Majibu ya Rais Samia Suluhu hata Kama yangekuwa uongo lakini Yanaridhisha

Majibu ya Rais Samia Suluhu hata Kama yangekuwa uongo lakini Yanaridhisha

Upinzani hawana Agenda wanayoipigania.

Ni Kama ngedere anayerukia Tawi hili na hili

Kama wangekuwa na Agenda moja wakaipigania mpaka ikakamilika huenda wangekuwa mbali.

CCM wanachoringia ni kuwa na Upinzani dhaifu sana
Huu ndio ukweli.

CCM hawaringii polisi wala Tume ya Uchaguzi, wanachoringia ni kuwa na UPINZANI DHAIFU SANA.
 
Assalamu Aleykum

Nimemsikia Mhe. Rais, Mama Samia Suluhu akiwa anahojiwa na Mwandishi, Salimu Kikeke. Kwa kweli Maswali yamejibiwa vizuri Sana.
Nafahamu Siasa zilivyo, nafahamu mambo ya kiutawala Kwa kiasi kidogo, Kwa majibu ya Rais Samia ni wazi amejibu kwa kiwango cha juu mno.

Ingawaje amejibu kirahisi sana karibu maswali yote lakini majibu yake yalikuwa yanafungua majibu ya baadhi ya maswali ambayo angeulizwa Mbele.

Hata Kama Samia atakandiwa na mahasimu wake kuwa amejibu Kama mjinga, au ameongea uongo, au vyovyote watakavyo mwambia lakini ukweli ni kuwa amejibu Kwa kiwango kizuri cha juu kabisa. Kama ni uongo basi ni ule uongo unaoridhisha kabisa.

SSH moja ya majibu yake, hasa kwenye mikutano ya Kisiasa ameniongezea Jambo jipya ambalo nikiri kuwa sikuwa nalifahamu.
Jambo Hilo ni kuhusu Katiba ya Vyama vya Kisiasa ambapo ndani yake kuna vipengele vinavyoelezea idadi ya vikao na mikutano Kwa mwaka ambayo Chama kitapaswa kikae.

Mikutano hii Kwa vile IPO kikatiba(ya kila chama kulingana na Chama) ikiitishwa haina haja ya kuomba kibali Kwa polisi.
Hii Kwa kweli sikuwa nafahamu.

Kwa maelezo yake Kama nitakuwa nimekuelewa Sawia, alikuwa anamjibu Kikeke kuwa, Mikutano au vikao vya kichama inaruhusiwa ikiwa vimeorodheshwa ndani ya Katiba. Na Kama havijaorodheshwa basi sharti kuwepo na Kibali kutoka Polisi.

Kwa mujibu wa maelezo ya SSH anajaribu Kueleza kuwa baadhi ya Vyama vya Upinzani hutaka kufanya mikutano hovyo hovyo hata Kama vikao/mikutano hiyo haipo kikatiba(Katiba ya chama husika) na pia hawajaomba Kibali polisi.

Nikiri kuwa sikujua Jambo Hilo. Na niliona Wapinzani wanaonewa lakini Kama ni hivyo basi nilikuwa sipo Sahihi.

Lakini Kama SSH anadanganya basi Wanasheria mtanieleza kuhusiana na hoja hiyo aliyoisema Mhe. Rais.

Kuhusiana na Kesi ya Mbowe, siwezi elezea lolote isipokuwa naiachia Mahakama, ingawaje maswali ninaweza kuwa nayo, mathalan, iweje Mbowe akamatwe kipindi hiki akidai Katiba mpya na sio kipindi cha nyuma?

Ingawaje SSH ameeleza kana kwamba Tayari kulikuwepo na mchakato wa kesi hiyo na ndio maana Mbowe amejiingiza katika kudai Katiba mpya kujikinga na mshale wa kesi hiyo.

Yote tisa, mwisho ni majibu ya Mhe. Rais ni mepesi Sana lakini Yanaridhisha mno kiasi kwamba hata muulizaji anajikuta maswali mengine aliyonayo kichwani yanayeyuka.

Muhimu:. Tunataka Katiba Mpya Kwa kizazi kipya.
Ishu ya Katiba si suala la kiongozi kuamua liendelee ama liendelee. Ni takwa la kizazi kipya.

Taikon wa Fasihi
Turiani, Mvomero
HUYU SAMIA NI MUONGO, ANATAKA KUTUAMBIA UCHAGUZI ULIOPITA ULIKUWA HURU NA WA HAKI? WANACHOLALAMIKA HAO WAPINZANI KUBWA ZAIDI NI KUWA NA KATIBA ITAKAYOONDOA BIASNESS KWENYE HII TUME YA UCHAGUZI YA OVYO. NDIYO WATU WATASUBIRI SEHEMU NYINGINE YA KATIBA, LAKINI HILI LA TUME HURU, WEWE SAMIA UNATAKIWA ULIFANYA SASA, HUPENDWI WEWE NA SERIKALI YAKO, KWANINI MNALAZIMISHA MPENDWE????
 
