Majibu ya TANESCO kuhusu changamoto za wateja zilizowasilishwa kupitia JamiiForums - Juni 2026

TANESCO

Official Account
Joined
Jul 12, 2014
Posts
5,210
Reaction score
2,779
MAJIBU YA TANESCO KUHUSU CHANGAMOTO ZA WATEJA ZILIZOWASILISHWA KUPITIA JUKWAA LA JAMII FORUMS

WhatsApp Image 2026-06-18 at 22.44.00.jpeg
WhatsApp Image 2026-06-18 at 22.44.01.jpeg
 
Na hapa Kenyamonta na Iramba wilaya ya serengeti mkoa wa Mara ni kwanini huwa munakatakata huu umeme kila baada ya masaa mawili bila taarifa?

Hii kero ya kuukata na kurudisha, kukata na kurudisha kila wakati bila taarifa imekuwa taabu. hakuna predictability ya kufanya shughuli za maendeleo bila kuwa na uhakika utakatika saa ngapi, kwa muda gani , na utarudi saa ngapi...

Msije kusema ni matengenezo madogo madogo au transforma, mambo hayo yote huwa yanatolewa maelezo kwa wakazi husika...
 
Wafanyakazi wa TANESCO hua wanazarau sana, mtu una hela zako unalipa kila kitu ila sasa kukuunganishia umeme hadi uwabembeleze na rushwa juu💔💔💔
 
Habari Mbabani, asante kwa kuwasiliana na TANESCO huduma kwa wateja na pole kwa changamoto hiyo, tafadhali tufahamishe namba ya ombi kwa msaada zaidi.^HN
 
Huu ujinga sasa
Yaani kwenye uzi umekimbia halafu unaanzisha uzi mwingine kwa ajili ya ufafanuzi wa changamoto 5 kati ya mamia ya changamoto watu walizozitoa
 
Habari Mbabani, asante kwa kuwasiliana na TANESCO huduma kwa wateja na pole kwa changamoto hiyo, tafadhali tufahamishe namba ya ombi kwa msaada zaidi.^HN
Samahani mkuu, nina swali tofauti na wenzangu hivi kuna hii hali ya umeme kukatika usiku kwenye majira ya saa 7 hivi au saa 8 usiku halafu unakaa km dakika 5 hivi au dakika 10 kisha umeme unarudi, hivi hii sijawahi kuelewa kunakuaga na tatizo gani usiku? Namaanisha ni kila siku na ukirudi haukatiki tena mpaka kesho tena saa 7 usiku utakata dakika 5/10 unawaka haukatiki tena mpaka kesho tena usiku muda ule ule unakata vile vile kisha unawaka mpaka mnaanza kuzoea kwamba ukifika muda huo basi TANESCO lazima wakate umeme
 
Habari, na asante kwa ujumbe wako.

TANESCO hutoa taarifa kwa wateja wake kuhusu matengenezo yaliyopangwa au hitilafu zinazoweza kusababisha kusitishwa kwa huduma ya umeme. Ili kuhakikisha taarifa zinawafikia wateja kwa haraka na kwa ufanisi, tunatumia ujumbe mfupi wa simu (SMS) pamoja na makundi ya WhatsApp yaliyogawanywa kulingana na mikoa, wilaya, kanda na maeneo mbalimbali.

Iwapo hadi sasa hupokei taarifa kuhusu huduma zetu, hususan taarifa za kusitishwa kwa huduma ya umeme, tafadhali tujulishe mkoa au wilaya unayoishi. Tutakutumia kiungo (link) cha kujiunga na kundi husika la WhatsApp, na pia tutahakikisha namba yako inaingizwa kwenye mfumo wa kupokea taarifa kupitia SMS.

Tunatumia njia zote mbili za mawasiliano ili kuhakikisha taarifa zinawafikia wateja wote, ikizingatiwa kwamba si kila mteja ana simu yenye huduma ya intaneti. Kwahiyo, kupitia kundi la WhatsApp, utaweza pia kuuliza maswali juu ya huduma zetu ili iwe rahisi kwako kujua kinachoendelea. Pole sana, Mteja wetu kwa hizi changamoto.

Asante kwa kuwasiliana nasi.
 
Habari Mbabani, asante kwa kuwasiliana na TANESCO huduma kwa wateja na pole kwa changamoto hiyo, tafadhali tufahamishe namba ya ombi kwa msaada zaidi.^HN
Habari TANESCO ukitaka kuingiza umeme eneo ambalo umeme upo ila changamoto nyumba ipo mbali kidogo na nguzo ya kupokelea umeme ni gharama kiasi gani ninatakiwa kulipia
 
Habari TANESCO ukitaka kuingiza umeme eneo ambalo umeme upo ila changamoto nyumba ipo mbali kidogo na nguzo ya kupokelea umeme ni gharama kiasi gani ninatakiwa kulipia
Habari, na asante kwa ujumbe wako.

TANESCO hutoa taarifa kwa wateja wake kuhusu matengenezo yaliyopangwa au hitilafu zinazoweza kusababisha kusitishwa kwa huduma ya umeme. Ili kuhakikisha taarifa zinawafikia wateja kwa haraka na kwa ufanisi, tunatumia ujumbe mfupi wa simu (SMS) pamoja na makundi ya WhatsApp yaliyogawanywa kulingana na mikoa, wilaya, kanda na maeneo mbalimbali.

Iwapo hadi sasa hupokei taarifa kuhusu huduma zetu, hususan taarifa za kusitishwa kwa huduma ya umeme, tafadhali tujulishe mkoa au wilaya unayoishi. Tutakutumia kiungo (link) cha kujiunga na kundi husika la WhatsApp, na pia tutahakikisha namba yako inaingizwa kwenye mfumo wa kupokea taarifa kupitia SMS.

Tunatumia njia zote mbili za mawasiliano ili kuhakikisha taarifa zinawafikia wateja wote, ikizingatiwa kwamba si kila mteja ana simu yenye huduma ya intaneti. Kwahiyo, kupitia kundi la WhatsApp, utaweza pia kuuliza maswali juu ya huduma zetu ili iwe rahisi kwako kujua kinachoendelea. Pole sana, Mteja wetu kwa hizi changamoto.

Asante kwa kuwasiliana nasi.
TANESCO umelielewa swali ?
 
Habari TANESCO ukitaka kuingiza umeme eneo ambalo umeme upo ila changamoto nyumba ipo mbali kidogo na nguzo ya kupokelea umeme ni gharama kiasi gani ninatakiwa kulipia
Utaambiwa mpaka aje mtu wa survey.

Jaribu kufanya tathmini mwenyewe nguzo ngapi zinatakiwa.

Kama ni zaidi ya moja, andaa kuanzia laki 5
 
Back
Top Bottom