Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
Assalamu Aleykum
Nimemsikia Mhe. Rais, Mama Samia Suluhu akiwa anahojiwa na Mwandishi, Salimu Kikeke. Kwa kweli Maswali yamejibiwa vizuri Sana.
Nafahamu Siasa zilivyo, nafahamu mambo ya kiutawala Kwa kiasi kidogo, Kwa majibu ya Rais Samia ni wazi amejibu kwa kiwango cha juu mno.
Ingawaje amejibu kirahisi sana karibu maswali yote lakini majibu yake yalikuwa yanafungua majibu ya baadhi ya maswali ambayo angeulizwa Mbele.
Hata Kama Samia atakandiwa na mahasimu wake kuwa amejibu Kama mjinga, au ameongea uongo, au vyovyote watakavyo mwambia lakini ukweli ni kuwa amejibu Kwa kiwango kizuri cha juu kabisa. Kama ni uongo basi ni ule uongo unaoridhisha kabisa.
SSH moja ya majibu yake, hasa kwenye mikutano ya Kisiasa ameniongezea Jambo jipya ambalo nikiri kuwa sikuwa nalifahamu.
Jambo Hilo ni kuhusu Katiba ya Vyama vya Kisiasa ambapo ndani yake kuna vipengele vinavyoelezea idadi ya vikao na mikutano Kwa mwaka ambayo Chama kitapaswa kikae.
Mikutano hii Kwa vile IPO kikatiba(ya kila chama kulingana na Chama) ikiitishwa haina haja ya kuomba kibali Kwa polisi.
Hii Kwa kweli sikuwa nafahamu.
Kwa maelezo yake Kama nitakuwa nimekuelewa Sawia, alikuwa anamjibu Kikeke kuwa, Mikutano au vikao vya kichama inaruhusiwa ikiwa vimeorodheshwa ndani ya Katiba. Na Kama havijaorodheshwa basi sharti kuwepo na Kibali kutoka Polisi.
Kwa mujibu wa maelezo ya SSH anajaribu Kueleza kuwa baadhi ya Vyama vya Upinzani hutaka kufanya mikutano hovyo hovyo hata Kama vikao/mikutano hiyo haipo kikatiba(Katiba ya chama husika) na pia hawajaomba Kibali polisi.
Nikiri kuwa sikujua Jambo Hilo. Na niliona Wapinzani wanaonewa lakini Kama ni hivyo basi nilikuwa sipo Sahihi.
Lakini Kama SSH anadanganya basi Wanasheria mtanieleza kuhusiana na hoja hiyo aliyoisema Mhe. Rais.
Kuhusiana na Kesi ya Mbowe, siwezi elezea lolote isipokuwa naiachia Mahakama, ingawaje maswali ninaweza kuwa nayo, mathalan, iweje Mbowe akamatwe kipindi hiki akidai Katiba mpya na sio kipindi cha nyuma?
Ingawaje SSH ameeleza kana kwamba Tayari kulikuwepo na mchakato wa kesi hiyo na ndio maana Mbowe amejiingiza katika kudai Katiba mpya kujikinga na mshale wa kesi hiyo.
Yote tisa, mwisho ni majibu ya Mhe. Rais ni mepesi Sana lakini Yanaridhisha mno kiasi kwamba hata muulizaji anajikuta maswali mengine aliyonayo kichwani yanayeyuka.
Muhimu:. Tunataka Katiba Mpya Kwa kizazi kipya.
Ishu ya Katiba si suala la kiongozi kuamua liendelee ama liendelee. Ni takwa la kizazi kipya.
Taikon wa Fasihi
Turiani, Mvomero