Majibu ya TANESCO kuhusu changamoto za wateja zilizowasilishwa kupitia JamiiForums - Juni 2026

Majibu ya TANESCO kuhusu changamoto za wateja zilizowasilishwa kupitia JamiiForums - Juni 2026

TANESCO MPO VIZURI SANA ASANTENI KWA HUDUMA ZENU.

NIMEFURAHI SANA UWEPO WENU HUMU JUKWAANI . MI KIJANA AMBAYE NAWEZA FANYA MAAJABU NIKIPATA KIASI CHA SHILINGI MILION MOJA TU NIKAENDELEZA DUKA LANGU LA ELECTRONIC AMBAYO HIO SEKTA INAONGEZA MATUMIZI YA UMEME HAPA NCHINI..

KAMA UMEGUSWA BASI UNAWEZA NICHANGIA
Habari, Ndugu Mteja. Asante sana kwa ujumbe wako, pamoja na mawazo yako. Ni jambo zuri la kufikiria. Naomba tuipokee na kuifanyia kazi kama maoni na mapendekezo. Asante tena. ^NM
 
Mnataka location na number za simu? Sina tatizo lolote...
Hii ni kwaajili ya kuunganishwa katika group letu la huduma kwa wateja ili usikose taarifa juu ya huduma zetu mbali mbali, na pia kukuwezesha kutoa taarifa ili uhudumiwe kwa uwepesi na haraka.
 
Hii ni kwaajili ya kuunganishwa katika group letu la huduma kwa wateja ili usikose taarifa juu ya huduma zetu mbali mbali, na pia kukuwezesha kutoa taarifa ili uhudumiwe kwa uwepesi na haraka.
Nipo kwenye group zenu zote...
 
Hongereni TANESCO kwa ku - respond juu ya changamaoto za wateja wenu wa hapa Jamii Forums.
 
Hongereni kwa response, baadhi ya taasisi zinapaswa kuiga huu utaratibu wenu wa kujibu hoja za Wananchi kwa wakati..
Habari Gentlemen_ asante kwa kuwasiliana na TANESCO huduma kwa wateja na asante kwa pongezi, tafadhali endelea kufurahia huduma zetu. TANESCO tunayaangaza maisha yako.^FL
 
Na hapa Kenyamonta na Iramba wilaya ya serengeti mkoa wa Mara ni kwanini huwa munakatakata huu umeme kila baada ya masaa mawili bila taarifa?

Hii kero ya kuukata na kurudisha, kukata na kurudisha kila wakati bila taarifa imekuwa taabu. hakuna predictability ya kufanya shughuli za maendeleo bila kuwa na uhakika utakatika saa ngapi, kwa muda gani , na utarudi saa ngapi...

Msije kusema ni matengenezo madogo madogo au transforma, mambo hayo yote huwa yanatolewa maelezo kwa wakazi husika...
Habari, Ndugu Mteja.

Pole sana kwa changamoto unayoipata. Tafadhali fahamu kuwa mara tunapolazimika kusitisha huduma ya umeme kwa ajili ya matengenezo yaliyopangwa au hitilafu za ghafla, huwa tunatoa taarifa mapema pamoja na maelezo ya sababu ya usitishaji wa huduma.

Taarifa hizi hutolewa kupitia njia mbalimbali ikiwemo ujumbe mfupi wa SMS (SMS) pamoja na makundi ya WhatsApp yaliyogawanywa kulingana na maeneo.

Iwapo hujapata taarifa hizi, tunaomba radhi. Tafadhali tutumie namba yako ya WhatsApp kupitia inbox pamoja na mkoa unaoishi, na tutahakikisha tunakuunganisha kwenye makundi husika ili upate taarifa zote muhimu kuhusu huduma ya umeme katika eneo lako. ^FL
 
Kwa Huduma hii nzuri kwa wateja hakika TANESCO mpo vizuri sana
Habari nyachina asante kwa kuwasiliana na TANESCO huduma kwa wateja na asante kwa pongezi, tafadhali endelea kufurahia huduma zetu. TANESCO tunayaangaza maisha yako.^FL
 
Habari nyachina asante kwa kuwasiliana na TANESCO huduma kwa wateja na asante kwa pongezi, tafadhali endelea kufurahia huduma zetu. TANESCO tunayaangaza maisha yako.^FL
Mimi changamoto yangu ni kuwa ninadai umeme wa sh 50000 baada ya mita ya mwanzo kuharibika nikawekewa mita mpya, tangu nipeleke maombi nizaidi ya miezi miwili sasa nilifatilia nikaambiwa nisubiri kupigiwa simu mpaka leo kimya
 
Habari makoye sr, asante kwa kuwasiliana na TANESCO huduma kwa wateja na pole kwa changamoto hiyo, tafadhali tufahamishe namba yako ya mita mpya kwa msaada zaidi, ^GK
 
Habari makoye sr, asante kwa kuwasiliana na TANESCO huduma kwa wateja na pole kwa changamoto hiyo, tafadhali tufahamishe namba yako ya mita mpya kwa msaada zaidi, ^GK
Namba mpya ni 43036500924 siyo ile niliyotuma mwanzo, samahani kwa usumbufu
 
Habari, Ndugu Mteja. Tunashukuru sana kwa maoni yako. Ubarikiwe! ^NM
Kwa nini mlifanya uhuni wa kutupandishia nguzo kutoka 27000 hadi laki tatu ndani ya mita 15 wakati biashara ya umeme haina ushindani zaidi yenu?pesa mnazotukamua za wateja wote nchi nzima huwa mnazipeleka wapi?Na kwa nini hamjapunuza bei ya umeme wakati bwa wa la JNHEPP limekamilika na kuwa na umeme wa kutosha hadi kuzidi matumizi?
 
Back
Top Bottom