Majibu ya TANESCO kuhusu changamoto za wateja zilizowasilishwa kupitia JamiiForums - Juni 2026

Majibu ya TANESCO kuhusu changamoto za wateja zilizowasilishwa kupitia JamiiForums - Juni 2026

Kwa nini mlifanya uhuni wa kutupandishia nguzo kutoka 27000 hadi laki tatu ndani ya mita 15 wakati biashara ya umeme haina ushindani zaidi yenu?pesa mnazotukamua za wateja wote nchi nzima huwa mnazipeleka wapi?Na kwa nini hamjapunuza bei ya umeme wakati bwa wa la JNHEPP limekamilika na kuwa na umeme wa kutosha hadi kuzidi matumizi?
Habari Afcon kinanuka asante kwa kuwasiliana nasi kupitia ukurasa huu, tunapenda kukufahamisha kuwa gharama za umeme hazijapanda, gharama ya kuunganisha umeme vijijini kwa wateja wa njia moja ni shilingi 27,000/= na gharama za kuunganisha umeme ndani ya mita 30 kwa mteja wa njia moja kutoka kwenye miundombinu ya umeme shilingi 320,960/=,tafadhali tembelea tovuti yetu kwenye chati ya huduma kwa wateja kwa ufafanuzi zaidi na asante kwa maoni tumeyapokea.^CM
 
Ss hv kuna shida ya umeme kusumbua Yani kama unafifia alf unaongezeka.
 
Kwa Huduma hii nzuri kwa wateja hakika TANESCO mpo vizuri sana
Habari nyachina, asante kwa kuwasiliana na TANESCO huduma kwa wateja, tumepokea pongezi hizi, tafadhali endelea kufurahia huduma zetu. TANESCO tunayaangaza maisha yako.^ MY
 
Nimefanya maombi ya umeme tokea mwezi wa nne hadi sasa sijapata control namba na surveyor alishakuja kwangu. Nilifika ofisini Chanika majbu ni kwamba hakuna NGUZO. Mpaka sasa sijaunganishiwa nomba mnisaidie namba ya ombi 290426-0330
 
Habari Mpenda kazi, na asante kwa kuwasiliana nasi.

Tunaomba radhi kwa kuchelewa kukurudia juu la ombi lako, ila fahamu kuwa tunaifuatilia na bado ipo katika hatua ya wewe kutumiwa control number kwaajili ya malipo.

Ofisi husika bado inaomba uvumilivu wako, na itakutumia kwa njia ya ujumbe mfupi (SMS) kwenye simu yako.

Asante. ^FL
 
Asante. ^FLSawa
 
Back
Top Bottom