh, sikutegemea kama utakuwa hujui umuhimu wa weather forecasts in our daily decisions, pole sana.
[h=3]Utility companies[/h]
An air handling unit is used for the heating and cooling of air in a central location (click on image for legend).


Main article: Degree day
Electricity and gas companies rely on weather forecasts to anticipate demand which can be strongly affected by the weather. They use the quantity termed the degree day to determine how strong of a use there will be for heating (heating degree day) or cooling (cooling degree day). These quantities are based on a daily average temperature of 65 °F (18 °C). Cooler temperatures force heating degree days (one per degree Fahrenheit), while warmer temperatures force cooling degree days.[SUP][81][/SUP] In winter, severe cold weather can cause a surge in demand as people turn up their heating.[SUP][82][/SUP] Similarly, in summer a surge in demand can be linked with the increased use of air conditioning systems in hot weather.[SUP][83][/SUP] By anticipating a surge in demand, utility companies can purchase additional supplies of power or natural gas before the price increases, or in some circumstances, supplies are restricted through the use of brownouts and blackouts.[SUP][84]

Soma zaidi: [/SUP]http://en.wikipedia.org/wiki/Weather_forecasting
 
Halafu dada Faiza naomba tukupe likizo ya malipo.Kusudi utupe sisi wazalendo nafasi ya kuchambua vizuri hekima za humu jamvini.Hivi huoni aibu kumfuata nzi?Ebu jaribu kufuata nyuki bwana.
Chonde chonde mimi mdogo wako tena si ajabu mwanao wa pili.Naomba ujaribu basi kuiga busara kama hauna kabisa.
 
Unategemea nn kutoka kwenye hii statment, "mzee ruksa alikaa miaka 10 hakuyamalza, mzee Nkapa miaka 10 hakuyamalza, mie miaka 5 sijayamalza na mingne mitano hayatakwsha"
 
Halafu dada Faiza naomba tukupe likizo ya malipo.Kusudi utupe sisi wazalendo nafasi ya kuchambua vizuri hekima za humu jamvini.Hivi huoni aibu kumfuata nzi?Ebu jaribu kufuata nyuki bwana.
Chonde chonde mimi mdogo wako tena si ajabu mwanao wa pili.Naomba ujaribu basi kuiga busara kama hauna kabisa.

Mwenye busara hu appreciate kazi za watu si kutwa Kikwete hajafanya hiki, hajafanya kile.

Data zipo mbona hamzijibu? mnanikurupukia mie, mie naleta data za uhakika. Leteni zenu! achana namimi kabisa tena, wewe jibizana na hoja zangu tu.
 
Ni kama mtu anavaa Thong (si inaficha mbele tu kwa kuwa nyuma hakuna noma) Mungu ampe maisha marefu
 
Hayo ya juu sikujibu kwani ni pumba tuu, au hujui kuwa huwezi tuu kuushusha umeme mkubwa kila kijiji? lazima uwe na substations?

Hilo la mwisho ni very simple, gas inaweza kusafirishwa na mabomba yakaongezwa na au kutumia transport ya gas trucks mpaka bomba kubwa litapokuwa tayari.

Jamani hebu kuweni, kidooogo mna appreciate yafanywayo, hivi miaka 80 (80 Years) 600MW na miaka 3 (3 Years) 300MW na tayari zaidi ya 2,000 signed and projects have started. Hivi kuna nini ambacho mnashindwa kuelewa? Au ndio majina tu yanawatatiza?

Tatizo lako ni kwamba hutaki kuuona ukweli, unajaribu kuchangia hasa kwa ushabiki, Nimekuuliza mtambo wa IPTL wanataka kuubadilisha utumie gas badala ya mafuta at the same time wanajenga mtambo wa mafuta ambao uko mbali sana kutoka bandarini wewe unaona pumba, hii nini kama sio kuchanganyikiwa?

Na kigezo cha kwamba MW600 kwa muda wote halafu ndani ya miaka3 MW300 naona na wenyewe ni upofu tu na kutotaka kuona ukweli, utaaje kujisifia MW300 wakati kuna mgawo kila siku, na wale pamoja na kwamba MW600 tu ndo walizalisha lakini hapakuwa na mgawo wa kizembe kama huu.

Na mwisho hujanijibu kwa nini mtambo wa Aggreko ulizimwa?
 