Sasa ndio maana watu tunasema kwamba wanaodai katiba wanadai kwa maslahi yao ndio maana tunaona wanapiga kelele.

Kelele iliyokuwepo ni tume huru tuuu hayo mengine ni kuzuga tu,wanakatiba mpya wasiwatie wananchi katika ajenda zao za kimaslahi aisee.
 
Rais amezungumza vizuri kweli tena kwa uwazi ulio uwazi kwamba sauli hili sio la leo lilikuwepo na bw yule yule alikuwa analifahamu fika na baadhi ya wahusika wa jambo hili walikuwepo rumamnde kwa muda mrefu tu kabla bwana yule hajakamatwa isipokuwa bw yule ni intelegent wa kutisha sana ana akili nyingi sana akaona atafanyaje suala hile alipe mlangpo au mwonekano mwingine wa ki umma zaidi akaingilia kwa kasi ya katiba mpya bahati mbaya kondoo wake hawajui haya au intelegency aliyonayo kiongozi wao katika kuwatumia vyema koondoo wake, ''Rais amesaema mahakama itatupa majawabu sahihi baada ya mahakimu na wanasheria wa pande zote mbili kukabiliana kwa kina na kuja na jawabu moja tuvute subraaaaa''
Mbowe ana Uhuru wa kufanya na kudau kitu chochote kile, kudai katiba mpya haijawahi kuwa kosa la jinai acha ujinga
 
Mimi binafsi nilihoji toka mwanzo kwamba mnataka katiba mpya ili iweje?

Sijawahi pata majibu toka kwa machadema
Muulize kikwete kwanin alihidhinisha zile ela za tume ya katiba ya warioba kuzunguka nchi zima na bunge la katiba umeuliza swali la kijinga Sana
 
Sasa ndio maana watu tunasema kwamba wanaodai katiba wanadai kwa maslahi yao ndio maana tunaona wanapiga kelele.

Kelele iliyokuwepo ni tume huru tuuu hayo mengine ni kuzuga tu,wanakatiba mpya wasiwatie wananchi katika ajenda zao za kimaslahi aisee.
We ni mjinga sana, kulikua na haja gani kuwa na bunge la katiba na kuanzisha Ile tume ya warioba ya kukusanya maoni ya wananchi juu ya katiba mpya na husu Samia naye alishiriki
 
Mwenye rasmu ya katiba iliyopendekezwa anipe ili nione kama naweza unga tela la katiba mpya
 
Mimi Mkristo na ninakubaliana na Samia
Wote wanaomsifia Samia ni Kwa sababu ya udini and nothing else , wanajaribu kumkingia kifua agombee tena 2025 japo indicator zinaonyesha worst to come!!! Kama nilimpinga Jiwe , sina cha kumsifia SSH madam Yale ya Maghufuli anayaendeleza Kwa udhabiti zaid
 
HUYU SAMIA NI MUONGO, ANATAKA KUTUAMBIA UCHAGUZI ULIOPITA ULIKUWA HURU NA WA HAKI? WANACHOLALAMIKA HAO WAPINZANI KUBWA ZAIDI NI KUWA NA KATIBA ITAKAYOONDOA BIASNESS KWENYE HII TUME YA UCHAGUZI YA OVYO. NDIYO WATU WATASUBIRI SEHEMU NYINGINE YA KATIBA, LAKINI HILI LA TUME HURU, WEWE SAMIA UNATAKIWA ULIFANYA SASA, HUPENDWI WEWE NA SERIKALI YAKO, KWANINI MNALAZIMISHA MPENDWE????

Unaweza kuwa sahihi, ndio maana nikasema hata Kama ni uongo lakini unaridhisha
 
Mambo mazuri yapi watu wamekaa miaka 60+ still wanafunzi wanakaa chini mazuri yapi ambayo hayaonekani
Kama unaamini hakuna mazuri sawa.

Mimi mazuri nayaona yamefanyika japokuwa ninatamani yafanyike zaidi,wewwe huoni mazuri yoyote yaliyofanyika ati kwa sababu tu kuna mambo mengine hayajafanyika.

Hakuna ugomvi mkuu,wewe endelea kuona mabaya,ssi wengine tutaendelea kuona mazuri.

Chaguo ni lako mkuu
 
Back
Top Bottom