Majibu ya Postmoterm yaonyesha kwamba Hayati Ali Kibao alipigwa sana na kumwagiwa Tindikali

Yaanii siasa zimetufikisha hapa ? Hadi kuuana kisa siasa ? Ili yulee aweeer kiongozo ? Siaminiìiii
 
Kumbukumbu la Torati 28
18 Utalaaniwa uzao wa tumbo lako, na uzao wa nchi yako, maongeo ya ng'ombe wako, na wadogo wa kondoo zako.

19 Utalaaniwa uingiapo, utalaaniwa na utokapo,

20 Bwana atakuletea laana na mashaka, na kukemewa, katika yote utakayotia mkono wako kuyafanya, hata uangamie na kupotea kwa upesi; kwa ule uovu wa matendo yako, uliyoniacha kwayo.

21 Bwana atakuambatanisha na tauni, hata atakapokwisha kukuondoa katika nchi uingiayo kwa kuimiliki.

22 Bwana atakupiga kwa kifua kikuu, na kwa homa, na kwa kuwashwa, na kwa hari ya moto, na kwa upanga, na kwa ukaufu, na kwa koga; navyo vitakufukuza hata uangamie.

23 Na mbingu zako zilizo juu ya kichwa chako zitakuwa shaba, na nchi iliyo chini yako itakuwa chuma.

24 Bwana atafanya mvua ya nchi yako iwe vumbi na mchanga; itakujilia juu yako kutoka mbinguni hata uangamie.

25 Bwana atakufanya upigwe mbele ya adui zako; utawatokea juu yao kwa njia moja, lakini utakimbia mbele yao kwa njia saba; nawe utatupwa huko na huko katika falme zote za duniani.

26 Na mzoga wako utakuwa chakula cha ndege wote wa angani, na wanyama wote wa duniani, pasiwe na mtu wa kuwafukuza.

27 Bwana atakupiga kwa majipu ya Misri, na kwa bawasiri, na kwa pele, na kwa kujikuna, ambayo hupati kupoa.

28 Bwana atakupiga kwa wazimu, na kwa upofu, na kwa bumbuazi la moyoni;
Haya maombi yangu ya Leo kwa SSH,Spika wa Bunge, Watawala wote na Magenge yao ya Utekaji
 
Ndio umeandika nini? Hakuna tofauti ya serikali ya Magufuli na ya Samia Katika kulinda raia na mali zao. Serikali zote mbili zimeshindwa kupamba na utekaji wa watu, sasa Magufuli unampa credit ya nini kuhusu utekaji?
 
Amen
 
Wewe pia omba Kwa Imani yako
Sisi tunaoamini katika Mungu acha tumuombe aingilie kati huu unyama
 
Mkuu sikatai. Uko sahihi kabisa. Ila pamoja na kuwa wapenzi wa CCM, baadhi ni kwa sababu tu hawana la kufanya. Inabidi wamtumikie kafiri ili kupata mradi wao. Unajua mtu unapokuwa kwenye chain kama hiyo kujiondoa ni vigumu. Ukianza wewe, unashughulikiwa na kuondolewa na wezako wanabaki wakijilia. Nakuhakikishia kabisa leo hii kama umma wa kitanzania ukitoka kwa wingi, kuna polisi wengi watu wataacha kuwalinda watawala. Wanachokumbana nacho ni kile kile kinachowatokea wananchi. Kila mmojajapo haridhiki lakini anakuwa mwoga wa kutoka kwanza.
 
Maombi yako asiyapokee BWANA...

Ayapokee haya yangu hapa chini ,na atayapokea aaaamin aaaamin;

Eee BWANA WA MAJESHI endelea kumpa ulinzi mkuu Rais wetu Samia Suluhu Hassan na wasaidizi wake wote ,aaaamin aaaamin.

Eee BWANA WA MAJESHI nchi haisimami bila ya uwepo wa Rais ,basi kwalo ninakuomba uendelee kumsimamisha kwa kumpa siha njema ,umri mrefu ,nguvu na busara zaidi rais wetu Samia Suluhu Hassan aaamin aaaamin aaaamin[emoji7]

#Nchi Kwanza [emoji7]

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…