Majibu ya Serikali Kuhusu Vitambulisho vya NIDA Vyenye Ukomo na Visivyo na Ukomo

Majibu ya Serikali Kuhusu Vitambulisho vya NIDA Vyenye Ukomo na Visivyo na Ukomo

Mimi kilichonishangaza!
Nakumbuka wakati wa kuandikisha kitambulisho cha Mpiga Kura kilikuwa kinatoka saa hiyo hiyo! Lakini cha NIDA kinachukua miaka!🤔🤔
Mimi nilipoteza kitambulisho cha NIDA najuta! Ni miaka 4 pamoja na kwamba nililipia na kukamilisha taratibu zote lakini wapi!
 
View attachment 2626015
SERIKALI KUANZA KUTOA ELIMU KWA WANANCHI KUHUSU VITAMBULISHO VYA NIDA VYENYE UKOMO NA VISIVYO NA UKOMO

Mbunge wa Viti Maalum anayewakilisha Wafanyakazi Nchini anayetokea Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Janejelly James Ntate ameuliza swali lililoelekezwa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kuhusu vitambulisho vya NIDA ambalo lilijibiwa na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira na Muungano) Mhe. Khamis Hamza Khamis

"Je, wale waliopewa namba za NIDA kabla ya tangazo la GN96 ya mwaka 2003 vitambulisho vyao vitatoka vikiwa na ukomo au vikiwa havina ukomo"? - Mhe. Janejelly James Ntate

"Je, Serikali imejipangaje kuleta uelewa kwa wananchi ili wajue kwamba vitambulisho vyao ambavyo vimekaribia kuwa na ukomo na ambavyo vina ukomo havitawaathiri ili kupunguza taharuki Iliyo kwa wananchi sasa?" - Mhe. Janejelly James Ntate

"Vitambulisho ambavyo vitakuja baada ya tangazo hili havitakuwa na ukomo. Vitambulisho ambavyo vitakuja na tangazo lilishatoka kabla wataendelea kwa sababu lengo la Serikali ni kuhakikisha wananchi hawakosi huduma za muhimu na vitambulisho vilivyokwisha muda vitaendelea kutumika kuwapatia wananchi huduma mpaka pale Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi itakapotoa maelekezo mengine" - Mhe. Khamis Hamza Khamis

"Wananchi watafikiwa na taaluma, kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Mheshimiwa Waziri ameshatoa tangazo kupitia TV, Radio na Magazeti. Tumeshatoa maelekezo na muda wowote tunaweza kuanza mafunzo kwa Watendaji wote wa NIDA ili waanze kuwafundisha wananchi ili wajue mchanganuo wa kipi kimekwisha ukomo, kipi hakitakwisha ukomo na kipi kitatumika" - Mhe. Khamis Hamza Khamis
MBONA MAELEKEZO YALIKWISHA TOLEWA KUWA VITAENDELEA KUTUMIKA, MNATAKA MAELEKEZO YAPI TENA!
 
Back
Top Bottom