Soma post #45 kwa miradi iliyopo. Halafu kawalaumu watu wa weather-forecast waliosema kuwa hakuna matatizo ya mvua mpaka mwisho wa 2011.

Hiyo habari nimeisoma kutoka kwenye tovuti ya Tanesco kwenyewe sio lazima nisome kwenye post yako, Mheshimiwa rais alisema shida ni ukame kwa maana kwamba ukame umeanza kipindi yeye akiwa rais sasa swali langu kama kweli ukame umeanza yeye akiwa rais kwa nini basi walijenga IPTL tena yeye akiwa waziri mwenye dhamana ya Nishati?
 
Mwenye busara hu appreciate kazi za watu si kutwa Kikwete hajafanya hiki, hajafanya kile.Data zipo mbona hamzijibu? mnanikurupukia mie, mie naleta data za uhakika. Leteni zenu! achana namimi kabisa tena, wewe jibizana na hoja zangu tu.
Data unazileta cye twazijua toka wewe ujaijua JF.In auditing there z smthn fraudulent known as "Window dressing data" sasa kwenye siasa nacho kipo.Data zisizo na uwiano kulingana na hali halisi nazo tunaziita "Window dressing data" na kwa mtu mwelewa hawezi tegemea kutengeneza hoja kulingana na data kama hizo. Hivi unadhani kuibadili IPTL iwe ya gas na kuibua mradi wa asili ya IPTL Mwanza ni utimamu kweli?Unajua huu co wakati wa kushangilia goli moja wakati tumeshafungwa saba na dakika tisini zinabisha hodi.
 
Kikwete ana matatizo kujieleza, akibanwa anakuwa kama ana hasira hivi.

Lakini, kama haya maelezo ni kweli you gotta hand it to him, and ask him "what took you so long?"

Rais Kikwete: Mimi nasema hivi yeye si Mbunge atoe maarifa yake tu; anayo maarifa gani na anapendekeza kitu gani. Kwa sababu toka Uhuru mabwawa tuliyotengeneza ni Kidatu MW200, Mtera MW80, Kihansi MW 165 mimi nilipokuwa Waziri wa Nishati, pale Pangani tumeongeza.Sasa ufikirie kwamba toka Uhuru tumeweza kuzalisha umeme wa MW600, lakini toka 2009 mpaka Disemba mwaka huu tutakuwa tumeongeza MW300!
 
Wakuu heshima mbele,
Yafuatayo ni mahojiano kati ya Rais Kikwete na Mwandishi wa BBC Bw. Omar Mutasa huko Afrika Kusini ambako Rais Kikwete alikuwa anaendelea na ziara yake ya Kiserikali.


BBC: Kuna njia kama umeme wa jua, umeme wa kutokea ardhini wa mvuke, kwanini serikali haitafuti njia mbadala kuzalisha umeme kwa njia hizo?

Rais Kikwete: Nasema hivi, hata umeme wa jua lazima ujenge, umeme wa mvuke lazima ujenge, si kitu cha mwezi mmoja. Nasema huo ndio ukweli wenyewe na wakati mwingine na nyinyi mjifunze hayo mambo ya kitaalamu kulikoni kuuliza tu hivi hivi. Unajua ungekuwa na wewe unauliza kwa hoja - “unajua kwamba hiki kitu hiki ingekuwa umeme wa jua miezi miwili tu upo” - tungeweza kufanya hivyo.Sisi sasa hivi kwa mfano tunajiandaa kuzalisha umeme wa kutumia Upepo, pale Singida. Tuna mwaka wa tatu sasa tuna mipango na Wakorea wa Kusini, umeme haujakuwepo. Kwa hiyo nasema hayo ni maelezo rahisi. Wanasema “mbona jua lipo?” katengeneze umeme wa jua kama jua lipo! (kicheko).
MWISHO.

2005 mpaka 2011....unahiyaji miaka mingapi kujenga?
 
Yan me naona ttz lake yeye alikua anataka kua rais tu,ila alikua hajui atafanya nn na huo urais,mana kma alijua matatizo yapo na aliyakuta angekua na plan kbs in hand kwamba ntashugulikia hili mpk nikimaliza muda wangu mambo yatakua sawa, ila suala la kisema nimeyakuta matatizo ni uzembe na uvivu wa kufikiria na ni ishara ya kua na weak character unakimbizia majukumu yako kwa walio kutangulia
 
Back
Top Bottom